Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-31 19:45:10    
Jeshi la China laanza kupeleka askari kwenye luteka ya kimataifa kwa njia ya ndege

cri

Kikosi cha kwanza cha jeshi la China kinachoshiriki kwenye luteka ya kimataifa ya mapambano dhidi ya ugaidi inayoitwa "Jukumu la Amani?2007" tarehe 31 Julai kimeanza kupelekwa kwa ndege aina ya IL-76.

Imefahamika kuwa kazi zote za kupeleka askari wa jeshi la China zinatekelezwa kwa ndege za IL-76 za jeshi la China, vikosi vitatu vya China vitapelekwa kwa ndege mara 18.

Luteka ya mapambano dhidi ya ugaidi inayoitwa "Jukumu la Amani?2007" itafanyika kuanzia tarehe 9 Agosti hadi tarehe 17 katika mkoa wa Xinjiang nchini China na jimbo la Chelyabinsk nchini Russia.