Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-03 19:34:04    
Ushirikiano kati ya China na Afrika una manufaa halisi kwa waafrika

cri

Kwenye ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwezi Novemba mwaka jana, rais Hu Jintao wa China alitoa hatua nane za kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Afrika. Waziri wa mambo ya nje wa China wa wakati huo Bw. Li Zhaoxing alisema hatua hizo zilizotolewa na China zitakuwa na manufaa halisi kwa waafrika.

Waziri mteule ambaye pia ni katibu mkuu wa chama tawala cha Nigeria PDP Bw. Ojo Maduekwe alipohojiwa na waandishi wa habari wa China alisema, baada ya kufanyika kwa mkutano wa wakuu mjini Beijing, watu mbalimbali wa Nigeria wana matumaini makubwa ya kuendelezwa kwa uhusiano wa kirafiki na ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Nigeria, anaona kuwa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika kunaambatana na maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili. Alisema serikali za China na Nigeria zimesaini na zitasaini makubaliano kadhaa ya ushirikiano, tunataka makubaliano hayo yaweze kutekelezwa mapema iwezekanavyo.

Bw. Maduekwe alisema Nigeria ni nchi kubwa ya Afrika ya magharibi yenye watu wengi sana, ina uwezo mkubwa wa kuendeleza uchumi na kuwa na fursa nyingi za uwekezaji. Anatumai kuwa wafanyabiashara wengi zaidi wa China watawekeza nchini Nigeria. Pia alivikaribisha viwanda vya China kujenga sehemu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara nchini Nigeria.

Bw. Maduekwe pia alizungumzia mradi wa reli ya kisasa ya Nigeria inayojengwa na kampuni ya China, alisema mradi huo unajengwa kutokana na mkopo wa China, na unaonesha kuwa nchi hizo mbili zinaimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi. Alisisitiza kuwa, mradi huo ni muhimu kwa Nigeria, kwa kuwa Nigeria ni nchi kubwa za Afrika ya magharibi yenye makabila mengi zaidi, kujenga reli inayounganisha sehemu mbalimbali nchini Nigeria kutasaidia Nigeria kuimarisha Umoja na utulivu wa taifa. Aidha, reli hii itahimiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya sehemu zilizoko kwenye kando mbili za reli hii.

Naibu meneja wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Bw. Chen Xiaoxing alifahamisha kuwa, reli hiyo yenye mrefu wa kilomita 1315 itaunganisha mji wa Lagos na Abuja, na itajengwa kwa kutumia kigezo cha China cha teknolojia ya reli. Mradi huo utaisaidia Nigeria kuunda mfumo wa kwanza wa viwanda vya reli, na kuleta fursa nyingi za ajira katika sehemu zilizoko kwenye kando mbili za reli. Bw. Chen Xiaoxing alikadiria kuwa wataajiri wafanyakazi elfu 50 wa Nigeria .

Kampuni za China siyo tu zinapeleka fedha na teknolojia barani Afrika, bali pia zinazisaidia nchi za Afrika kuwaandalia watu wenye ujuzi. Konsela anayeshughulikia mambo ya uchumi na biashara wa ubalozi wa China nchini Nigeria Bw. Huang Jie alisema China itazisaidia nchi za Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi kwa njia mbili, kwanza serikali ya China kutenga fedha ili kuandaa semina za mafunzo kwa ajili ya maofisa na mafundi wa Afrika, aidha kampuni za China kutumia fursa ya ujenzi wa miradi yao barani Afrika kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa huko. Alisemamatokeo ya hali halisi yameonesha kuwa, teknolojia ya China inafaa kwa nchi zinazoendelea na ni rahisi kwa wafanyakazi wa nchi hizo kujifunza.

Waandishi wa habari walipotembelea sehemu za ujenzi wa mradi wa utoaji wa maji wa ziwa la Viktoria nchini Tanzania waliona kuwa, kampuni ya Afrika ya mashariki ya China Civil Engineering Construction ilipotekeleza mradi huo, ilikuwa inatoa mafunzo kwa wafanyakazi zaidi ya mia moja, kiwango cha teknolojia cha wafanyakazi kadhaa kati yao kimefikia au kimekuwa zaidi ya ngazi ya nne.

Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, baada ya mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana, kazi ya kutekeleza ahadi za China kwa nchi za Afrika nchini Nigeria na Tanzania zilikuwa zinaendelea kwa utaratibu. Nchini Nigeria, China ilitoa dawa za kukinga na kutibu ugonjwa wa malaria na kuanzisha ujenzi wa shule za vijijini. Nchini Tanzania, China imeanzia kazi ya kuisaidia nchi hiyo kujenga kituo cha matibabu na upasuaji wa moyo na mradi wa shule za vijijini. Aidha Tanzania imetoa ombi la kutumia mkopo wenye nafuu wa China kutekeleza mradi wa mtandao wa Cable, hivi sasa mazungumzo kuhusu mradi huo yanaendelea.

Ofisa wa wizara ya maji wa Tanzania alisema, katika miaka ya hivi karibuni China imekuwa inachukua hatua halisi ili kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii kwa nchi za Afrika, reli ya TAZARA ni mfano mzuri kabisa. Alisema kuwa wanaamini ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika utazinufaisha nchi za Afrika na wananchi wake.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2006, thamani ya uwekezaji wa China wa moja kwa moja barani Afrika imefikia dola za kimarekani bilioni 6.64, hili ni ongezeko la mara saba kuliko mwaka 1999. Thamani hiyo imechukua asilimia 9 ya thamani ya jumla ya uwekezaji wa China katika nchi za nje.

Takwimu zinaonesha kuwa, katika miaka 50 iliyopita, China ilitekeleza miradi ya utoaji misaada zaidi ya 800 barani Afrika, 137 kati ya hiyo ni ya kilimo, na 133 ni ya miundo mbinu. Miradi hiyo pia inahusu utengenezaji wa bidhaa, utengenezaji wa chakula na sekta nyingine. Kuanzia mwaka 2000, kampuni za China zilifanya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita elfu sita, reli zenye urefu wa kilomita elfu tatu, na vituo vinane vya kuzalisha umeme barani Afrika. Kampuni za China zimeanzisha miradi zaidi ya 100 ya biashara ya utengenezaji wa bidhaa, na asilimia 70 ya uwekezaji wa miradi hayo ilitumika kwa ajili ya kununua vifaa na kugharamia ujenzi wa majengo ya viwanda barani Afrika. Mwaka 2006, asilimia 31 ya thamani ya mapato ya kandarasi zilizotekelezwa na kampuni za China katika nchi za nje zilitoka barani Afrika.