Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-08 16:46:11    
Mapishi ya kuchemsha doufu kwa mvuke ndani ya majani ya yungiyungi

cri

Mahitaji:

Doufu gramu 300, nyama ya kuku gramu 30, uyoga gramu 10, uyoga mweusi gramu 10, yai moja, vipande vya paja la ash la nguruwe gramu 10, majani ya yungiyungi, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, vipande vya vitunguu maji na tangawizi kila kimoja gramu 5, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, wanga wa pilipili manga kijiko kimojra, siki kijiko kimoja, mchuzi wa sosi vijiko viwili, mharadali kijiko kimoja

Njia:

1. kata kata doufu iwe kama iliyosagwa, saga nyama ya kuku. Kata uyoga na uyoga mweusi viwe vipande vipande. Koraga yai halafu washa moto mimina mafuta kwenye sufuria, mimina yai lililokorogwa kwenye sufuria likaange. Halafu lipakue na vikata liwe vipande vipande.

2. koroga doufu, nyama ya kuku, vipande vya paja la ash la nguruwe, uyoga, chumvi, sukari, vipande vya vitunguu maji na tangawizi, mafuta ya ufuta, wanga wa pilipili manga, siki, mchuzi wa sosi na mharadal, halafu weka kwenye majani ya yungiyungi, weka vipande vya yai na uyoga mweusi. Washa moto tena mimina maji kwenye sufuria weka majani ya yungiyungi kwenye sufuria chemsha kwa mvuke kwa dakika 10, ipakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.