Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-14 19:45:57    
Ndoa kwenye kituo cha kuwazlzimisha watumiaji kuacha kutumia dawa za kulevya

cri

Hivi karibuni, shamrashamra zilionekana kwenye kituo cha kuwalazimisha watumiaji wa dawa za kulevya waache kutumia dawa za kulevya, mji wa Kunming mkoani Yunnan. Watumiaji wanne wa dawa za kulevya walikuwa wanafunga ndoa. Hii ni mara ya kwanza kwa watu wanaolazimishwa kuacha kutumia dawa za kulevya kufunga ndoa kwenye kituo kama hicho kulevya nchini China. Leo katika kipindi hiki tunawaletea maelezo kuhusu jinsi Wang Jingying na Zhang Qing walivyofunga ndoa.

Mwendeshaji aliwauliza: "mnapenda kuoana?

Bi harusi na Bw harusi walijibu: "Ndio tunapenda!"

Wasikilizaji wapendwa, mliyosikia ni majibu ya Bw harusi Zhang Qing na Bi harusi Wang Jingying siku ya harusi yao. Wazazi wao na marafiki zao walipiga makofi na kuwapongeza. Bi. Wang Jingying na Bw. Zhang Qing waliwahi kuondokana na maisha ya kawaida kutokana na kutumia dawa za kulevya. Walifahamiana baada ya kuingia kwenye kituo cha kuwalazimisha watumiaji wa dawa za kulevya waache kutumia dawa za kulevya, wakapendana na hatimaye wakafunga ndoa.

Bi harusi Wang Jingying ni mwenye uwezo wa aina mbalimbali aliwahi kuwa msichana aliyependwa na wazazi wake na walimu wake. Tangu mwanzoni mwa miaka ya 90 ya karne iliyopita, dawa za kulevya zilikuwa zikiingia sehemu mbalimbali nchini China kutoka mkoani Yunan, Bi. Wang Jingying ambaye wakati huo alikuwa kijana, hakujua madhara ya dawa za kulevya, alijaribu kutumia dawa za kulevya, na baadaye akawa na uraibu wa dawa za kulevya na hakuweza kujizuia. Pia alipoteza vitu vingi vizuri katika maisha yake, aliachwa na mchumba wake na alifukuzwa kazini. Mama yake alisikitika sana na kufa moyo kutokana na hali ya binti yake. Bi. Wang Jingying alijaribu kujilazimisha kuacha tabia ya kutumia dawa za kulevya, lakini alishindwa, alisema.

"baada ya miaka mingi kupita, niliona njia hiyo ni ngumu sana."

Bi. Wang Jingying aligunduliwa na polisi alipotumia dawa za kulevya, na baadaye alipelekwa kwenye kituo cha kuwalazimisha watumiaji kuacha kutumia dawa za kulevya. Mfanyakazi wa kituo hicho alisema, Bi. Wang Jinying alipopelekwa kwenye kituo hicho, alikuwa anatumia dawa za kulevya ambapo alionekana na hali ambayo hata yeye mwenyewe hawezi kujidhibitiwa. Kituo hicho kilimpima afya na kumpangia utaratibu wa kumfanya aache kutumia dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi wa kazi kwa wanafunzi wa kituo cha kuwalazimisha watumiaji kuacha kutumia dawa za kulevya cha Kunming Bw. Li Jing alisema: "

"kutokana na kuwa alitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu, maisha na kula kwake si kwa kawaida, na kinga yake ni dhaifu. Hivyo tulimwongezea nguvu kwa kumdunga sindano ya Glucose, alikuwa anapona siku hadi siku. Baadaye akaweza kufundishwa na tukamfundisha mambo kadhaa kuhusu sheria".

Kituo cha kuwalazimisha watumiaji waache kutumia dawa za kulevya cha Kunming kilimpanga Bi. Wang Jingying kwenye idara ya usimamizi wa mafunzo ya wanawake. Kuna wanawake zaidi ya elfu moja wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya, kila siku wanaishi pamoja na kufundishana, wanajifunza ufundi wa ajira na kutengeneza vitu mbalimbali. Bi. Wang Jingying na wenzake walipata ufuatiliaji na mafunzo kutoka kwa walimu wao katika maisha yao na mambo mbalimbali ya jamii. Mwalimu wa kituo hicho Bw. Yao Dunyi alisema:"

"walitaka kuacha kabisa kutumia dawa za kulevya, lakini kutokana na kutegemea dawa za kulevya moyoni, hawawezi kuacha mara moja, huenda watatumia muda mrefu na hata maisha yote, ili kuondokana kabisa na dawa za kulevya, hivyo huo ni mchakato mgumu sana. Mtumiaji wa dawa za kulevya ni mtu anayepata madhara, alifanya makosa kutumia dawa za kulevya, tunapaswa kumsaidia na kumwokoa. "kuna vijana wengi walioacha kutumia dawa za kulevya kwenye kituo hicho, kwa ajili ya kustawisha maisha ya utamaduni ya watu wanaoacha kutumia dawa za kulevya, kituo hicho kilianzisha kikundi cha sanaa. Kwa kuwa wengi wao wanajua kuimba nyinbo na kufanya maonesho ya michezo ya sanaa, Bi. Wang Jingying na Bw. Zhang Qing walichaguliwa kujiunga na kikundi hicho. Walifahamiana kwenye kikundi hicho. Kituo hicho kilikuwa na waalimu wa kuwaongoza kufanya mazoezi kila siku, walianza kufahamiana kwenye mchakato huo. Bw. Zhangqing anapenda muziki na anaweza kupiga vinanda mbalimbali, pia alikuwa anatunga muziki. Kabla ya kupelekwa kwenye kituo cha kuacha kutumia dawa za kulevya, Bw. Zhang Qing alikuwa anaimba kwenye baa ya karaoke, lakini alitumia dawa za kulevya kwa sababu ya kuwa na rafiki mbaya.

Maonesho ya michezo ya sanaa ya kikundi hicho yaliandaliwa na watumiaji wanaoacha kutumia dawa za kulevya, ambayo yalionesha hali ya maisha yao na mabadiliko ya fikra kwenye kituo hicho. Bi. Wang Jingying na Bw. Zhang Qing walisema hao wawili kila mmoja anajihisi mabadiliko yake mwenyewe na ya mwingine na wote wamelewa umuhimu wa maisha na jukumu lao, na sasa wanmekuwa na matumaini tena na maisha.

Kutokana na kuwa na hali inayofanana, kuwa na hamu na upendo wa namna moja na kuweza kuwasiliana kila siku, Bi. Wang Jingying na Bw. Zhang Qing walikuwa wanapendana siku hadi siku. Mwishowe Bw. Zhangqing alimwambia Bi. Wang Jingying kuwa anataka kumwoa. Lakini Bi. Wang Jingying alifikiria suala hilo, na aliona kuwa kufunga ndoa kwenye kituo cha kuwalazimisha kuacha kutumia dawa za kulevya ni jambo lisilowezekana.

"alipozungumza kufunga ndoa, nilishangaa, nilikuwa sikuthubutu kufikiri jambo hili kwani niliona hatua msingi wa kiuchumi tena hatuwezi kufunga ndoa katika kituo hiki."

Lakini baada ya viongozi wa kituo hicho kuambiwa uamuzi wa Bw. Zhang Qing, walimpa uungaji mkono mkubwa. Kituo hicho kiliwaandalia nyumba mpya na kuwanunulia zawadi nyingi. Bw. Lijing alisema: "

"wakati huo niliona kuwa yeye alikuwa anatarajia kuishi kama mtu wa kawaida, na alikuwa anafikiria kuwa na familia."

Tarehe 12 mwezi Februari mwaka 2007, Bi. Wang Jingying na Bw. Zhang Qing walikwenda kujiandikisha kwenye ofisi inayotoa cheti cha ndoa, na si muda mrefu baadaye walifunga ndoa na kituo hicho kiliwaalika wazazi wao kuja kuhudhuria harusi yao. Baada ya kufanya harusi, walipanda mti wa msonobari ambapo walifurahi sana. Bw. Zhang Qing alisema: "

"Ninafuraha sana, nimepata maisha mazuri.

"Nimeridhika sana."

Idhaa ya kiswahili 2007-09-13