Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-01 19:25:23    
Gazeti la Renminribao la China latoa makala ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi wa umma wa China

cri

Tarehe mosi Agosti ni siku ya kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi wa umma wa China. Siku hiyo gazeti la Renminribao la China limetoa makala ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi wa umma wa China.

Makala hiyo inasema, baada ya juhudi za miaka 80 iliyopita, jeshi la ukombozi wa umma wa China limepata maendeleo makubwa, kiwango cha kufanya jeshi liwe la kisasa kimeinuliwa zaidi, na uwezo wa kutekekeza majukumu pia umeendelea kuimarishwa, China imefuata njia ya ujenzi wa jeshi la umma inayolingana na hali halisi ya China, na kuwa na mfumo kamili wa kanuni na mikakati yenye umaalum wa kichina kuhusu kujenga na kutawala jeshi, China pia imeandaa wataalamu wengi hodari wa kijeshi, na kuunda nadharia tatu za jeshi, yaani fikra ya Mao Zedong kuhusu mambo ya kijeshi, fikra ya Deng Xiaoping kuhusu ujenzi wa jeshi katika zama mpya na fikra ya Jiang Zemin kuhusu ulinzi wa taifa na ujenzi wa jeshi.