Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-01 10:45:48    
Mkutano wa maadhimisho ya miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China wafanyika Beijing

cri

Mkutano wa kuadhimisha miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China na wajumbe wa mashujaa na hodari wa kuigwa wa jeshi la China umefanyika tarehe 1 Agosti kwenye Jumba la mikutano ya umma la Beijing, ambapo viongozi wa chama na serikali ya China Hu Jintao, Wu Bangguo, Wen Jiabao na wengineo wamehudhuria Mkutano huo. Mkutano huo umeendeshwa na waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao, na katibu mkuu wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni rais wa China na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi Bwana Hu Jintao ametoa hotuba muhimu.

Tarehe 1 Agosti mwaka 1927, Chama cha Kikomunisti cha China kiliongoza mapinduzi huko Nanchang mkoani Jiangxi, kusini ya kati ya China, ambapo jeshi lililoongozwa na Chama cha kikomunisti cha China peke yake likazaliwa.