|
Mkutano wa 15 usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC unatazamiwa kufanyika huko Sydney, Australia kuanzia tarehe 8 hadi 9 Septemba, ambapo viongozi au wajumbe wa nchi wanachama wa Jumuiya ya APEC akiwemo rais Hu Jintao wa China watajadili masuala makubwa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo yasiyo na uchafuzi, uungaji mkono wa mazungumzo ya raundi ya Doha, na utandawazi wa uchumi wa kikanda.
Hivi sasa hali ya jumla ya siasa ya dunia nzima na kanda ya Asia na Pasifiki ni ya utulivu, ambapo mambo ya uchumi yanaongezeka kwa hatua madhubuti, na ushirikiano wa kikanda unaendelea kwa kina. Lakini dunia nzima na kanda ya Asia na Pasifiki pia zinakabiliwa na matatizo makubwa kama vile hali isiyo na uwiano kwenye mambo ya uchumi inazidi kuwa mbaya, mwelekeo wa kujilinda kibiashara unaibuka, shinikizo la nishati na maliasili linaongezeka, na hali ya mazingira ya viumbe inazidi kuwa mbaya. Kauli mbiu ya Mkutano huo wa APEC ni "Kuimarisha ujenzi wa jumuiya yetu na kujenga kwa pamoja siku zetu za mbele zenye maendeleo endelevu". Kwenye Mkutano wa kipindi cha kwanza, viongozi wa nchi mbalimbali watajadili hasa suala la mabadiliko ya hali ya hewa, na kwenye Mkutano wa kipindi cha pili watajadili masuala mengine pamoja na mazungumzo ya raundi ya Doha ya WTO na utandawazi wa uchumi wa kikanda.
Suala la mabadiliko ya hali ya hewa linafuatiliwa zaidi kwenye Mkutano huo wa APEC, kwa sababu kamati maalum ya kiserikali kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa IPCC iliyoanzishwa na Jumuiya ya hali ya hewa duniani na Shirika la mipango ya mazingira la Umoja wa Mataifa ilitoa ripoti ya nne inayothibitisha mabadiliko ya hali ya hewa siku chache zilizopita, ripoti hiyo inaona kuwa zaidi ya asilimia 90 ya mabadiliko ya hali ya hewa huenda yanasababishwa na shughuli za binadamu; aidha kuna uwezekano wa kudhibiti uzito wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani kwenye kiwango cha chini, hivyo dunia nzima inapaswa kuchukua hatua mara moja. Ripoti ya Kamati ya IPCC ina umuhimu mkubwa wa kuelekeza utoaji wa sera wa pande mbalimbali. Zaidi ya hayo, "Makubaliano ya Kyoto" yaliyoweka malengo ya nchi zilizoendelea kupunguza utoaji wa hewa zinasababisha kuongezeka kwa joto duniani, yatafanya kazi mpaka mwaka 2012 tu. Hivi sasa mazungumzo kuhusu makubaliano ya Kyoto ya siku za baadaye yameanza ili kuamua kuwa pande mbalimbali zitafuata kanuni gani kupunguza utoaji huo wa hewa kwa kila upande baada ya mwaka 2012. Ndiyo maana, Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo Jumuiya ya APEC inatakiwa kufanya juhudi kujadili suala hilo kwa hivi sasa.
Aidha hivi sasa suala la mabadiliko ya hali ya hewa halihusiani tu na hali ya mazingira na hali ya hewa, bali pia linahusiana na mambo ya siasa, uchumi na maendeleo, undani wake ni pande mbalimbali kugombea hadhi yenye nguvu katika maendeleo ya nishati na ushindani wa uchumi katika siku za mbele, suala hilo ni kama suala la matumizi na mgawanyo wa raslimali za nchi zote za dunia nzima. Kuhusu namna ya kutatua suala la mabadiliko ya hali ya hewa, hivi sasa kuna migongano kati ya pande mbalimbali na makundi yenye maslahi tofauti, hivyo lazima kuimarisha mawasiliano na mashauriano kuhusu suala hilo kubwa, ili kufikia maoni ya pamoja. Inatarajia kuwa kwenye Mkutano huo, nchi mbalimbali wanachama wa Jumuiya ya APEC zitafanya majadiliano kwa juhudi ili kufikia na kutangaza "Taarifa ya Sydney" kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwenye Mkutano huo suala kuhusu kuunga mkono mazungumzo ya raundi ya Doha linafuatiliwa na pande mbalimbali, ambapo nchi wanachama wa APEC ambazo thamani ya biashara kati yao inachukua zaidi ya nusu ya ile ya jumla duniani zitafikia maoni gani ya pamoja, ni muhimu sana kwa mazungumzo ya raundi ya Doha.
Na suala kuhusu utandawazi wa uchumi wa kikanda pia linafuatiliwa na wengi kwenye Mkutano huo. Tokea kuanzishwa kwa Jumuiya ya APEC, jumuiya hiyo imeonesha umuhimu mkubwa katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kuhimiza biashara na uwekezaji huria na wenye urahisi, na ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia kati ya nchi wanachama. Inatazamiwa kuwa Mkutano huo utapitisha "Ripoti kuhusu utandawazi wa uchumi wa kanda ya Asia na Pasifiki", na kupitisha mapendekezo ya sera ili kuhimiza mchakato wa utandawazi wa uchumi wa kikanda.
|