Mkutano wa 7 wa Baraza la wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ulifanyika tarehe 16 huko Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan. Rais Hu Jintao wa China na viongozi wengine wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo walihudhuria Mkutano huo na kusaini "Mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai' na nyaraka nyingine muhimu.
Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa mambo ya Ulaya ya mashariki, Russia na Asia ya kati katika Idara ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China Bwana Chen Yurong alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alidhihirisha kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, mafanikio makubwa na maendeleo dhahiri yamepatikana katika ushirikiano kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwenye sekta za siasa, uchumi na utamaduni. Kusainiwa kwa "Mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai' kumefungua ukurasa mpya muhimu wa maendeleo ya jumuiya hiyo. Akisema:
"nyaraka zilizosainiwa kwenye mkutano huo zimeonesha kuwa, Mkutano huo una umuhimu mkubwa katika mchakato wa maendeleo ya jumuiya hiyo. Aidha Mkutano huo umetia nguvu mpya ya uhai kwa maendeleo ya siku za baadaye ya jumuiya hiyo na ushirikiano kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwenye sekta mbalimbali".
"Mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai' uliosainiwa kwenye Mkutano huo uliwavutia watu zaidi. Mkataba huo ulipendekezwa na rais Hu Jintao wa China kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo uliofanyika mwaka jana. Bwana Chen alisema, mkataba huo utaufanya uhusiano wa ujirani mwema na uaminifu, mshikamano na ushirikiano kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo uendelezwe kwenye kiwango kipya, na kufungua ukurasa mpya muhimu kwenye historia ya maendeleo ya jumuiya hiyo. Akisema:
"Mkataba huo uliotungwa kwa kuhimizwa na upande wa China ulikubaliwa na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo, kwani mkataba huo uliokuwa mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano kati ya pande mbili mbili umeinuka kuwa mkataba wa pande nyingi wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano wa muda mrefu, hakika una umuhimu wa kihistoria kwa maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Hivyo mkataba huo, si kama tu ni mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye Mkutano wa wakuu wa Bishkek wa jumuiya hiyo, bali pia ni mkataba wa alama ya umuhimu wa kipindi katika mchakato wa maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai".
Bwana Che alidhihirisha kuwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai inalingana na maslahi ya pamoja ya China, Russia na nchi za Asia ya kati katika mambo ya siasa, usalama na uchumi. "Mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai' umethibitisha kisheria nia ya kudumisha urafiki na amani kizazi kwa kizazi waliyonayo wananchi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo, ambao hakika utatia nguvu kubwa ya kusukuma mbele maendeleo ya jumuiya hiyo. Bwana Chen alisema:
Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai imepata mafanikio makubwa ya kuwavutia watu macho, hii imeonesha kuwa jumuiya hiyo ni jumuiya ya kimataifa ya kanda hiyo. Nguvu ya mshikamano na nguvu ya uhai ya jumuiya hiyo vitahimiza jumuiya hiyo isonge mbele siku hadi siku, kutekeleza vizuri majukumu yake ya kimsingi ya kulinda usalama wa kikanda na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa kikanda, hakika jumuiya hiyo itaendelea kwenye kipindi kipya na kuwa na mustakabali mpya.
|