Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-12 17:07:22    
Mwaka wa sita baada ya tukio la "Septemba 11", Mapambano dhidi ya ugaidi yanahitaji ushirikiano wa pande zote

cri

Tarehe 11 ilikuwa ni siku ya kuadhimisha mwaka wa sita baada ya tukio la "Septemba 11". Watu wengi wamegundua kwamba mwaka huu Marekani haikufanya shughuli nyingi kukumbuka siku hiyo kama ilivyokuwa zamani. Mkurugenzi wa kitengo cha utafiti wa mapambano dhidi ya ugaidi katika Taasisi ya Utafiti wa Uhusiano wa Kimataifa ya China Bw. Li Wei anaona kuwa, hapo kabla kulikuwa na haja kuifanya tarehe 11 Septemba iwe siku ya kukumbukwa ili sera za Marekani za mapambano dhidi ya ugaidi zipate uungaji mkono, lakini kutokana na mabadiliko ya hali nchini Marekani na nchi za nje, Marekani imekuwa na mtizamo mwingine kuhusu maadhimisho ya siku hiyo. Bw. Li Wei alisema,
"Kwa nini mwaka huu Marekani haikupiga kelele sana kukumbuka siku hiyo? Mimi binafsi naona kuwa kwanza tokea tukio la 'Septemba 11' hadi sasa sera za Marekani za kupambana na ugaidi kimsingi zimekuwa nyingi, lakini hasara iliyopata Marekani ni kubwa kuliko faida. Kimya cha Marekani katika siku hiyo kinamaanisha kujichambua."
Bw. Li Wei alisema, wakati Marekani inapokuwa kimya kukumbuka siku ya tukio la 'Septemba 11', kiongozi wa kundi la Al-Qaida Osama bin-Laden alijitokeza kwenye mtandao. Hii inamaanisha kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yanatatanisha sana, na huku Marekani ikiwa inafanya makosa mengi katika mapambano hayo. Ugaidi ni tishio linaloikabili dunia nzima. Bw. Li Wei alisema, mapambano dhidi ya ugaidi kote duniani yana faida na hasara, matatizo bado ni mengi. Alisema,
"Tokea tukio la 'Septemba 11' litokee hadi sasa ushirikiano wa kimataifa kwenye mapambano dhidi ya ugaidi umepata mafanikio makubwa, viongozi wengi waandamizi wa kundi la Al-Qaida wameuawa au kukamatwa, na njama nyingi za ugaidi zimegunduliwa. Lakini kwa upande mwingine kundi la Al-Qaida linaendelea na kuenea. Zaidi ya hayo, kuenea kwa ushawishi wa kundi la Al Qaed kumeleta usumbufu mkubwa katika mapambano hayo ya kimataifa."
Bw. Li Wei pia alieleza matatizo yaliyomo katika mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi. Alisema mfumo wa kupambana na ugaidi unaoongozwa na Umoja wa Mataifa bado haujapatikana, ingawa ushirikiano wa kikanda kati ya pande mbili kwa kiasi fulani unaweza kuzuia matukio ya kigaidi, lakini hauwezi kupunguza vilivyo maeneo ya shughuli za magaidi. Bw. Li Wei alisema,
"Hivi sasa shughuli za mapambano dhidi ya ugaidi zinalenga kupambana na magaidi waliopo, na hakuna njia za kutatua matatizo ya shina yanayosababisha ugaidi, yaani hatujapata njia ya kimsingi ya ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya ugaidi."
Bw. Li Wei anaona kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yanahitaji ushirikiano wa pande zote duniani, na mapambano hayo ya kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa ndio yanayoweza kufyeka mizizi ya ugaidi. Bw. Li Wei alisema,
"Tukitaka kutatua matatizo ya ugaidi kuna haja ya kufuata njia inayoongozwa na Umoja wa Mataifa. Nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na China zimekuwa zikijitahidi kusukuma Umoja wa Mataifa upitishe makubaliano ya mapambano dhidi ya ugaidi kwa pande zote chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa, makubaliano hayo ya mapambano kwa pande zote yatatatua matatizo yanayokanganya hivi sasa katika mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi na kutatua chanzo cha matatizo ya ugaidi, ili kupata ufanisi kwenye mapambano hayo.

Idhaa ya kiswahili 2008-09-12