Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-01 10:44:14    
Ofisi za ubalozi wa China katika nchi za nje zafanya tafrija za kuadhimisha miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China

cri

Tarehe 1 Agosti ni siku ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kuundwa kwa Jeshi la ukombozi wa umma la China. Ofisi za ubalozi wa China nchini Ufaransa, Serbia, na Peru kwa nyakati tofauti zimefanya tafrija za kuadhimisha siku hiyo. Ofisa wa kijeshi wa ubalozi wa China nchini Ufaransa Jenerali Zhang Changtai tarehe 31 Julai kwenye tafrija iliyofanyika huko Paris aliwaelezea wageni mafanikio ya Jeshi la ukombozi wa umma la China, ambapo makamanda wa jeshi la Ufaransa waliohudhuria tafrija hiyo walifurahia mawasiliano yanayozidi kuimarika siku hadi siku kati ya majeshi mawili ya China na Ufaransa, na kuutakia maendeleo zaidi ya uhusiano wa kimkakati kati ya China na Ufaransa kwenye sekta mbalimbali.

Kwenye tafrija za kuadhimisha miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China zilizofanyika kwenye ofisi za ubalozi wa China nchini Serbia, Peru, Antigua na Barbuda, na Ecuador, maofisa wa kijeshi wa ubalozi wa China katika nchi hizo vilevile waliwajulisha wageni hali kuhusu kuundwa, kukua na kuendelezwa kwa Jeshi la ukombozi wa umma la China, ambapo wageni waliohudhuria tafrija walipongeza mafanikio ya jeshi la China, na pande mbili mbili zimeeleza matumaini ya kukuza zaidi mahusiano na ushirikiano kati ya majeshi mawili mawili na nchi mbili mbili.