Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-27 11:55:45    
Korongo wenye utosi mwekundu wa Zhalong

cri

Hifadhi ya mazingira ya maumbile ya Zhalong ni moja ya sehemu muhimu zenye ardhi oevu katika dunia yetu, hifadhi ya Zhaolong ina eneo la hekta laki 2.1. Katika hifadhi hiyo inaota mimea mingi ya aina ya matete na kuwa na samaki na kamba wengi, hivyo ni mahali pazuri sana kwa ndege kuishi. Mfanyakazi wa hifadhi hiyo Bw. Wang Kun alisema,

"Kwa nini Zhalong inajulikana duniani? Kwanza, ni kwa kuwa sehemu hiyo ya ardhi oevu inachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa nchini China na barani Asia, na inachukua nafasi ya nne duniani. Pili, sura ya ardhi ya sehemu hiyo ni ya asili na ya kale kabisa, haijaathiriwa na shughuli za binadamu kutokana na kuwa mwamko wa watu wa huko kuhusu hifadhi ya ardhi oevu umeinuka."

Hifadhi ya Zhalong ni moja ya sehemu muhimu wanazoishi korongo wenye utosi mwekundu. Kundi kubwa kabisa la korongo wenye utosi mwekundu duniani wanaishi kwenye sehemu hiyo, hivyo sehemu hiyo inasifiwa kuwa ni maskani ya korongo wenye utosi mwekundu. Mwongoza watalii dada Liu Na alisema, korongo wenye utosi mwekundu pia wanaitwa korongo wa peponi, kuna hadithi moja inayozungumzia uhusiano kati ya asili ya ardhi oevu ya Zhaolong na korongo wa peponi.

"Dragon mdogo mweusi na dragon mdogo mweupe mwovu waliotoka Mto Heilongjiang walipigana huko kwa siku 49, hatimaye dragon mweusi alimshida dragon mweupe, lakini dragon mweusi alijeruhiwa vibaya na alishidwa kurejea kwenye Mto Heilongjiang, alianguka ardhini na kusababisha shimo moja kubwa, korongo wa peponi alitaka kumwokoa, akachukua maji ili kumsaidia, hivyo yakatokea maziwa na ardhi oevu."

Maji ya hifadhi ya Zhalong ni safi sana, korongo wenye utosi mwekundu wanaoishi huko wanakula samaki, kamba, kombe na mizizi ya mimea. Matete yanayoota kwenye hifadhi ya Zhalong yana kimo cha mita 1 hadi mita 3, ni vigumu sana kwa binaadamu kuingia kwenye sehemu hiyo, mazingira hayo ni mazuri sana kwa kuishi na kuzaliana kwa ndege hao adimu. Kila ifikapo mwezi Machi, ambapo hali ya hewa siyo baridi tena, na maua yanaanza kuchanua, makundi mengi ya korongo wenye utosi mwekundu huenda huko kujenga viota na kuzaliana baada ya kuruka kutoka sehemu ya mbali ya kusini.

Ili kuhifadhi mazingira ya kupatana kwa viumbe, serikali ya huko imeweka sehemu ya utalii pembeni mwa ardhi oevu na kuwakataza watalii kuingia kwenye ardhi oevu. Watalii wanaweza kuangalia ardhi oevu na korongo wenye utosi mwekundu kutoka kwenye jengo lenye kimo cha mita 30. Mtu akisimama kwenye jengo hilo na kuangalia mbali, anaweza kuona mandhari nzuri, ardhi oevu inayoota matete isiyo ya upeo, maji yameungana na mbingu, vivuli vya maua ya matete vinaonekana kwenye maji maangavu, korongo wenye utosi mwekundu na manyoya meupe wanatembea kwa madaha, au kuruka chini kwa chini juu ya maji ya maziwa, hiyo ni mandhari nzuri iliyoje!

Ili kuwahifadhi ndege hao adimu, hifadhi ya Zhalong licha ya kuwalinda korongo mwitu, wanatotolesha vifaranga vya korongo, na sehemu hiyo imekuwa kituo kikubwa cha kuwafuga na kutotolesha korongo wenye utosi mwekundu nchini China. Hifadhi hiyo ilianza kufuga korongo wenye utosi mwekundu mwaka 1979, hadi sasa sehemu hiyo imetotolesha korongo wenye utosi mwekundu zaidi ya 640. Korongo waliototoleshwa na binadamu wanapelekwa haraka katika makundi ya korongo mwitu ili kuongeza idadi ya korongo mwitu. Habari zinasema hivi karibuni walitotolesha vifaranga zaidi ya 40 wa korongo wenye utosi mwekundu, na sasa wanaishi kwa afya nzuri chini ya uangalizi ya wafugaji. Mfanyakazi wa hifadhi hiyo Bw. Wang Kun alisema,

"Korongo jike hutaga mayai mawili kwa mwaka, na korongo hao huchukua vifaranga vyao kwenye sehemu ya kusini mwishoni mwa Oktoba na mwanzoni mwa mwezi Novemba, na wanawarejesha katika majira ya Spring ya mwaka unaofuata ili kuwapa mazoezi ya kuishi peke yao na kuzaliana. Sisi tunapokwenda kuchukua mayai ya korongo, huwa tunachukua yai moja katika kiota chao, kisha korongo mzazi anataga yai moja lingine, endapo tunachukua mayai yote mawili, korongo mzazi atataga mayai mawili tena, ikiwa tutachukua mayai mawili tena, basi ataruka kwenda sehemu nyingine, kwani anaona mahali anapokaa sasa hakuna usalama. Hii ndiyo sababu ya korongo wenye utosi mwekundu kuitwa kuwa 'ndege wanaoonesha kiwango cha mazingira', yaani mahali wanapoishi korongo wenye utosi mwekundu ni mahali penye mazingira bora."

Ili kukidhi matarajio ya watalii kuwa karibu na korongo wenye utosi mwekundu, wafanyakazi wa hifadhi wametenga sehemu moja ya ardhi oevu, ambayo korongo wenye utosi mwekundu wanaofugwa, wanaachiwa nje kutoka katika vizimba ili wapate nafasi ya kutembea kwa uhuru. Kila unapofunguliwa mlango wa kizimba, korongo hao wanatoka nje kwa haraka huku wakinyoosha mabawa, wanapenda kurukaruka kwenye ardhi yenye majani na kukimbizana, wanapenda kurusha juu mizizi ya majani kwa midomo yao, kisha wanaruka na kudaka chakula chao. Mfugaji Bw. Xu Jianfeng alisema, korongo wenye utosi mwekundu wanaofugwa ni wapole sana, hawaogopi binadamu. Mwandishi wa habari alimwuliza,

"Wakati gani unafurahia zaidi kazi yako?

Ninafurahi sana wakati akirukaruka na kulia huku akiniangalia.

Ni wakati gani wanapenda kurukaruka wakikuangalia?

Kila siku asubuhi ninapowalisha chakula, au hawaruki kwa siku kadhaa. Lakini kama ukimwacha aruke kwa mzunguko mmoja, kama vile korongo tuliyemwokoa mwaka uliopita, kila siku asubuhi anakungoja, baada ya kuruka mzunguko mmoja, anarudi kwenye miguu yako, wakati huu unaona ndege amekuwa na upendo kwa binadamu, hili ni jambo la kufurahisha."

Bw. Xu Jianfeng alisema, mfugaji anatakiwa kuwaangalia korongo hao mara tatu ili kugundua mabadiliko ya hisia zao, korongo hunyongonyea kama binadamu hajisikii vizuri; ikiwa wana afya nzuri, korongo wanaelewa vitendo vya binadamu, wakiona mfugaji akiwasogelea, wanalia kwa furaha, na kurukaruka kwa kunyoosha mabawa.

Hifadhi ya Zhaolong inapokea watalii wengi wanaovutiwa na korongo wenye utosi mwekundu, baada ya kuona hali ile, wanasifu sana uhusiano mzuri uliopo kati ya binadamu na maumbile.

Idhaa ya kiswahili 2007-08-27