Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-06 16:06:36    
Baraza la vijana la duniani lina matumaini kuwa amani itaweka mizizi mioyoni mwa vijana

cri

Mkutano wa 9 wa Baraza la vijana duniani la Umoja wa Mataifa ulifanyika tarehe mosi hadi tarehe 3 Septemba huko Sharm el-Sheikh nchini Misri, mji unaojulikana kama "mji wa amani". Hii ni mara ya kwanza kwa Misri kuandaa mkutano wa Baraza la vijana duniani, ambapo vijana 600 hivi kutoka nchi 85 walijadili kuhusu "mchango wa vijana katika kulinda amani".

Mwandaaji wa mkutano wa baraza hilo, ambaye ni mke wa rais wa Misri Bibi. Suzanne Mubarak ambaye pia ni mwanzilishi wa "harakati za amani za wanawake duniani za Suzanne Mubarak" alitoa hotuba akiwahamasisha vijana wachukue hatua mara moja kwa ajili ya amani. Alisema:

"tunapaswa kushirikiana ili kujenga amani ya dunia nzima. Tutawafuatilia zaidi vijana kwa kusikiliza maoni yao, tutawaletea fursa nyingi zaidi ili muweze kutoa mchango wa kuleta amani kwa kutumia njia yenu. Leo mnaweza kutoa nguvu zenu na kujenga amani yenu katika dunia yenu. Mpige hatua na kubeba wajibu wenu na kuleta mabadiliko mapya kwa maisha ya watu, ili watu wote waweze kuishi pamoja kwa amani."

Bibi. Suzanne alisema amani haiko mbali nasi, kila kijana anaweza kuona amani katika familiayake, shuleni, mitaani na kutoka kwa marafiki zake. Alisema baraza hilo linatoa fursa kwa vijana kutoa maoni yao, lakini ana matumaini kuwa mkutano wa baraza hilo unaweza kuwa mwanzo kwa vijana kushiriki kwenye harakati za kudumisha amani.

Watu wanaohudhuria mkutano wa baraza hilo waliona kuwa hali ya siku za mbele itaamuliwa na vijana, vijana ni viongozi wa siku za mbele. Inapaswa kuwatia moyo kushiriki kwenye mambo ya kisiasa ya taifa, na kuwaandaa wawe na uwezo wao wa kuongoza. Mshauri maalumu wa kamati ya maendeleo ya mabunge ya Ulaya Bw. Ricard Torrell alipozungumzia hali ilivyo ya sasa ya maendeleo ya vijana nchini Ujerumani alisema, inapaswa kutilia maanani zaidi hali ya vijana kutofuatilia mambo ya kisiasa. Akisema

"Maingiliano kati ya Ujerumani na nchi nyingine kuhusu utafiti wa mambo yanayowahusu vijana ni muhimu. Je, vijana wanafanya nini? Wanafikiri nini? Wanafuatilia masuala gani ya kisiasa? Aslimia 28 ya vijana wa Ujerumani wanafuatilia mambo ya kisiasa, na wengine wanaona uamuzi wa kisiasa hauwahusu, wanaona kuwa mambo yote ya ujerumani yanahusiana na uchumi, hali hii inaonesha kuwa wao hawafuatilia mchakato wa siasa, hawapendi kushiriki kwenye mambo ya vyama na namna ya kutunga sera. Hivyo tulianzisha mradi katika shule za sekondari na vyuo vikuu, ili vijana waweze kushiriki zaidi kwenye mambo ya kisiasa.

Mkurugenzi wa idara ya mradi wa vijana ya Kituo cha utafiti wa sera cha Lebanon Bw. Jamil Mouawad pia alisema, inapaswa kuwahamasisha vijana washiriki kwenye mambo ya kisiasa kwa machanguo ya aina mbalimbali. Akisema:

"tunawaunga mkono sana vijana kushiriki kwenye mambo ya kisiasa kwa kupitia uchaguzi. Kwanza, kushiriki kwenye kugombea nafasi kwenye uchaguzi kwa vijana kunaweza kugundua watu wenye uwezo wa kutoa maamuzi ya kisiasa. Aidha, inaweza kuhusisha mashirika mbalimbali ya jamii na kuondoa migongano kati yao kwa njia ya amani. "

Mkutano wa Baraza hilo umependekeza vijana wafundishwe namna ya kuelewa, kuheshima na kuamini watu wa makabila mbalimbali na watu wenye dini mbalimbali. Wakati wanapopata matatizo, wanaweza kutatua matatizo hayo kwa njia ya mazungumzo badala ya mapambano, na kujenga na kulinda amani kwa njia yao.

Idhaa ya kiswahili 2007-09-06