Waziri mkuu wa Iraq Bw. Nouri al-Maliki kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 26 mwezi Agosti, aliwakosoa mbunge wa baraza la juu la bunge la Marekani wa chama cha Democrat cha Marekani na Bw. Carl Levin, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kijeshi ya baraza la juu la bunge la Marekani, akiwalaali kwa kuchukulia Iraq kama ni kijiji kimoja cha Marekani na kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo. Alitoa wito wa kutaka viongozi hao wa Marekani wasisahau kuiheshimu Iraq wakati wanapoizungumzia nchi hiyo.
Vyombo vya habari vinaona kuwa Bw. Maliki alisema maneno hayo kabla ya kufanyika kwa mkutano wa bunge la Marekani tarehe 4 mwezi Septemba, na amirijeshi mkuu wa jeshi la Marekani nchini Iraq Bw. David Petraeus na balozi wa Marekani nchini Iraq Bw. Ryan Crocker kwenda Washington kutoa ripoti ya tathmini kuhusu hali ya Iraq tangu Marekani iongeze askari elfu 30 nchini Iraq mwaka huu, hii inaonesha wasiwasi wake kuhusu Marekani kubadilisha sera zake kuhusu Iraq. Bw. Maliki kuwa na wasiwasi kutokana na hali halisi ilivyo nchini Iraq.
Kabla ya hapo Maliki na serikali inayoongozwa naye licha ya kukosolewa na wabunge wa Marekani wa chama cha demokrasia cha Marekani, pia wanakosolewa kwa mfululizo na baadhi ya maofisa wa ngazi ya juu akiwemo rais George Bush. Balozi wa Marekani nchini Iraq Bw. Crocker alisema, "vitendo vya Iraq katika shughuli za kisiasa vinasikitisha kabisa". Taarifa ya tathmini iliyotolewa hivi karibuni na idara ya upelelezi ya Marekani pia inasema mwendo wa kisiasa nchini Iraq umesimama, uwezo wa viongozi wa serikali ya Iraq unatia mashaka. Mbunge mashuhuri aliyetoka chama cha Republican cha Marekani Bw. John Wana pia alihimiza rais Bush kuondoa baadhi ya askari wa Marekani kabla ya Krismasi mwaka huu. Kutokana na hali ya namna hiyo, wakati Maliki anapowaonya wanachama wa chama cha Democrat cha Marekani, pia anaisihi serikali ya Bw Bush isimtelekeze. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 26, alisema anatarajia kuwa Bw David Petraeus atachukua msimamo wa kuiunga mkono serikali ya Iraq katika taarifa ya tathmini, ili kufanya wanasiasa wanaotaka kuipinga serikali ya Iraq kwa kutegemea taarifa hiyo, wasikitike.
Wachambuzi wanasema ingawa Bw Maliki analalamika kuhusu ukosoaji wa serikali ya Bw Bush na chama cha Republican cha Marekani, lakini anajua kuwa hivi sasa yeye hawezi kukosa uungaji wa Marekani. Lengo lake la kuwaonya wanachama wa chama cha demokrasia ni kuieleza serikali ya Bw Bush isibadilishe haraka sera zake kuhusu Iraq kutokana na shinikizo ya wanachama wa chama cha Democrat, kwa serikali yake itaingia kwenye hali ya kuangamia, na wakati huo makundi mbalimbali ya kisiasa nchini Iraq yatapimana nguvu na nchi ya Iraq itafarakana vibaya.
Wachambuzi pia wanasema katika mambo ya usalama, serikali ya sasa ya Iraq haiwezi kusimama vizuri bila uungaji mkono na misaada ya jeshi la Marekani, lakini kuweko kwa nguvu ya kijeshi ya Marekani na kudhibiti mambo ya ndani ya kidiplomasia ya Iraq, pia kunakwamisha ujenzi wa uwezo wa serikali ya Bw Maliki na jeshi la nchi hiyo. Ukaliaji wa muda mrefu wa jeshi la Marekani nchini Iraq umefanya majeshi ya polisi na usalama ya Iraq kukosa imani, wakati magaidi wamekuwa wanajipenyeza kwenye jeshi la askari katika muda mrefu uliopita.
Katika mambo ya ndani, kuweko kwa nguvu ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq, kumedhoofisha nguvu za hatua za serikali ya Maliki kutoa msamaha mkuu kwa maofisa wa serikali na jeshi la zamani, kuvutia makundi yasiyopendelea upande wowote na kuhimiza mchakato wa usuluhisho wa kisiasa. Katika mambo ya kidiplomasia, Bw Maliki anatarajia kuboresha uhusiano na nchi jirani zikiwemo Iran na Syria, ili kuungwa mkono na nchi za jirani katika mambo ya usalama, kustawisha uchumi na usuluhisho wa kisiasa. Lakini serikali ya Bw Bush imekuwa inadhoofisha jitihada za kidiplomasia ya serikali ya Bw Maliki, na kumfanya awe katika hali ya kutokuwa na mbele wala nyuma.
Kwa muda mfupi ujao, serikali ya Bw Maliki itaendelea kuitegemea Marekani, lakini kutokana na kupamba moto kwa mapambano ya kisiasa kati ya vyama viwili vya kisiasa nchini Marekani, na serikali ya George Bush kukabiliwa na shinikizo kubwa zaidi la kisiasa, serikali ya Bw Maliki itakabiliwa na hali ngumu zaidi katika mambo ya ndani na ya kidiplomasia.
|