Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-16 16:53:58    
Siku nyingine ya umwagaji damu yatokea nchini Iraq

cri

Tarehe 14 kwenye maeneo kadhaa wanakoishi wafuasi wa dhehebu la Yazidi kaskazini mwa mkoa wa Neineva ilitokea milipuko minne ya mabomu yaliyofichwa ndani ya gari ilitokea kwa mfululizo na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 250 na wengine 300 kujeruhiwa. Haya ni mauaji makubwa kabisa tangu ya vita vya Iraq kutokea mwaka 2003.

Taarifa ya polisi ya Iraq inasema kuwa milipuko hiyo ilitokea karibu kwa wakati mmoja na aina za milipuko ni sawa, na yote ilitokea kwenye maeneo wakakoishi wafuasi wa dhehebu la Yazidi, kwa hiyo milipuko hiyo ilitokea kwa kupangwa. Taarifa pia inasema wakazi kwenye maeneo hayo wote ni Wakurd ambao ni wafuasi wa dhehebu la kale la Yazidi, kwa hiyo mashambulizi hayo yalifanywa kwa lengo wazi. Milipuko hiyo ilisababisha nyumba nyingi kubomoka na watu wengi walizikwa chini ya vifusi, kazi ya kuokoa na kuhesabu watu walioathirika ni ngumu. Hadi sasa hospitali mbalimbali mkoani humo zinaendelea kupokea majeruhi, na idadi ya vifo huenda itaongezeka.

Milipuko hiyo imezishtusha serikali za Marekani na Iraq na jumuyia ya kimataifa. Tarehe 15 Ofisi ya rais Jalal Talabani wa Iraq ilitoa taarifa ikitaka watu wa Iraq waungane na kupinga njama ya kufarakanisha taifa, na siku hiyo serikali ya Iraq ilipiga marufuku ya kutembea katika maeneo yote kaskazini mwa Iraq. Kadhalika kamanda mkuu wa jeshi la Marekani nchini Iraq Bw. David Petreus na balozi wa Marekani nchini humo Bw. Ryan Croker siku hiyo pia walitoa taarifa kulaani milipuko hiyo ya "kinyama" inayowalenga watu wasio na hatia. Msemaji wa jeshi la Marekani nchini Iraq Bw. Christopher Garver alisema, ingawa bado hawajaweza kuthibitisha nani ni muuaji, lakini kutokana na milipuko yenyewe kuwa mikubwa, kundi la Al-Qaida ndio linashukiwa zaidi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 15 alitoa taarifa akilaani sana milipuko hiyo mfululizo na kusema kwamba sababu yoyote isingekuwa kisingizio cha kuwaua raia wa kawaida. Nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya, Ureno, tarehe 15 usiku ilisema nia ya milipuko hiyo ni kuchochea migogoro kati ya madhehebu nchini Iraq, kwa hiyo Umoja wa Ulaya unataka watu wa madhehebu yote wafuate njia ya amani na kuacha vitendo vyote vya umwagaji damu.

Wachambuzi wanaona kuwa hii ni siku nyingine iliyojaa damu nchini Iraq, raia wengi wa kawaida waliuawa bila hatia, msiba huo unatokana na vita vilivyoanzishwa na Marekani bila idhini ya Umoja wa Mataifa.

Kwanza vita vya Marekani dhidi ya Iraq vimeharibu usuluhisho wa kisiasa na kimaslahi uliokuweko katika kipindi cha utawala wa Saddam, na vimeongeza migongano ya kikabila. Baada ya serikali ya Saddam kupinduliwa, dhehebu la Suni liliokuwa na nafasi ya uongozi katika serikali ya Iraq limepuuzwa na limepoteza madaraka, mali na hadhi, badala yake watu wa dhehebu ya Shia na wa Kurd waliokuwa wakipuuzwa katika utawala wa Saddam wamekuwa watawala wa kisiasa. Mabadiliko hayo yamesababisha chuki na uhasama kati ya makabila na madhehebu ya kidini nchini Iraq na kusababisha hali mbaya ya usalama.

Pili, Serikali ya Iraq ni serikali ya bendera tu, na haina uwezo wowote wa kutawala. Vita vya Marekani dhidi ya Iraq vimeharibu vyombo vya taifa, vimevunja jeshi la polisi, jamii ya Iraq imezama katika hali ya vurugu. Serikali kadhaa za Iraq zilizoundwa kwa juhudi za Marekani zote zinakuwa na maisha mafupi kutokana na kukosa uungaji mkono. Serikali ya sasa ingawa iliundwa kwa kura, lakini serikali hiyo ni zao la kurudi nyuma kwa makundi tofauti, ndani ya serikali hiyo tofauti kati ya makundi zinaendelea kutokea, hali kama hiyo imedhoofisha vibaya uwezo wa serikali hiyo. Hivi sasa serikali ya Bw. Nuri Al-Maliki imekuwa inakabiliwa na hatari ya kuvunjika kutokana na kujiondoa kwa dhehebu la Suni na madhehebu mengine, na inashindwa kudhibiti hali ya nchi.

Tatu, Sababu mbili za Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iraq zote zimethibitishwa kuwa si kweli. Vita bila sababu vingeweza kupata ushindi, lakini ushindi huo haudumu na utasababisha misiba isiyo na mwisho. Jeshi la Marekani lenye askari zaidi ya laki moja nchini Iraq na kufanya misako mingi isiyohesabika, ingawa ni pigo kwa watu wenye silaha wanaopinga Marekani, lakini pamoja na pigo hilo, watu hao wamesababisha vifo vya raia wengi wa kawaida, mbegu za chuki zimepandwa mioyoni mwa watu wa Iraq. Wachambuzi wanaona kuwa siku ya usalama haitapatikana, kama jeshi la Marekani litaendelea kuwepo nchini Iraq.

Idhaa ya kiswahili 07-08-16