Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-02 19:39:49    
Vikosi vya jeshi la ukombozi wa umma la China vilivyoko Hongkong na Makau vyasherehekea miaka 80 ya Jeshi la China

cri

Tarehe 1 Agosti ni siku ya kuundwa kwa Jeshi la ukombozi wa umma la China, siku hiyo vikosi vya jeshi hilo la China vilivyoko Hongkong na Makau kwa nyakati tofauti vilifanya tafrija ya maadhimisho ya miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China.

Makamanda wa vikosi hivyo vilivyoko Hongkong na Makau walipotoa risala walisema, vikosi vilivyoko Hongkong na Makau vitaendelea kufuata kwa makini sheria za msingi za Hongkong na Makau, na sheria kuhusu vikosi vilivyoko kwenye mikoa hiyo miwili, kufanya vizuri mambo ya ulinzi wa Hongkong na Makau na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kulinda ustawi na utulivu wa mikoa hiyo miwili.