Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-30 16:04:24    
Umaalumu wa utamaduni wa sehemu ya msitu wa mawe nchini China

cri

Tamasha la vijinga la mila ya kabila la wa-yi nchini China, ambalo linafisiwa kuwa ni tamasha kubwa kabisa ya mashariki, ni tamasha kubwa ya kabila la wa-yi kwenye sehemu ya msitu wa mawe. Endapo unafanya matembezi kwenye sehemu ya msitu wa mawe kati ya mwishoni mwa mwezi Juni na mwanzoni mwa mwezi Julai, licha ya kuona mandhari nzuri ya kimaumbile ya msitu wa mawe, pia unaweza kuona shamrashamra za tamasha la mila ya kabila la wa-yi.

Kwenye ardhi hiyo watu wa kabila la wa-yi walikuwa wanafanya kazi, matambiko, kuimba na kucheza ngoma, na kuweza kuendeleza mchezo wa vijinga kuwa "tamasha kubwa maarufu kwenye sehemu ya mashariki ya dunia". Watu wengi walianza kuwafahamu wa-yi kutokana na tamasha la vijinga. Wa-yi walianza kuabudu moto toka zamani za kale. Bibi mzee mmoja anayeishi kwenye sehemu ya msitu wa mawe alituambia kuwa kila mwaka ifikapo tamasha ya vijinga, wanakijiji huwasha vijinga wakati giza inapoingia na kutembea kwenye mashamba ya mpunga.

"Tunasherehekea tamasha la vijinga kwa kunyanyua juu vijinga na kutembea kwa kuzunguka kwenye mashamba yetu ya mpunga kwa kuomba mungu aue wale wadudu waharibifu na kuleta mavuno mazuri ya kilimo."

Bibi mzee alisema kutembea kwenye mashamba na vijinga, kunaweza kuua wadudu waharibifu na kuhakikisha mavuno mazuri katika majira ya mpukutiko wa majani. Vijinga vinavyobaki vinachukuliwa kwenda nyumbani, wazee wanachoma maharage ya horsebean kwa kutumia vijinga hivyo, wakiamini kuwa watakuwa salama kabisa wakila maharage hayo yaliyochomwa. Kijana mmoja anayeitwa Ang Gui alisema, wa-yi wanaoishi kwenye sehemu ya msitu wa mawe, wanalichukulia tamasha la vijinga kuwa ni sherehe yao kubwa, wakati wa usiku wanavijiji wanaadhimisha sikukuu hiyo kwa shughuli mbalimbali usiku kucha.

"Katika sikukuu ya vijinga, wanavijiji wanatoka majumbani mwao wakiwa na vijinga, wanaamini kuwa wakifanya hivyo wanaweza kuwafukuza pepo wabaya. Katika usiku wa tarehe 24 mwezi Juni kwa kalenda ya kichina, wanakijiji wanasherehekea sikukuu hiyo kwa shughuli mbalimbali za tamasha usiku kucha, zikiwa ni pamoja na shughuli zilizofanyika mchana kama vile mchezo wa kupigana kwa maksai na mchezo wa mieleka."

Katika sikukuu ya vijinga, toka alfajiri na mapema watu wanamiminikia kwenye sehemu ya msitu wa mawe kutoka pande mbalimbali. Wakati wa adhuhuri watu wanapiga mbiu, ambapo vikundi vya vijana wavulana kwa wasichana waliovalia nguo za sikukuu za kabila la wa-yi vinaingia kwenye uwanja vikipiga ala za muziki zinazofanana na gambusi lenye nyuzi tatu huku wakirukaruka kwa furaha. Watu wa makamo wanapiga ala za muziki kwa kuambatana na muziki wa vijana kwa kutumia gambusi dogo na filimbi za mwanzi, na baadhi yao wanajitokeza kucheza 'ngoma ya wazee', mara moja uwanjani kunakuwa na furaha kubwa.

Wakati wa usiku, vijana wa kabila la wa-yi wanawasha vijinga walivyoshika mikononi na kucheza ngoma barabarani. Wageni wanaoshiriki tamasha ya vijinga, wanashikana mikono na kuimba huku wakicheza ngoma, na kila mmoja aliyeshuhudia shamrashamra hiyo huwa na furaha kubwa pia. Hapo mwanzoni tamasha la vijinga lilichukuliwa kama ni sikukuu ya kimila ya kabila la wa-yi, shughuli za maadhimisho zilifanyika kwenye kila kijiji, halafu zikaendelezwa kuwa nembo ya msitu wa mawe kutokana na maendeleo ya shughuli za utalii kwenye sehemu ya msitu wa mawe. Kila likikaribia tamasha hilo kubwa, watalii wa sehemu mbalimbali duniani humiminikia huko kushuhudia sherehe kubwa za sikukuu.

Katika siku za maadhimisho, kila sehemu za mandhari hujaa watazamaji, michezo ya mieleka na kupambana kwa maksai inafanyika wakati wa mchana. Watu wenye nguvu kubwa wanachuana, wakati maksai hodari kutoka wilaya mbalimbali wanapambana uwanjani, ambapo wakazi wengi wa makabila mbalimbali wanaimba na kucheza ngoma kwa kufuata muziki wa gambusi, licha ya hayo kuna migahawa inayouza supu za nyama ya ng'ombe na kondoo kwa wageni. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa sehemu ya msitu wa mawe bibi Zhang Yunlei alisema, utalii kwenye msitu wa mawe umekuwa wa kupendeza zaidi baada ya kuunganisha utamaduni na mila za makabila pamoja na shughuli za utalii.

"Toka miaka mingi iliyopita, utalii kwenye sehemu ya msitu wa mawe ulikuwa ni kuangalia mandhari ya kimaumbile tu. Lakini hivi sasa tumekuza maendeleo ya baadhi ya sekta zinazohusiana na mambo ya utalii. Kwa mfano, tunaunganisha utamaduni wa kikabila pamoja na utalii ili kuongeza uhai wa utalii."

Bibi Zhang Yunlei alisema baada ya kuendelezwa kwa miaka mingi iliyopita, hivi sasa utalii kwenye sehemu ya msitu wa mawe umeweka lengo la kuendeleza utalii wa kuangalia mandhari ya kimaumbile kuwa utalii wa mapumziko, kujenga sehemu ya msitu wa mawe kuifanya ifikie kiwango cha juu kabisa duniani, na kufanya sehemu hiyo iwe maarufu duniani katika mambo ya utalii. Aliongeza,

"Kazi zetu katika kipindi cha karibuni ni kama kuanzisha kwa mara ya pili shughuli za utalii, tumebuni mipango, sasa baadhi ya miradi inaendelea kutekelezwa. Kwa mfano kuunganisha utamaduni wa kikabila na shughuli za utalii, na kujenga 'mji mmoja, kijiji kimoja na kituo kimoja'."

Bibi Zhang Yunlei alisema, "mji mmoja" ni kujenga "mji wa kabila la wa-sani", tutahamisha majumba ya ofisi, hoteli za wageni na baadhi ya majengo ya michezo kutoka sehemu yenye msitu wa mawe ili kutenganisha sehemu ya mandhari na sehemu ya huduma. Licha ya hayo, tutatatua masuala yanayohusu chakula, malazi, burudani na ununuzi vitu wa wageni. Watalii wanaweza kupata vyakula mbalimbali vyepesi vya kabila la wa-yi na wa-sani kwenye mtaa wa chakula wa wa-sani: Vilevile wageni wanaweza kuona mfululizo wa kazi za utengenezaji wa vitu vya zawadi vya sekta ya utalii, ikiwemo kazi ya utarizi katika karakana za bidhaa maalumu za kikabila; Aidha sehemu ya msitu wa mawe imenuia kujenga hoteli moja ya ngazi ya nyota tano ikijifunza usanifu, uwekezaji na usimamizi wa hoteli maarufu za kisasa duniani, na kukuza uwezo wa sehemu hiyo kufikia utalii wa mapumziko kutoka kuangalia mandhari ya kimaumbile tu.

"Kijiji kimoja" ni kujenga kijiji cha kwanza cha kabila la wa-yi nchini China. Watalii wanaweza kujiburudisha kwa furaha ya watu wa kabila hilo na kufahamu vizuri utamaduni wa kabila la wa-yi. Kwa upande mwingine tutahimiza maendeleo ya uchumi wa huko kwa shughuli za utalii na kutekeleza lengo la kusaidia sekta ya kilimo kwa shughuli za utalii.

"Kituo kimoja" ni kujenga "kituo cha michezo". Baada ya kufanya matembezi kwenye sehemu ya msitu wa mawe, watalii wanaweza kujiburudisha kwa mila na desturi ya wakazi wa huko na kuimba na kucheza ngoma pamoja na vijana wa kabila la wa-yi.

Msitu wa mawe ukiwa mabaki ya maumbile ya dunia na urithi wa binadamu, sasa unajitahidi kuwa moja ya sehemu maarufu sana za utalii duniani, tunaamini kuwa watalii waliotoka sehemu mbalimbali za dunia, watapata furaha.

Idhaa ya kiswhili 2007-07-30