Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-27 11:03:00    
Tamasha la kimataifa la washairi lafanyika nchini China

cri

Tamasha la kwanza la kimataifa la washairi limefungwa hivi karibuni kwenye Ziwa Qinghai, ziwa ambalo lipo kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet, kaskazini magharibi mwa China. Katika tamasha hilo washairi kutoka nchi 34 wakiwa pamoja na washairi wa China, walighani mashairi yanye mada ya "Binadamu na Maumbile, Dunia Yenye Mapatano".

Mnaosikia ni utenzi uitwao "Shujaa Gesar" ambao umekuwa ukisimuliwa kwa miaka mingi katika mikoa ya Qinghai na Tibet. Huu ni utenzi unaomsifu shujaa Gesar wa kabila la Tibet katika zama za kale. Washairi zaidi ya 300 walishiriki kwenye tamasha hilo na katika siku chache zilizopita walisikia wenyeji walivyoimba utenzi huo katika kijiji kimoja cha Watibet.

Tamasha hilo lilifunguliwa tarehe 7 Agosti kwenye Ziwa Qinghai. Hilo ni tamasha la kwanza la kimataifa la washairi lililofanywa na China, Shirikisho la Washairi la China na serikali ya mkoa wa Qinghai zinatumai kulifanya tamasha hilo la washairi liwa maarufu duniani.

"Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet ni sehemu inayowavutia sana washairi. Katika sehemu hiyo washairi wanaweza kuona mambo mengi ya ajabu ambayo hawatasahau maishani mwao. Mshairi na mhakiki mashuhuri Bw. Shu Cai ni mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo, anasema,

"Mada hii ni ya maana sana, ni mada ambayo inawakutanisha washairi wa nchi kumi kadhaa baada ya wao kuacha tofauti zao, huu ndio uhusiano kati ya binadamu na maumbile. Katika historia sanaa inayoeleza zaidi uhusiano mzuri kati ya binadamu na maumbile ni mashairi. Tamasha hili ni kubwa kuliko tamasha la kimataifa nililoshiriki barani Ulaya kwa idadi ya washairi na kiwango chake. Niliona washairi kadhaa wasioweza kuona kutoka Mexico, nilifurahi sana."

China ni nchi yenye washairi wengi. Tangu karne ya 7 hadi 13 mashairi ya kale yalikuwa yanastawi sana, walijitokeza mashauri kama Li Bai, Du Fu, Su Shi, Li Qingzhao na washairi wengine walijitokeza wakati huo. Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita wakati China ilipoanza mageuzi na kufungua mlango, kutokana na kuhamasishwa na hali mpya ya kijamii washairi vijana walijitokeza kwa wingi. Lakini kadiri uchumi unavyoendelea, na hasa kutokana na athari ya biashara na utandawazi duniani, fikra za kuzingatia pesa zimeenea, na utamaduni wa Kimagharibi unaolenga kujipatia faida haraka umeingia nchini China, fasihi yakiwemo mashairi imedidimia. Baada ya karne mpya kuanza hali hiyo imekuwa inabadilika pole pole. Katibu mkuu wa Shirikisho la Washairi la China Bw. Zhang Tongwu anaona kuwa si China au katika nchi za nje, mashairi hayawezi kuwa kama utamaduni wa kawaida. Anasema,

"Baada ya kuingia karne ya 21, hali ya mashairi imeanza kustawi, siku hizi matamasha ya kusoma mashairi yapo katika sehemu nyingi za China, kila mwaka napokea mashairi zaidi ya mia tano kutoka sehemu mbalimbali nchini. Haifai kuona kwamba mashairi yanaweza kupokelewa na watu wote kama utamaduni wa kawaida. Naamini mashairi nchini China hakika yatastawi."

Bw. Zhang Tongwu aliongeza, miaka 30 imepita tangu China ilipoanza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, itikadi ya Wachina imeanza kurudi kwenye utamaduni wake wa jadi. "Elimu ya utamaduni wa jadi" ikiwa pamoja na utafiti wa falsafa, fasihi na historia imetiliwa mkazo katika nyanja ya elimu. Kuhusu fasihi, mashairi ambayo yanafaa kueleza hisia kwa maneno machache yanazidi kupendwa na wasomaji wengi. Imefahamika kuwa hivi sasa kuna washairi zaidi ya milioni moja wanaoandika mashairi mara kwa mara, na tovuti za washairi na wapenda mashairi nchini China hazipungui 300. Washairi waliozaliwa katika miaka ya 60, 70 na 80 ya karne iliyopita walijitokeza na kuwa na ufanisi mkubwa.

Tamasha hilo licha ya kuwa mkusanyiko mkubwa wa washairi, pia ni fursa nzuri ya mawasiliano kati yao. Mshairi kutoka Venezuela, Bw. Juan Gaviria alisema,

"Hii ni fursa nzuri kwangu kuwasiliana na washairi wa nchi mbalimbali. Tunatoka kutoka sehemu tofauti duniani, lakini sote tuko katika dunia moja na tunanufaika na maumbile kwa pamoja, hii ni mada nzuri ya tamasha hili."

Kusoma mashairi ni ajenda muhimu katika tamasha hilo. Washairi wote walikabidhi mashairi waliyoandika kwa ajili ya tamasha hilo kwa kamati ya maandalizi, kati ya mashairi hayo, shairi lililoandikwa na mshairi Petros Mastoris wa Ugiriki ni tofauti na mengine. Alisema, michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 itafanyika katika mji wa Beijing, hii ni michezo inayotukuza amani na masikilizano duniani, alisoma shairi lake liitwalo "Olimpia 2008"

Wakati wa tamasha hilo la kimataifa, washairi walikwenda vijijini na kutembelea mbuga za malisho na kwenye ukingo wa mto Huanghe wakijionea mandhari nzuri ya maumbile, na kwenye ukingo wa Ziwa Qinghai walisikiliza muziki wa simfoni na walisaini "Taarifa ya Tamasha la Kimataifa la Washairi la Ziwa Qinghai".

Mwisho wa taarifa inasema turudishe heshima kwa maumbile, turudishe uhuru kwa maisha, turudishe heshima kwa ustaarabu na turudishe upendo kwa dunia, na mashairi yarudishwe kwenye maisha ya binadamu.

Idhaa ya kiswahili 2007-08-27