Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-09 15:41:33    
Walinzi wa amani wa China walioko nchini Liberia

cri

China ni moja ya nchi wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Tangu mwezi Januari mwaka 1992 hadi hivi sasa, China imetuma wanajeshi zaidi ya 6,000 kushiriki kwenye shughuli 15 za kulinda amani zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Bw. Yu Changzhong ni daktari wa kijeshi wa China. Mwezi Februari mwaka jana alitumwa kwenda Liberia, kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa China kinachotekeleza majukumu ya kulinda amani nchini humo. Daktari Yu alieleza hisia zake alipofahamishwa kuwa anaweza kushiriki kwenye shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, akisema  "Wakati huo nilikuwa na furaha, lakini pia nilikuwa na wasiwasi kidogo."

Wasiwasi wake ulitokana na hali mbaya ya usalama nchini Liberia na kutokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu baadhi ya magonjwa yanayotokea katika ukanda wa ikweta, vile vile aliona lugha ni moja ya tatizo kupata mazoezi ya kujenga mwili na mafunzo ya lugha ya Kiingereza na mambo ya kijeshi kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja, daktari Yu Changzhong ni madaktari wenzake 42 wa China walipitia mtihani.

Daktari Yu alisema "Kwenye mazoezi na mafunzo ya zaidi ya 30, tulikuwa tunafanya maandalizi mazuri kuhusu mambo mengi. Wanajeshi waliowahi kushiriki kwenye shughuli za ulinzi wa amani nchini Liberia walituelezea hali ya usalama ya huko, majukumu tunayobeba, na tulifanya mazoezi yanayolingana na mahitaji ya majukumu yetu. Kwa jumla nilikuwa na imani kubwa kabla ya kufunga safari."

Mwezi Aprili mwaka 2006, daktari Yu Changzhong na madaktari wenzake 42 wa China walipelekwa hadi Liberia, na kuanza kufanya kazi kwenye hospitali moja ya Umoja wa Mataifa. Pamoja na kutoa huduma za matibabu kwa walinzi wa amani wenzake, hospitali hiyo pia iliwavutia watu wengi wa Liberia. Daktari Yu alielezea jinsi yeye na madaktari wenzake walivyofanikiwa kumwokoa mgonjwa mahututi. Alisema "Asubuhi ya siku moja, tulikuwa tunakula chakula cha asubuhi. Mjamzito mmoja mwenye umri wa miaka 18 alipelekwa kwenye hospitali yetu. Yeye alikuwa amepoteza damu nyingi. Ilikuwa inatubidi tufanye kila tuwezalo kumwokoa. Kutokana na jitihada za muda wa karibu saa 8, tatizo la kutoa damu kwa mjamzito huyo lilidhibitiwa na yeye alizaa mtoto wa kiume salama usalimini."

Kikosi cha madaktari wa kijeshi wa China kilisifiwa sana na watu wa Liberia kutokana udaktari hodari na moyo wa dhati wa kuwahudumia wagonjwa. Daktari Yu alisema walipokamilisha majukumu na kukaribia kurudi nyumbani mwezi Desemba mwaka jana, walisifiwa sana na wenyeji. Alisema  "Tulipofika uwanja wa ndege, tuliwakuta marafiki zetu, baadhi ya wagonjwa tuliowahi kuwahudumia, baadhi ya wenyeji na maofisa wa Umoja wa Mataifa, wao walikuwa wamefika uwanja wa ndege kutuaga. Maofisa wa Liberia walisema walinzi wa amani wa China hususan madaktari wa China, wametoa mchango mkubwa kwa afya ya watu wa Liberia."

Kutokana na mafanikio ya kikosi cha madaktari wa kijeshi wa China katika kutekeleza majukumu ya kulinda amani nchini Liberia, madaktari hao walipewa medali na Umoja wa Mataifa.

Pamoja na madaktari wa kijeshi, China pia inawapelekea askari wahandisi nchini Liberia, ambao wanashughulikia ujenzi na ukarabati wa barabara. Naibu mkuu wa kikosi cha askari wahandisi Bw. Chen Dajun alisema "Ni vigumu sana kukarabati barabara ya hapa, kwani sehemu kubwa ya udongo wa hapa ni matope na mchanga, ikinyesha mvua na barabara kupitwa na magari, inasababisha matope mengi."

Kutokana na jitihada za askari wahandisi, hivi sasa barabara za udongo nchini Liberia zimeimarika sana, ambapo magari yanaweza kukimbia kwa kasi ya kilomita 60 hadi 80 kwa saa, lakini zamani kasi hiyo ilikuwa kilomita 30 kwa saa. Mkuu wa mkoa wa Grand Gedeh Bw.Christopher Bailey aliwashukuru sana wanajeshi wahandisi wa China kutokana na mchango mkubwa waliotoa kwa ajili ya ukarabati wa mkoa huo.

Alisema "Tunakushukuru. Sisi na askari wahandisi wa China tumejenga uhusiano mzuri, tunawapenda na kuwachukulia kama wao ni jamaa zetu."

Kikosi cha mawasiliano cha China kinashughulikia kazi zote za mawasiliano kwa ajili ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Liberia. Karibu kila siku wanajeshi wa kikosi hicho wanasafirisha vitu na vifaa. Kazi hiyo ni muhimu sana kwani kuchelewa kunaweza kusababisha watu mia kadhaa hata zaidi ya elfu moja kukosa maji ya kunywa, chakula au nishati.

Siku moja kikosi hicho kilipeleka vitu hadi kituo kimoja kilichoko umbali wa kilomita 500. Njiani wanajeshi walikumbwa na tukio fulani, na safari hiyo iliwachukua siku 5 kurudi kwenye kambi. Hata hivyo walikamilisha kazi kwa kutegemea chakula na maji yanayoweza kuwatosheleza kwa siku mbili tu.

Kikosi cha mawasiliano cha China kilisifiwa na Umoja wa Mataifa kutokana na kufuata nidhamu kwa makini. Amrijeshi wa jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Liberia Bw. C. I. Obiakor alisema "Wanajeshi wa China wametoa mchango mkubwa sana. Ninawaambia wenzangu mara kwa mara kwamba, jeshi letu nzima litashindwa kutekeleza jukumu bila kuwepo kwa kikosi cha mawasiliano cha China."

Mbali na Liberia, walinzi wa amani wa China pia wanajitokeza katika nchi na sehemu nyingine kama vile Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Sudan na Lebanon. Hivi sasa wanajeshi wa China wapatao 1,500 wanatekeleza majukumu ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa katika sehemu 9 duniani.

Idhaa ya kiswahili 2007-08-09