Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-13 15:19:23    
Wauguzi wa makabila madogo madogo mkoani Xinjiang

cri

Hospitali ya kwanza iliyo chini ya Chuo kikuu cha udaktari cha Xinjiang ni hospitali kubwa zaidi katika sehemu inayojiendesha ya kabila la wauygur ya Xinjiang. Hivi karibuni hospitali hiyo imekuwa na wauguzi wengi wanaofanya kazi vizuri, ambao ni wa makabila madogomadogo.

Kituo cha utoaji wa zana na dawa za kuua vijidudu, ni moja ya sehemu muhimu kwenye hospitali hiyo. Bi. Ma Binna wa kabila la wahui pamoja na wauguzi na wafanyakazi wengine zaidi ya 20 wa kabila la wahan, kabila la Uygur na makabila mengine wanafanya kazi kwenye kituo hicho.

Mwaka 1981 Bi. Ma Binna alipata ajira katika kituo cha kutoa zana na dawa za kuua vijidudu cha hospitali ya kwanza iliyo chini ya chuo kikuu cha udaktari cha Xinjiang, hadi sasa amefanya kazi kwenye hospitali hiyo kwa zaidi ya miaka 20. alisema:

"wakati tulipoanza kufanya kazi kwenye kituo hiki, tulikuwa hatupendi kazi hii, kwani kila siku tunafanya kazi za kusafisha vyombo kwa kutumia dawa ya kusafishia. Tuliona kuwa, hatutapata ufundi wa kazi katika kituo hiki. Lakini baada ya muda tulianza kuipenda kazi hii. Utoaji wa zana na dawa za kuua vijidudu ni kazi muhimu katika hospitali. Sifa ya kazi zetu inahusiana na sifa ya matibabu na usalama wa matibabu ya hospitali yetu."

Katika miaka 20 iliyopita wenzake waliondoka kutoka kituo hicho kwa sababu mbalimbali, lakini Bi. Ma Binna siku zote anaendelea na kazi hiyo.

Baada ya mwaka 1993 aliteuliwa kuwa mkuu wa wauguzi, ambapo alipata uelewa mpya kuhusu kazi zake. Wakati hospitali hiyo ilipofanya ukarabati, Bi. Ma Binna alitoa pendekezo la kuboresha ujenzi wa kituo cha utoaji wa zana na dawa za kuua vijidudu kwa mujibu wa uzoefu wake. Kutokana na pendekezo lake, kituo hicho kimebadilika na kuwa na sura mpya. Hadi sasa maofisa na wafanyakazi wengi wa hospitali nyingine za mkoani Xinjiang wanakwenda kuitembelea. Alisema kuwa anafurahi kuwaelezea uzoefu wake ili waweze kufanya kazi kwa njia ya kisasa.

Mwuguzi wa kabila la wauygur Bi. Sahipjamal amefanya kazi katika chumba cha upasuaji kwa miaka 12. Kazi za wauguzi katika chumba cha upasuaji ni nyingi na za muda mrefu, kila siku madaktari wanamaliza kazi zao saa ngapi, na wauguzi wanamaliza kazi zao saa ngapi. Kutokana na kazi nyingi, Bi. Sahipjamal alimpeleka bin yake mwenye umri wa miaka 3 kwa mama yake huko Hetian, umbali wa kilomita elfu 2 kutoka Urmuqi. Baada ya kumaliza kazi zake za kila siku, akirudi nyumbani, humpigia simu bin yake, ni jambo linalomfurahisha kusikia sauti ya bin yake. Alisema:

"Mama yangu alikuwa mwuguzi pia, nilimwona mara nyingi akizungumza na wagonjwa. Jamaa za wagonjwa walikuja nyumbani kwetu kumshukuru mama yangu, nilifurahi sana. Wakati huo huo nilikuwa nataka kufanya kazi kama ya mama yangu. Kwa kuwa nafanya kazi hapa, ninapaswa kufanya kazi vizuri. Na sasa napenda kazi yangu. "

Katika hospitali ya kwanza iliyoko chini ya chuo kikuu cha udaktari cha Xinjiang, kuna wauguzi wengine wengi kama Bi. Ma Binna na Bi. Sahipjamal, ambao wanafanya kazi kwa makini bila kujali uchovu na kutoa mchango kwa ajili ya afya za watu wa makabila madogo madogo mkoani Xinjiang.

Idhaa ya kiswahili 2007-09-13