Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-05 16:15:50    
Mapishi ya vichipukizi vya mianzi na nyama ya nguruwe iliyokaushwa

cri

Mahitaji:

Vichipukizi vya mianzi gramu 120, nyama ya nguruwe iliyokaushwa gramu 250, vitunguu maji gramu 20, mvinyo wa kupikia gramu 4, mchuzi wa sosi gramu 3, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, pilipili hoho gramu 2, mafuta gramu 70

Njia:

1. kata nyama ya nguruwe iliyokaushwa iwe vipande, kata vichipukizi vya mianzi viwe vipande.

2. washa moto mimina maji kwenye sufuria , baada ya kuchemsha, weka vipande vya nyama ya nguruwe kwenye maji moto, korogakoroga vipakue.

3. tia mafuta kwenye sufuria, tia pilipili hoho, vipande vya vichipukizi vya mianzi, korogakoroga, tia vipande vya nyama ya nguruwe iliyokaushwa, mvinyo wa kupikia, mchuzi wa sosi, chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, mimina maji chemsha kwa dakika 10, tia vipande vya vitunguu maji, korogakoroga ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.