Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-02 19:41:43    
Vikosi vya upande wa China vyaanza kukaa kwenye Kijiji cha makambi ya Luteka ya pamoja ya "Jukumu la amani la mwaka 2007"

cri

Vikosi vya upande wa China vinavyoshiriki kwenye Luteka ya pamoja ya "Jukumu la amani la mwaka 2007" tarehe 1 Agosti vilianza kukaa kwenye Kijiji cha kambi ya luteka hiyo.

Maofisa na askari karibu 200 wa vikosi vya jeshi la nchi kavu na jeshi la anga la China wametangulia kukaa kwenye Kijiji cha kambi ya luteka. Aidha, kikosi cha helikopta cha jeshi la China pia kimefika kwenye sehemu itakapofanyika luteka nchini Russia.

Tarehe 1 Agosti ni siku ya maadhimisho ya miaka 80 ya Jeshi la ukombozi wa umma la China, maofisa na askari wa China walisherehekea siku hiyo kwenye kambi za jeshi la nchi ya nje. Usiku wa tarehe 31 Julai, upande wa Russia ulianda tamasha kwa ajili ya vikosi vya jeshi la China kuadhimisha miaka 80 ya jeshi la China.