Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-06 18:44:07    
Rais Hu Jintao atoa hotuba kwenye Mkutano wa kilele wa mambo ya biashara wa APEC

cri

Mkutano wa kilele wa mambo ya biashara wa jumuiya ya ushirikiano wa uchumi wa Asia na sehemu ya Pasifiki, APEC, ambao utafanyika kwa siku 2, umefunguliwa tarehe 6 mwezi Septemba kwenye jumba la michezo ya opera la Sydney, Australia. Viongozi wa nchi wanachama wa APEC watafanya majadiliano pamoja na wanaviwanda na wafanyabiashara kuhusu masuala ya biashara, utandawazi wa uchumi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais Hu Jintao wa China ametoa hotuba kwenye mkutano wa kilele, kauli-mbiu ya hotuba hiyo ni "kuimarisha ushirikiano wa pande zote, na kuwa na maendeleo endelevu", akitoa ufafanuzi wa msimamo wa serikali ya China kuhusu masuala muhimu yanayotokea katika maendeleo ya uchumi ya dunia na sehemu ya Asia na Pasifiki.

Hivi sasa mabadiliko makubwa yanatokea katika mambo ya uchumi wa dunia, katika hali ambayo fursa na changamoto zimetokea kwa pamoja, namna ya kushirikiana na kujenga kwa pamoja siku za mbele zenye maendeleo endelevu, limekuwa ni somo kubwa linalozingatiwa kwa makini. Rais Hu Jintao ametoa mapendekezo matano akisema:

"ni lazima kuhimiza maendeleo ya uwiano wa uchumi wa dunia, kuunda utaratibu unaofaa wa biashara ya pande nyingi, kutosheleza mahitaji ya nishati, kuhifadhi mazingira bora ya kimaumbile na kukuza uvumbuzi na elimu ya sayansi na teknolojia".

Rais Hu Jintao amesema uzoefu umeonesha kuwa, mambo ya uchumi wa China yanayoendelea katika hali ya utulivu, si kama yanawanufaisha wananchi wa China wapatao bilioni 1.3, bali pia yameleta fursa kubwa ya biashara kwa nchi mbalimbali duniani, na kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa dunia. Amesisitiza kuwa China itaendelea kutoa mchango wake kwa maendeleo endelevu ya dunia. Akisema:

"China itashikilia njia mpya ya kukuza mambo ya viwanda ya teknolojia ya kisasa, yenye ufanisi mzuri wa uchumi, kuokoa raslimali, kupunguza utoaji wa vitu vya uchafuzi na kutumia ipasavyo hali bora ya nguvukazi, kuanzisha mtindo wa uzalishaji mali na mtindo wa matumizi ya bidhaa unaokwenda sambamba na maendeleo endelevu, China pia itaendelea kutekeleza sera za ufunguaji mlango zinazonufaisha pande zote mbili, kuunga mkono kuunda utaratibu wa biashara ya pande nyingi, wa haki, mwafaka, na kutokuwa na ubaguzi, na itaimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara pamoja na nchi na sehemu mbalimbali duniani zikiwemo nchi wanachama za APEC kwa msingi wa usawa na kunufaishana".

Rais Hu Jintao wa China ameeleza msimamo na mapendekezo ya China kuhusu sifa na usalama wa bidhaa. Akisema:

"China inatilia maanani sana sifa na usalama wa bidhaa zinazouzwa nchi za nje. China ina msimamo wa kuwajibika kwa makini sana na kufanya juhudi kubwa kuhakikisha sifa na usalama wa bidhaa katika mchakato wa kuzalisha bidhaa, kusambaza bidhaa, kusafirisha nje au kuagiza kutoka nje, katika kazi za utungaji wa sheria, utekelezaji wa sheria, na kufanya usimamizi, ili kuhakikisha sifa na usalama wa bidhaa. China inapenda kupanua ushirikiano na pande mbalimbali katika kazi za kusimamia sifa na usalama wa bidhaa, na kuongeza mawasiliano ili kuinua kwa pamoja kiwango cha sifa na usalama wa bidhaa katika biashara duniani. Amesema kama tutatumia fursa iliyopo kuzidisha ushirikiano na kuimarisha ujenzi wa jumuiya yetu, hakika tutaweza kujenga siku zetu za mbele zenye maendeleo endelevu.