Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-12 19:54:56    
China yaanza kutekeleza utaratibu mpya wa kutoa misaada kwa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi

cri

Vyuo vikuu mbalimbali nchini China vimeanza muhula mpya wa masomo mwezi Septemba, ambapo wanafunzi milioni 5.6 wapya watajiunga na vyuo vikuuu. Miongoni mwao, wanafunzi milioni 1 hivi wanatoka familia zenye matatizo ya kiuchumi. Kuanzia muhula huo mpya, China itaongeza kwa kiasi kikubwa misaada kwa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi, wanafunzi hao na wazazi wao hawatakuwa na wasiwasi tena kutokana na ada za masomo.

Msichana Xu Chenxi na familia yao wanaishi katika kijiji cha Zhushan katika wilaya ya Qu mkoani Sichuan. Hivi karibuni sehemu hiyo ilikumbwa na maafa makubwa ya mafuriko. Katika maafa hayo nyumba yao ilibomoka na nafaka za nyumbani ilizolewa, maisha yao yaliyokuwa maskani yamezidi kuwa magumu. Namna ya kukusanya fedha kwa ajili ya ada za masomo ya Xu Chenxi imekubwa suala kubwa linaloisumbua familia hiyo.

Hivi sasa elimu ya juu nchini China si ya lazima, wanafunzi wanatakiwa kulipa ada kubwa za elimu. Kwa wastani mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu anagharamu yuan elfu 10 kila mwaka. Gharama hiyo ni mzigo mkubwa kwa familia zenye matatizo ya kiuchumi, hasa familia za vijijini.

Lakini suala lililosumbua familia ya Xu Chenxi lilitatuliwa haraka, idara ya mambo ya raia na ya elimu ya huko si kama tu zilipeleka kwao yuan elfu 6 ya misaada ya masomo, bali pia ziliwaelezea sera mpya ya seriakali ya misaada ya masomo. Mkuu wa idara ya elimu ya wilaya ya Qu Bw. Xiong Changhong alisema:

"muhula huo sera nyingi mpya za kutoa misaada ya masomo zimeanza kutekelezwa, kwa upande mmoja ni kutoa udhamini wa masomo wa yuan elifu 5 kwa mwaka ili kuwafanya wanafunzi waongeze juhudi za masomo, kwa upande mwingine ni kutoa misaada ya masomo kwa ajili ya waanfunzi wanaotoka kwenye familia zenye matatizo ya kiuchumi. Aidha, wanafunzi pia wanaweza kufanya kazi katika vyuo vikuu au kutoa ombi la mkopo ya msaada ili kumudu ada za shule."

Ili kuwasaidia wanafunzi hao kumaliza masomo, serikali ya China imeendelea kufanya juhudi katika kujenga utaratibu wa kutoa miaada kwa njia nyingi. Hivi sasa njia za kutoa misaada kwa wanafunzi ni pamoja na kutoa mikopo ya misaada ya masomo na udhamini wa masomo, kuhamasisha wanafunzi kufanya kazi baada ya masomo katika vyuo vkuu, na kuwapunguzia ada za shule wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi nyumbani.

Lakini asilimia 20 hivi kati ya wanafunzi milioni 17 wanaosoma katika vyuo vikuu nchini China wanatoka kwenye familia zenye matatizo ya kiuchumi, kutokana na idadi hiyo kubwa, misaada ya taifa haiwezi kunufaisha kila mwanafunzi mwenye tatizo hilo, kuliwahi kuwa na wanafunzi walioshindwa kumaliza masomo yao kutokana na matatizo ya kiuchumi. Ili kutatua suala hilo, kuanzia muhula huo wa Autumn, China itaongeza kwa kiasi kikubwa misaada kwa wanafunzi hao. Mkurugenzi wa idara ya elimu, sayansi na afya katika wizara ya fedha ya China Bw. Zhao Lu alisema:

"katika muhula huo wa Autumn, serikali kuu na ya mitaani ziemtenge yuan bilioni 15.4 kwa ajili ya misaada ya masomo, kabla ya hapo fedha zilizotumika katika kazi hiyo ni yuan bilioni 1.8 tu kila mwaka. China imeinua kwa kiasi kikubwa kiwango cha misaada hiyo na pia imeongeza kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanaoweza kunufaika kutokana na utaratibu huo."

Imefahamika kuwa, fedha za nyongeza zitatumika kutoa udhamini na misaada ya masomo kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia zenye matatizo ya kiuchumi. Kiwango cha misaada ya masomo ya kiserikali kimeinuliwa kufikia yuan elfu 2 kutoka yuan 1500 kila mwaka, idadi ya wanafunzi wanaopewa misaada hiyo itafikia miloni 3.4, ambayo ni mara saba kuliko ile ya zamani. Aidha, wanafuni laki 5 hodari kati hao watapewa yuan 5000 za udhamini wa masomo wa kiserikali kila mwaka. Utekelezaji wa sera hiyo mpya umeondoa wasiwasi ya Xu Chenxi na wazazi wake. Alisema:

"sina wasiwasi tena kuhusu ada za shule, katika chuo kikuu nitafanya bidii ili kupata udhamini wa masomo."

Mbali na sera za taifa za kutoa misaada, serikali za sehemu mbalimbali pia zimeweka utaratibu husika. Kama wilaya ya Qu anayotoka misichana Xu Chenxi, serikali ya huko inatoa misaada kwa kulingana na hali halisi ya familia za wanafunzi. Afisa wa huko anayeshughulikia mambo hayo Bw. Zhang Diping alisema:

"wilaya yetu imeanzisha kikamilifu utaratibu wa kutoa misaada ya masomo, wanafunzi wote wenye matatizo ya kiuchumi wa wilaya hiyo wakijiunga na vyuo vikuu, hupewa misaada ya zaidi ya yuan elfu mbili."

Aidha, ili kuhakikisha wanafanzi wenye matatizo ya kiuchumi waweze kufika katika vyuo vikuu bila matatizo, vyuo vikuu vya sehemu mbalimbali nchini China pia vimefanya maandalizi ya makini. Kwa mfano chuo kikuu cha Sichuan kinawatumia wanaufunzi barua ya kukubaliwa kusoma kwenye chuo pamoja na vitabu mbalimbali vya maelekezo. Vitabu hivyo vitaeleza sera za serikali za kutoa misaada kwa wanafunzi na njia ya kutoa ombi la misaada. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya wanafunzi katika chuo kikuu hicho Bw. Li Suanjiu alisema, chuo kikuu hicho kimeanzisha utaratibu kamili ili kuhakikisha wanafunzi wote wenye matatizo ya kiuchumi wanaweza kumaliza masomo yao.

Mbali na hayo, habari kutoka wizara ya elimu ya China zinasema, kuongeza misaada kwa wanafunzi kuanzia muhula huu wa masomo ni hatua ya mwanzo tu. Katika miaka kadha ijayo, fedha zinazotumika katika shguhuli hizo zitaongezeka hadi kufikia yuan bilioni 50, ambapo wanafunzi milioni 4 wa vyuo vikuu watanufaika kutokana na sera hiyo.