Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-02 16:06:57    
Siku moja ya askari mzee Bw. Fan Daquan

cri

Kila asubuhi Saa 12 asubuhi, askari Fan Daquan na wenzake wanaanza mazoezi ya siku nzima. Wao ni askari wa kufanya utengenezaji wa maderaya ya idara moja ya jeshi la ukombozi wa umma la China, kila siku kabla ya kupata kifungua kinywa, wanafanya mazoezi ya mwili na gwaride, utaratibu huo haubadiliki hata kama kukiwa na upepo au mvua kubwa.

Kazi ya askari hao wa jeshi la nchi kavu ni kukarabati na kuvitunza vifaru na amotkaa zote ili kuhakikisha vifaa hivyo vinaweza kuwasaidia askari kumaliza mazoezi yote na kutumika kwenye mapigano. Naibu mkurugenzi wa idara ya siasa ya kikosi hicho Bw. Zhao Xinjun alisema, Bw. Fan Daquan ana umri wa miaka 32 tu, lakini alijiunga na jeshi miaka 13 iliyopita, na yeye ni mmoja kati ya askari hodari wa kikosi hicho.

"Bw. Fan Daquan anastahili kuwa fundi hodari wa kutengeneza amotokaa, anajua vizuri uwezo, muundo na msingi wa amotokaa zote. Baada ya majaribio ya miaka mingi, ufundi wake na sifa yake ya kijeshi imefikia kiwango cha juu, na anaweza kutatua matatizo ya kawaida kwa urahisi."

Bw. Fan Daquan alizaliwa kwenye kijiji cha mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, yeye si mrefu, lakini anaonekana ni mwenye ukakamavu kuliko wenzake, kutokana na maisha ya jeshini ya miaka mingi.

Baada ya kifungua kinywa askari hao wanaanza kufanya mazoezi ya kijeshi. Kwa askari hao wa kutengeneza amotokaa, uwanja wa vita na uwanja wa mazoezi uko kwenye uwanja wa kutengeneza amotokaa. Huko kuna amotokaa zenye matatizo mbalimbali, pamoja na magari ya kuondoa mabomu, na kusafirisha askari, vifaru na magari ya uongozi wa mapigano Bw. Fan Daquan aliwaongoza askari wenzake kufanya utengenezaji wa gari moja. Alisema:

"Hii ni amotokaa ya kisasa ya uongozi wa mapambano uwezo wake ni kushirikiana na kikosi kufanya mapambano na mazoezi. Tunapaswa kuhakikisha kuwa magari hayo yanafanya kazi bila matatizo wakati wa mapambano au wakati wa mazoezi."

Kwenye medani ya vita ndani ya amotokaa ya uongozi wa mapambano wanakaa makamanda, hivyo amotokaa hiyo inakuwa shabaha kubwa ya kushambuliwa na maadui.

Bw. Fan Daquan alisema kazi ya kutengeneza amotokaa si rahisi kama kazi ya kutengeneza gari la kawaida, kunahitaji ufundi wa kiwango cha juu na pia kunahitaji kasi. Alisema:

"kwa kikosi kimoja, muda ni muhimu sana kwenye medani ya vita, ikiwa amotokaa likiharibika wakati wa mapambano, tunapaswa kulitengeneza ndani ya muda mfupi ili irudi kwenye mapambano haraka iwezekenavyo."

Aidha kutengeneza amotokaa pia kunahusiana na usalama, kama hutafanya kazi kwa makini basi unaweza kuumia vibaya, Bw. Fan Daquan alipoona kifaru kwa mara ya kwanza alishangazwa sana, na hata hakuthubutu kukisogelea. Katika kipindi cha mapumziko askari hao wanapenda kufanya mashindano madogo, wanafanya mashindano ya kukimbia kwa kuzungusha magurudumu ya vifaru, kikundi kitakachokwenda kwa kasi kabisa na kufuata mstari basi kitashinda.

Kwa askari hao mashindano hayo si mchezo tu, kwenye vita vya halisi wanapaswa kubeba vifaa vizito kwenda kutengeneza vifaru. Kama walivyo askari walioko kwenye mapambano, nao wanapaswa kukabiliana na hali ngumu, hivyo wanapaswa kuwa na nguvu na sifa ya kijeshi ya kiwango cha juu. Bw. Fan Daquan alisema:

"kwenye vita, askari wanapaswa kuwa na nguvu. Kwa askari wetu wa kutengeneza vifaru, kama wakikimbia wakiwa na vifaa na hawana nguvu za kutosha, basi hawawezi hata kukaribia sehemu yenye vifaru vilivyoharibika.

Askari wa kutengeneza amotokaa pia wanapaswa kushiriki kwenye mashindano ya kijeshi, ikiwemo kulenga shabaha, kutupa makombora, kukimbia kwa kilomita 3, kuingia duara la moto, kuruka nguvu za chuma na kujiokoa, baada ya kumaliza mashindano hayo, askari hao wanapaswa kukimbia kwenda kwenye sehemu iliyopangwa na kutengeneza amotokaa. Ili kumaliza mashindano hayo, Bw. Fan Daquan anahitaji dakika 20 tu, na amewahi kupata nafasi ya kuongoza katika mashindano ya kikosi hicho. Alisema:

Katika kambi ya jeshi, maisha ya askari ya kila siku ni ya kawaida, kufanya mazoezi asubuhi, kulala baada ya chakula cha mchana, na kuendelea kufanya mazoezi au kujifunza ujuzi wa aina mbalimbali wakati wa alasiri na usiku wanaweza kupata nafasi ya kufanya michezo. Kwa askari katika kipindi cha amani, wanapaswa kuchukua jukumu la kuokoa wakati wa maafa, kuboresha mazingira na kufanya ujenzi wa miundo mbinu. Bw. Fan Daquan alisema anapenda maisha hayo ya kawaida ya kijeshi, katika miaka 13 iliyopita kwenye kambi ya jeshi, alijifunza kutengeneza amotokaa na kutumia kompyuta, na alipata cheti cha ushiriki.

Baada ya mazoezi na mafunzo ya siku moja, askari hao wanarudi kambini kwao. Kambi yao ni ya kawaida na inafuata utaratibu. Kwenye kambi hiyo Bw. Fan Daquan si msimamizi wa askari hao tu, bali pia ni kaka yao. Bw. Ma Haofeng ameishi pamoja na Bw. Fan Daquan kwa miaka miwili, yeye anamheshimu sana, alisema: "

"mkuu wetu wa kikiosi ana ustadi mzuri wa kutengeneza amotokaa, na pia anatilia maanani maisha yetu, wakati nilipojiunga na kikosi hiki sikujua kufua nguo, alinifundisha.

Wakati wa mapumziko Bw. Fan Daquan anapenda kucheza kwenye kompyuta yake, yeye pia ana kamera ya aina mdogo na hutumia kamera hiyo kupiga filamu fupi kuhusu maisha ya wenzake na amekuwa mpiga picha kwenye kikosi hicho. Kila mwaka askari kadhaa wanaostaafu kutoka kwenye kikosi hicho, wanamwomba kuwasaidia kupiga filamu za kumbukumbu.

Kila siku kabla ya kulala, Bw. Fan Daquan anawapigia simu mke wake na mtoto wake mwenye umri wa miaka 5 walioko kwenye maskani yake mkoani Sichuan, na kusikilia sauti zao. Kwa kuwa yeye ni mume na pia ni baba, yeye na mke wake na mtoto wake wameishi sehemu tofauti kwa muda mrefu na hukutana kwa muda mfupi, anasikitishwa na hali hiyo kila mara.

Saa tatu na nusu usiku baada ya amri ya kuzima taa, Bw. Fan Daquan na askari wenzake wanakwenda kulala kwa wakati. Siku hadi siku, wao ni wanajeshi katika kipindi cha amani, ingawa wao ni watu wa kawaida lakini wanashikilia jukumu lao na kuona fahari.

Idhaa ya kiswahili 2007-08-02