Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-06 18:41:15    
Umoja wa Asia ya kusini mashariki umekuwa nguvu ya kikanda isiyopuuzika kwenye jukwaa la kimataifa

cri

Tarehe 8 Agosti mwaka huu itakuwa siku ya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuundwa kwa Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki. Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa mambo ya Asia na Pasifiki katika idara ya utafiti wa masuala ya kimataifa Bwana Shen Shishun alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, Umoja wa Asia ya kusini mashariki umekuwa nguvu ya kikanda isiyopuuzika kwenye jukwaa la kimataifa. Tokea Umoja wa Asia ya kusini mashariki uanzishwe mwaka 1967 mpaka sasa, umoja huo umekuwa na nchi 10 wanachama badala ya nchi 5 wanachama wa mwanzoni. Bwana Shen Shishun alisema:

"umuhimu na hadhi ya umoja huo inaimarishwa siku hadi siku. Nyaraka mbili za "Taarifa ya kuanzishwa kwa Umoja wa Asia ya kusini mashariki" na "Mkataba wa urafiki na ushirikiano wa nchi za Asia ya kusini mashariki" zimekuwa kanuni za uelekezaji wa uhusiano kati ya nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki, ambazo zimeufanya umoja huo uendelezwe siku hadi siku. Baada ya kupata maendeleo katika miaka ya hivi karibuni, umoja huo umejitokeza duniani kwa sura yake nzuri iliyo ya kuzifungulia mlango nchi za nje, kufanya mazungumo na mawasiliano na nchi zenye mifumo tofauti na utamaduni tofauti, kutafuta maoni ya pamoja wakati wa kuweka kando migongano, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana na nchi nyingine".

Nchi za Umoja wa Asia kusini mashariki nyingi ni nchi wastani na nchi ndogo, nchi hizo zinatilia maanani sana "kushika njia ya ushirikiano kwa kujiendeleza". Bwana Shen alisema :

"hivi sasa mchakato wa utandawazi wa uchumi wa Asia ya mashariki chini ya kundi la Asia ya kusini mashariki bado uko nyuma kuliko sehemu nyingine duniani, lakini sehemu hiyo inakabiliwa na fursa nzuri ya maendeleo. Kwanza Umoja wa Asia ya kusini mashariki unaimarisha siku hadi siku ujenzi wake wenyewe. Kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, huenda itapitishwa katiba ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki. Kupitishwa kwa katiba hiyo ni jambo kubwa. Hivi sasa Umoja wa Ulaya unajadili katiba ya Umoja wa Mataifa. Kama Umoja wa Asia kusini mashariki unaweza kutunga na kupitisha katiba yake mapema kuliko Umoja wa Ulaya, hakika katiba hiyo itasukuma mbele zaidi maendeleo ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki; tena hali ya hivi sasa ya kimataifa na kikanda zote zinasaidia maendeleo ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki".

China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki zilianzisha uhusiano wa mchakato wa mazungumzo mwaka 1991. Bwana Shen alisema:

"baada ya maendeleo ya miaka 16, China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki zimeona kuwa uhusiano kati yao ni uhusiano wa kirafiki, hivyo uaminifu wa kisiasa umeimarishwa, ambapo viongozi wa pande hizo mbili wanatembeleana mara kwa mara. Aidha ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye sekta ya usalama umeongezwa kidhahiri, na zimefanya ushirikiano mkubwa zaidi katika sekta za uchumi na biashara na kupata mafanikio kemkem".

Bwana Shen alisema katika miaka ya hivi karibuni, mawasiliano kati ya China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki kwenye sekta za jamii na utamaduni yamepata mafanikio makubwa. Tangu kusainiwa kwa "Kumbukumbu za maelewano kati ya Jamhuri ya watu wa China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki kuhusu ushirikiano wa kiutamduni" mwaka 2005, shughuli za maingiliano kati ya pande hizo mbili kwenye sekta za jamii na utamaduni zimeongezeka zaidi. Bwana Shen alisema:

"jambo linalostahili kutajwa ni kuwa mwaka jana Mkutano wa wakuu wa China na nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki ulifanyika huko Nanning, nchini China, ambapo washiriki wa Mkutano walifanya majumuisho ya mafanikio yaliyopatikana katika miaka 15 iliyopita, na kupanga mpango kabambe wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki".

Idhaa ya Kiswahili 2007-08-06