Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-30 18:52:02    
Manyani adimu waishio nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wauawa

cri

manyani wanne wakubwa waishio katika mbuga ya wanyama pori ya Virunga ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hivi karibuni waliuawa kwa kupigwa risasi. Tukio la kuuawa kwa Sokwe hao ni tofauti ya ujangili wa kawaida, mara hii miili ya sokwe iliachwa bila kuchukuliwa, hivyo watu husika wanashuku kuwa, huenda kitendo hicho kinahusiana na kundi la upinzani au kundi la wahalifu wa kukata miti kiharamu. Na kuwaua manyani hao kunaonekana kama ni kutoa onyo kwa wahifadhi mazingira wa huko.

Shirika la habari la Marekani CNN na gazeti la Times la Uingereza tarehe 27 Julai yalitoa habari zikisema, kati ya manyani wanne waliouawa mmoja alikuwa manyani dume mwenye mgongo wa rangi ya fedha, ambaye alikuwa kiongozi wa familia yake. Walinzi walisema, manyani hao wanne waliuawa usiku wa tarehe 22 Julai. Ofisa husika wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO alisema, familia ya manyani hao waliouawa ilikuwa na manyani 12, licha ya hao wanne, hivi sasa walinzi wamewapata wengine 6, manyani mmoja jike na mtoto wake bado hawajapatikana.

Manyani wa milimani wanaishi katika sehemu ya mpakani kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, sehemu ambayo inawavutia watalii wengi. Kuwatafuta manyani kwa kutembea ni kivutio maarufu sana cha utalii wa viumbe huko, kila mtalii anatozwa dola za kimarekani mia kadhaa kwa ajili ya kutembea ndani. Hicho ni chanzo kikubwa cha mapato kwa wakazi wa huko. Taarifa iliyotolewa na UNESCO inasema, kuuawa kwa manyani huenda kutaleta pigo kubwa kwa maendeleo ya viumbe na uchumi ya sehemu zilizo karibu na mbuga ya wanyama pori ya Virunga ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kudumu kwa miaka mingi, sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa imedhibitiwa na maofisa wafisadi wa huko na makundi ya upinzani. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilishindwa kuchukua hatua mwafaka kuzuia uwindaji haramu na kuwalinda wanyama pori adimu hasa manyani. Wataalamu wa hifadhi ya mazingira wamesema, mauaji hayo hayakufanywa na majangili, kama wangekuwa ni majangili basi wangechukua miili ya manyani kwa ajili ya chakula au ngozi.

Watu wanachukulia kuwa, kuuawa kwa manyani hao ni kwa ajili ya kuwapa onyo wahifadhi mazingira, ambao wanapinga vitendo vya kukata miti kwa ajili ya kupata kuni. Baada ya serikali ya Rwanda kutangaza kupiga marufuku ukataji miti, mahitaji ya kuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanaongezeka kwa haraka. Mhifadhi wa mazingira Bw. Lick alieleza wasiwasi yake kuwa, maofisa wafisadi wa huko wanajishughulisha biashara ya kuni. Hivyo kundi la uhalifu la kukata miti haramu huenda ndio wauaji.

Uchunguzi uliofanywa mwaka 2004 ulionesha kuwa, katika mbuga ya Virunga ya wanyama pori ya taifa na sehemu ya volkano ya karibuni kwa jumla wanaishi manyani 380, ambao wanachukua zaidi ya nusu ya manyani pori duniani. Shirika la UNESCO tarehe 27 Julai lilisema kuwa, litatuma kikundi cha wachunguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchunguza sababu halisi ya kuuawa kwa manyani hao, na kuwaunga mkono wahifadhi mazingira.

Wachunguzi wa Congo wamefanya msako katika sehemu ya kusini ya mbuga ya Virunga, na shirika la mimea na wanyama la kimataifa limesema, wahusika wameimarisha doria katika mbuga hiyo, na kuanzisha vituo vya ulinzi ili kuzuia kuuawa kwa wanyama pori wengine.

Idhaa ya kiswahili 2007-07-30