Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-20 20:39:49    
Nchi tatu za Amerika ya kaskazini zatumai kuharakisha mchango wa utandawazi wa uchumi wa kikanda

cri

Mkutano wa 3 wa siku mbili wa "wenzi wa ushirikiano wa nchi za Amerika ya kaskazini kuhusu usalama na ustawi" unatazamiwa kufunguliwa tarehe 20 Agosti huko Chateau Montebello ya Quebec ya kaskazini nchini Canada, ambapo rais George Bush wa Marekani, rais Felipe Calderon wa Mexico na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper watajadili kwa pamoja masuala ya nguvu ya ushindani duniani, usalama wa vyakula na bidhaa, nishati endelevu, usimamizi wa nishati na usalama wa kikanda.

Wachambuzi wanaona kuwa wakati wa Mkutano huo, wakuu hao watatu wataweza tu kusisitiza nia yao ya kisiasa ya kuimarisha ushirikiano, na hawataweza kuchukua hatua kubwa kuhusu masuala mbalimbali, kwani ingawa nchi hizo tatu zimeona kuwa zinategemeana kwa kiasi fulani, na zote zina matumaini ya kuharakisha mchakato wa utandawazi wa uchumi wa kanda ya Amerika ya kaskazini, lakini kutokana na kukosa sera ya uratibu, hivyo zikitaka kutimiza utandawazi bado zitafanya juhudi kwa muda mrefu. Zaidi ya hayo kwa kuwa Marekani itafanya uchaguzi wa rais mwakani, hakuna muda mrefu kwa Bw Bush kuendelea kuwepo madarakani, ndiyo maana katika muda huo hakuna uwezekano kwa Marekani kufanya mabadiliko makubwa kuhusu suala la uchumi wala suala la wahamiaji. Na suala la usalama wa mipakani na ukosefu wa vitega uchumi kwenye ujenzi wa miundo mbinu pia ni sababu kubwa ya kukwamisha utandawazi wa uchumi wa kanda hiyo.

Kwenye sehemu ya mipaka kati ya Marekani na Mexico siku zote kuna tatizo kubwa la uuzaji wa dawa za kulevya na tatizo la usalama. Mwanzoni mwa mwaka huu, Mexico ilianzisha kampeni kubwa ya kupambana na uhalifu wa dawa za kulevya, lakini chini ya vitendo vya kimabavu vilivyofanywa na wauza dawa za kulevya, polisi wa Mexico walipata hasara kubwa ya vifo na majeruhi. Katika hali hiyo, rais Calderon wa Mexico anataka kupata uungaji mkono na misaada kutoka Marekani na Canada. Hivi sasa ombi hili la Calderon limeitikiwa na Marekani, Marekani imeahidi kutoa misaada ya vifaa na zana na kuisaidia Mexico kuwaandaa mafundi. Hivyo rais Bush na rais Calderon wakihudhuria Mkutano watajadili mipango halisi ya utoaji misaada. Kwa kuwa suala la dawa za kulevya limekuwa tishio kwa pande hizo mbili, hivyo pande hizo mbili zitakuwa na maoni mengi ya pamoja kuhusu suala hilo.

Suala la wahamiaji ni suala lingine linalofuatililwa na pande mbili Marekani na Mexico. Wahamiaji wa Mexico nchini Marekani wanachukua nafasi kubwa, ili kulinda maslahi ya wahamiaji wao nchini Marekani, serikali ya Mexico inapaswa kuzingatia vizuri suala hilo. Lakini mwezi Juni mwaka huu, bunge la Marekani lilifuta tena muswada wa mageuzi kuhusu mambo ya wahamiaji, hii ikakwamisha mageuzi mapya ya Marekani kuhusu mambo ya wahamiaji. Tena Marekani inajenga ukuta wa utenganishaji kwenye mipaka kati ya nchi hizo mbili, hatua hii imezidisha migongano kati ya nchi hizo mbili kuhusu suala la wahamiaji. Hivyo suala la wahamiaji hakika litajadiliwa zaidi na marais wa nchi hizo mbili kwenye Mkutano wa wakuu wa Chateau Montebello, lakini si rahisi kwa pande mbili kupata maoni ya pamoja kuhusu suala hilo. Rais Calderon aliwahi kusema, hatua ya bunge la Marekani itaongeza hatari na hali isiyo ya usalama kwenye mipaka kati ya Marekani na Mexico.

Aidha nchi tatu za Marekani, Mexico na Canada pia zitajadili nguvu ya ushindani wa kiuchumi ya kanda ya nchi hizo. Nchi hizo tatu zilikuwa na mikwaruzano mikubwa ya biashara, lakini hivi sasa mbele ya maendeleo ya uchumi wa China, nchi hizo tatu zimetambua kuwa zinapaswa kuimarisha ushirikiano ili kuongeza nguvu zao za ushindani katikati uchumi wa dunia nzima.

Lakini Mkutano huo umesababisha upinzani wa watu nchini Canada. Tarehe 19 watu wapatao zaidi ya elfu moja huko Ottawa walifanya maandamano ya kupinga Mkutano huo, watu hao wanaona kuwa Mkutano huo hauna hali ya uwazi. Na pia wanapinga vita vya Iraq na vita vya Afghanistan, na kuyataka majeshi ya Marekani na Canada yaondoke kutoka kwenye medani za vita. Aidha vyama vingi vya Canada vinapinga Marekani na Canada kufanya ushirikiano katika maliasili ya maji na nishati.