Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-21 16:47:30    
Ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu waingia kipindi cha utekelezaji

cri

Tarehe 27 mwezi Julai, "Baraza la pili la ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu" lilifungwa huko Nanning, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, China. Wajumbe waliohudhuria baraza hilo walifanya majadiliano kuhusu "sehemu ya biashara huria ya ghuba ya Pan-Beibu na China-Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki", "utaratibu wa ushirikiano wa ghuba ya Pan-Beibu, maendeleo ya viwanda na uungaji mkono wa kifedha" na "ushirikiano wa mawasiliano, bandari, usafirishaji wa bidhaa na utalii wa ghuba ya Pan-Beibu". Wajumbe hao waliona kuwa, ushirikiano wa uchumi wa ghuba ya Pan-Beibu umeingia katika kipindi cha utekelezaji kutoka kipindi cha maandalizi, na katika siku za usoni ni lazima kuharakisha utekelezaji wa hatua mbalimbali za ushirikiano.

Ghuba ya Beibu ni ghuba inayozungukwa na ardhi za China na Vietnam pamoja na kisiwa cha Hainan cha China. Mwaka 2002, mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi ulioko kaskazini ya ghuba ya Beibu ulipanga kuanzisha "eneo la kiuchumi la ghuba ya Beibu" unaoundwa na mikoa mitatu ya Guangxi, Guangdong na Hainan ya China na baadhi ya mikoa ya Vietnam. Mwaka 2006, mkoa wa Guangxi ulitoa wazo la "ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu", ambalo lilipanua eneo la ushirikiano wa uchumi la ghuba ya Beibu hadi Malaysia, Singapore, Indonesia, Philippines na Brunei.

Naibu spika wa bunge la umma la China Bw. Jiang Zhenghua, ambaye alifanya utafiti wa kina kuhusu ushirikiano wa ghuba ya Pan-Beibu kwa mara nyingi alipohojiwa alisema, mpango wa ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu uliotolewa mwaka jana, hadi sasa umekubaliwa na viongozi wa China na nchi husika za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki, na sasa umeingia katika kipindi cha utekelezaji. Alisema,

"Viongozi wa nchi za Vietnam, Malaysia, Singapore, Indonesia, na Philippines wameeleza wazi kuunga mkono ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu, na wamefikia maoni ya pamoja kuhusu ushirikiano kwenye sekta husika na miradi mbalimbali. Miradi mingi ya ushirikiano imeanza kutekelezwa, ambayo imeufanya ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu uwe ushirikiano kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki. Tumeufanya ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu kuwa sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki, na kuuweka katika mkakati wa kujenga sehemu ya biashara huria kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki, ili uwe jambo jipya linalofuatiliwa katika ushirikiano mpya wa sehemu kwenye msingi wa nchi Kumi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki na China."

Alisema serikali ya China inatilia maanani sana ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu, na imeuweka ushirikiano huo katika mkakati wa maendeleo ya China, na viongozi wa China pia walitoa maagizo muhimu mara kwa mara kuhusu ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu.

Bw. Jiang Zhenghua alipendekeza kuwa, katika siku za usoni nchi mbalimbali husika za ghuba ya Pan-Beibu zinapaswa kuunda jumuiya ya kimataifa ya uratibu, ili kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa ushirikiano wa ghuba ya Pan-Beibu, ambao unahusika na msingi, njia na hatua za utekelezaji wa ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu, ili kuhimiza maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi wa sehemu hiyo.

Katibu wa kamati ya chama cha kikomunisti cha China cha mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang la Guangxi Bw. Liu Qibao pia anaona kuwa, ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu baada ya kukubaliwa na serikali ya China na nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki, kazi zinazofuata ni kuhimiza kwa hatua halisi, na jambo muhimu ni kuunda utaratibu wa ushirikiano.

Sekta muhimu za ushirikiano wa ghuba ya Pan-Beibu ni pamoja na miundo mbinu ya mawasiliano, bandari, usambazaji wa bidhaa, utalii, maliasili ya baharini na nishati. Mkuu wa benki ya maendeleo ya China aliyehudhuria baraza hilo Bw. Chen Yuan alisema, mitaji ni sharti muhimu la kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda, hivyo ili kuhimiza ujenzi wa miundo mbinu mikubwa ya ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu, katika siku za usoni ni lazima kuunda jukwaa la uwekezaji na ukusanyaji wa mitaji la ghuba ya Pan-Beibu, ili kuimarisha nguvu za uungaji mkono wa kifedha. Alisema,

"Ninapendekeza kuunda Umoja wa benki za kanda ya ghuba ya Pan-Beibu, ambao unaundwa na mabenki ya nchi mbalimbali za sehemu hiyo, ili kutoa huduma za fedha kwa maendeleo ya kikanda katika pande tatu. Kwanza ni kuhimiza sehemu hiyo kuunda ushirikiano na mabenki ya kimataifa; pili ni kuimarisha mawasiliano na utumiaji wa pamoja wa habari, kuunda idara ya miradi ya Umoja wa benki; tatu ni kufanya ushirikiano wa miradi mikubwa ya msingi unaoshirikisha na kunufaisha pande nyingi. Ujenzi wa Umoja wa benki utatoa njia ya kifedha yenye ufanisi kwa nchi mbalimbali za sehemu za ghuba ya Pan-Beibu kukabiliana na changamoto."

Imefahamika kuwa Benki ya maendeleo ya China siku zote inatilia mkazo kuunga mkono maendeleo ya ghuba ya Beibu. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni, benki hiyo iliahidi kutoa mikopo ya Yuan za RMB bilioni 24.8 kwa sehemu ya kiuchumi ya ghuba ya Beibu ya mkoa wa Guangxi. Aidha Benki ya maendeleo ya China pia ilituma kikundi cha kazi kwenye nchi mbalimbali za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki, kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu, na kuunga mkono maendeleo ya viwanda vya nchi hizo duniani.

Naibu mkuu wa benki ya maendeleo ya Vietnam Bw. Dao Van Chien alidokeza kuwa, Vietnam inafurahishwa na ushirikiano wa kiuchumi wa ghuba ya Pan-Beibu, na inapenda kufanya ushirikiano na benki za China katika sekta hiyo.

"Tunatumai kushirikiana na makampuni mbalimbali makubwa ya China, hasa katika sekta ya ujenzi wa miundo mbinu. Tunatumai kuimarisha ushirikiano na benki ya maendeleo ya China katika ujenzi wa miundo mbinu ya sehemu maskini ya Vietnam, au miradi ya Vietnam ya uuzaji bidhaa kwa nje."

Naibu mkuu wa benki ya maendeleo ya Asia Bw. Charles Lawrence Greenwood alidokeza kuwa, katika miaka miwili ijayo, benki hiyo itatoa mikopo yenye dola za kimarekani milioni 400 ili kusaidia ujenzi wa miundo mbinu ya Guangxi, ili kuhimiza maendeleo ya kasi ya ushirikiano wa ghuba ya Pan-Beibu.

Idhaa ya kiswahili 2007-08-21