Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-12 20:21:56    
Mapishi ya samaki na mafuta

cri

Mahitaji

Samaki mmoja, mafuta gramu 50, supu ya kuku gramu 300, pilipili manga gramu 3, mvinyo wa kupikia gramu 20, mchuzi wa sosi gramu 30, chumvi gramu 4, chengachenga za kukoleza ladha gramu 3, giligilani gramu 30, vipande vya vitunguu maji gramu 20, tangawizi gramu 20

Njia

1. ondoa vitu vilivyo ndani ya tumbo la samaki, osha samaki halafu kata kata kwa kisu kwenye pande mbili za samaki.

2. washa moto mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi, korogakoroga, halafu mimina supu ya kuku, mvinyo wa kupikia, tia chumvi korogakoroga, weka samaki kwenye sufuria, chemsha kwa dakika 15, halafu ipakue. Weka samaki kwenye sahani, weka vitunguu maji, tangawizi na pilipili manga.

3. washa moto tena, mimina mchuzi wa sosi kwenye sufuria, mimina mafuta halafu mimina juu ya samaki, tia chengachenga za kukoleza ladha. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.