Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-02 19:41:00    
Viongozi wa kamati kuu ya kijeshi ya China na wajumbe wa mashujaa na hodari wa kuigwa wa jeshi la China washerehekea pamoja maadhimisho ya miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China

cri

 

Viongozi wa kamati kuu ya kijeshi ya China pamoja na wajumbe wa mashujaa na hodari wa kuigwa wa jeshi la ukombozi wa umma la China usiku wa tarehe 1 Agosti hapa Beijing walisherehekea pamoja siku ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kuundwa kwa Jeshi la ukombozi wa umma la China. Naibu mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi Bwana Guo Boxiong na waziri wa ulinzi Bwana Cao Gangchuan walihudhuria Mkutano huo.

Naibu mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi Bwana Xu Caihou alidhihirisha kuwa, Jeshi la ukombozi wa umma la China ni jeshi la umma ambalo limewaandaa mashujaa wengi. Katika miaka 80 iliyopita, mashujaa wengi na idara nyingi za watangulizi walijitolea mhanga, kufanya juhudi kubwa zenye taabu na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya ujenzi na maendeleo ya jeshi hilo la umma.