Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-31 16:50:02    
Tarehe 31 mwezi Agosti mwaka 1997, Princess Diana wa Uingereza afariki dunia kwenye ajali ya gari

cri

Tarehe 31 mwezi Agosti mwaka 1997, Princess Diana wa Uingereza afariki dunia kwenye ajali ya gari

Asubuhi mapema ya tarehe 31 mwezi Agosti mwaka 1997, ili kukwepa waandishi wa habari waliong'ag'ania kumpiga picha, Princess Diana mwenye umri wa miaka 36 alikumbwa na ajali ya gari na kufariki dunia. Princess Diana aliolewa kwenye ukoo wa ufalme wa Uingereza mwaka 1981, lakini maisha yake hayakuwa mazuri, maisha yake ya muda mfupi yalimalizika kwa masikitiko.

Mwaka 1996 Prince Charles na Princess Diana walitengana, baadaye Princess Diana alikutana na mtoto wa mfanyabiashara tajiri wa Misri Bw. Dodi Al Fayed na hatimaye wakapendana haraka. Alasiri ya tarehe 30 mwezi Agosti Princess Diana na Bw. Dodi Al Fayed walifika Paris Ufaransa kutoka bahari ya Mediterranean, vyombo vya habari vilikuwa vimepata habari kuhusu watu hao wawili vikang'agania kuwapiga picha. Gari la Princess Diana lilikimbia kwa kasi ya kilometa 180 kwa saa kwenye barabara ya karibu na Mto Seine, kutokana na kasi kubwa, gari lake liligongana na kingo za barabara, Princess Diana na Bw. Fayed wote walikufa kwenye ajali hiyo.

Tarehe 28 mwezi Agosti mwaka 1963 Bw. Martin Luther King atoa hotuba maalumu "Nina ndoto "

Tarehe 28 mwezi Agosti mwaka 1963 Kiongozi maarufu wa watu waafrika nchini Marekani Bw. Martin Luther King aliendesha Mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na watu laki 2.5 huko Washington, na kuwaongoza watu hao kufanya maandamano kuelekea kwenye Jumba la Makumbusho la Lincoln kutoka kwenye Mnara makumbusho ya George wa Washington. Watu milioni kadhaa waliangalia maandamano hayo, na hadi leo watu wengi bado wanakumbuka hali hiyo ilivyokuwa.

Kwenye mkutano huo Bw. Martin Luther King alitoa hotuba iliyoitwa "Nina Ndoto" ambayo inajulikana duniani hadi leo. Alisema:

"Mimi nina ndoto, ndoto yangu inatokana na ndoto ya Marekani. Nina matumaini kwamba, katika siku za usoni sisi watu weusi tutasimama nchini humu, na kutimiza ndoto hiyo, yaani watu wote wa nchi yetu watakuwa na usawa tangu walipozaliwa. Katika Jimbo la Mississippi, watoto wa watumwa na watoto wa watu wenye watumwa wanakula chakula katika meza moja; siku moja uhuru na haki ya usawa utachukua nafasi ya ukandamizaji na unyonyaji; watu wote watapata uhuru, tunashukuru mungu, tutapata uhuru."

Tarehe 28 mwezi Agosti mwaka 2001 Mkutano wa Baraza la jumuiya zisizokuwa za kiserikali wa kupinga ubaguzi wa rangi lilifanyika Afrika ya Kusini

Mkutano wa Baraza la jumuiya zisizo za kiserikali wa kupinga ubaguzi wa rangi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa tarehe 28 mwezi Agosti mwaka 2001 ulifunguliwa huko Durban, Afrika ya Kusini, Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini alitoa mwito wa kutoa fidia kwa watu waliodhuriwa katika biashara ya utumwa, Utawala wa kikoloni na Ubaguzi wa Rangi.

Kwenye sherehe ya kufunguliwa kwa mkutano huo Rais Mbeki alisema, biashara za watumwa, utawala wa kikoloni na ubaguzi wa rangi ni ukurasa wa giza katika historia ya binadamu, watu wote wanapaswa kutambua historia hiyo na kuulaani vikali kithabiti. Nchi kadhaa zinapaswa kuchukua hatua zenye mafanikio ili kuondoa mabaki ya biashara za watumwa, utawala wa kikoloni na ubaguzi wa rangi. Alisisitiza kuwa waafirka walidhuriwa sana katika biashara ya watumwa na utawala wa kikoloni na ubaguzi wa rangi, na sasa wanaathirka na utandawazi wa uchumi duniani. Kama watu hawataungana chini ya mwito wa kupinga ubaguzi wa rangi duniani, baraza la jumuiya zisizokuwa za kiserikali na mkutano wa kupinga kupambana na ubaguzi wa rangi litapoteza maana yake.

Wajumbe kutoka Shirika kuu la wanawake wa China, Shirika la Urafiki kwa nchi za nje, Kamati ya haki za binadamu ya China, Shirika la Umoja wa Mataifa la China na Shirika la mambo ya utoaji msaada la China walihudhuria mkutano huo.

Idhaa ya kiswahili 2007-08-31