Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-02 19:33:54    
Makao makuu ya upande wa China ya jeshi litakaloshiriki kwenye luteka ya pamoja ya "Jukumu la Amani-2007" yafanya maandalizi

cri
Makao makuu ya upande wa China ya jeshi litakaloshiriki kwenye luteka ya pamoja dhidi ya ugaidi ijulikanayo kama "Jukumu la amani-2007" itakayoshirikisha majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai inafanya maandalizi kwa ajili ya luteka hiyo na kupata maendeleo mapya.

Mwongozaji mkuu wa luteka hiyo wa upande wa China Bw. Xu Qiliang aliongoza idara ya waongozaji kufanya ukaguzi kuhusu kazi ya makao makuu ya mapigano ya upande wa China, na matokeo ya ukaguzi huo yameonesha kuwa makao makuu ya China yameongeza tena uwezo wa kuongoza mapigano baada ya kufanya mazoezi kwa mwezi mmoja.

Mazoezi ya makao makuu ya pande mbalimbali za luteka ya pamoja yatafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 16 mwezi Agosti.