Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-22 15:28:14    
Mapishi ya kamba-mwakaje na uyoga

cri

Mahitaji

Kamba-mwakaje gramu 400, mafuta gramu 30, uyoga gramu 70, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, ute wa yai, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, pilipili hoho moja, wanga vijiko viwili, chembachembe za kukoleza ladha nusu ya kijiko.

Njia

1. osha kamba-mwakaje, koroga pamoja na ute wa yai, mvinyo wa kupikia, chumvi na wanga. Kata pilipili hoho iwe vipande. Kata uyoga uwe vipande.

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia kamba-mwakaje kwenye sufuria korogakoroga, tia vipande vya uyoga, pilipili hoho, halafu tia chumvi, sukari, chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, mimina maji ya wanga, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.