Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-18 15:31:21    
Kisiwa cha Changxing chaongoza kwenye wimbi la uwekezaji

cri

Kisiwa cha Changxing kiko mkoani Liaoning, kaskazini mashariki mwa China. Katika miaka ya hivi karibuni, kisiwa hicho kimekuwa kinawavutia wawekezaji wengi wa nchini na wa nje siku hadi siku. Zamani kilikuwa kisiwa kidogo kisichojulikana kwa watu wengi, lakini kutokana na uungaji mkono wa sera za serikali ya China kustawisha kituo kikongwe cha viwanda vya kaskazini mashariki, na mkoa wa Liaoning kuharakisha maendeleo na ufunguaji mlango wa uchumi, kisiwa cha Changxing kinaongoza kwa wimbi la uwekezaji wa sehemu za kaskazini mashariki mwa China kutokana na mwendo wake wa kasi wa uendelezaji na ujenzi.

Eneo la nchi kavu la kisiwa cha Changxing ni kilomita za mraba zaidi ya 250, kisiwa hicho kina mwambao wenye urefu wa zaidi ya kilomita 90, ni kisiwa kikubwa cha 5 nchini China. Kisiwa hicho ni sehemu ya Dalian, na sehemu ya mwambao ya kisiwa hicho inaweza kutumika kujengwa bandari na kuendeleza viwanda vya karibu na bandari. Mwaka 2005 mkoa wa Liaoning uliamua kujenga kisiwa cha Changxing kwa nguvu zote za mkoa huo, ili kiwe kituo cha viwanda vya karibu na bandari na kiwe moja ya bandari kubwa za kituo cha usafiri na uchukuzi wa kimataifa cha Dalian.

Ofisa mhusika wa sehemu za viwanda vya karibu na bahari za kisiwa cha Changxing Bw. Fan Hui alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, kisiwa cha Changxing kimepata fursa ya maendeleo ya kihistoria. Alisema,

"Mwaka 2003, serikali kuu ya China ilitoa sera ya kustawisha kituo kikongwe cha viwanda vya kaskazini mashariki, na mwaka 2005 ilizidi kupanua ufunguaji mlango wa sehemu za kaskazini mashariki, ndipo kisiwa cha Changxing kilipoorodheshwa kuwa eneo la uendelezaji. Katibu wa kamati ya mkoa wa Liaoning Bw. Li Keqiang alisema lazima kuendeleza na kujenga kisiwa cha Changxing kwa nguvu zote za mkoa huo, na kukipa kisiwa hicho Yuan za RMB bilioni 3, ili zitumike kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu nje ya kisiwa hicho. Aidha, benki ya maendeleo ya China pia ilitoa mikopo yenye unafuu ya Yuan za RMB bilioni 8 kwa kisiwa hicho, ambayo ilitoa fedha kwa ujenzi wa miundo mbinu wa kipindi cha mwanzoni wa kisiwa hicho."

Miaka miwili iliyopita, kisiwa cha Changxing ambacho kilikuwa na watu 40,000 tu, kilikuwa kisiwa kidogo kisichojulikana kwa watu wengine. Lakini anuani kipekee ya kijiografia, na mazingira mazuri ya kimaumbile, vimeweka msingi kwa ustawi wa haraka wa kisiwa hicho katika siku za baadaye. Katika miaka miwili iliyopita, uendelezaji na ujenzi wa kisiwa cha Changxing umeharakishwa zaidi. Hivi sasa, kazi za uhamiaji wa wakazi wa kisiwa hicho, kutoa matangazo na kuvutia wafanyabiashara, na ujenzi wa bandari, reli na barabara unaendelea kwa utaratibu. Imefahamika kuwa, miradi mikubwa ya miundo mbinu nje ya kisiwa hicho, kama vile reli inayoelekea kisiwani, barabara ya mwendo kasi, utoaji wa umeme na maji, hivi sasa yote imeanzishwa, na inaendelea vizuri. Bw. Wang Jun ni mkazi wa kisiwa hicho. Alipozungumzia maendeleo na mabadiliko mapya ya kisiwa hicho katika miaka hiyo miwili, alisema,

"Katika miaka hiyo miwili, kisiwa cha Changxing kimekuwa na mabadiliko makubwa, kwa mfano, serikali ilitusaidia kutatua masuala ya utoaji wa umeme na maji, pia ilijenga barabara ya mwendo kasi, na tunasikia kuwa itajenga reli inayoelekea kwenye kisiwa chetu. Hadi kufikia wakati huo, sisi wakazi wa kisiwa cha Changxing tutasafiri kwa urahisi zaidi, hakika makampuni mengi zaidi yatawekeza vitega uchumi hapa."

Katika uendelezaji na ujenzi, kisiwa cha Changxing kinatilia maanani ushirikiano wa kimataifa, na kuzingatia kujifunza uzoefu wa kisasa wa nchi zilizoendelea. Katika upande huo, ushirikiano wa kunufaishana kati ya kisiwa cha Changxing na kampuni ya Singapore ni mfano mzuri wa kuigwa. Ili kujifunza uzoefu wa Singapore katika mpango na ujenzi wa kisiwa, mpango wa sehemu ya viwanda ya kisiwa cha Changxing uliajiri kampuni maarufu ya Singapore kufanya usanifu. Ofisa mhusika wa mpango huo Bw. Fan Hui alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema,

"Mwezi Agosti mwaka 2006, kwenye mkutano wa 3 wa 'kamati ya ushirikiano wa China na Singapore', Naibu waziri mkuu wa China Bibi Wu Yi alitoa kuunga mkono ushirikiano kati ya kisiwa cha Changxing na Singapore. Ushirikiano huo ni pamoja na mpango wa ujumla, viwanda vya usimamizi na uwekezaji, utalii, elimu, utoaji mafunzo ya watu wenye ujuzi, ujenzi wa mawasiliano ya habari na hifadhi ya mazingira, na utoaji mafunzo kwa watumishi wa serikali."

Ofisa wa mkoa wa Liaoning alisema, kuendeleza na kujenga kisiwa cha Changxing ni sehemu muhimu ya kuharakisha ustawishaji wa kituo kikongwe cha viwanda vya Liaoning na ujenzi wa kituo cha safari za ndege za kimataifa cha Dalian, pia kuna umuhimu mkubwa kwa ufunguaji mlango na uhimizaji wa maendeleo ya uchumi wa sehemu za katikati za Liaoning hata peninsula ya Liaodong. Wakati wa kufanya uendelezaji na ujenzi, idara husika zinatambua umuhimu wa hifadhi ya mazingira kwa maendeleo endelevu ya kisiwa hicho.

Naibu katibu wa sehemu ya viwanda ya kisiwa cha Changxing iliyo karibu na bandari Bw. Chen Guangyin alipohojiwa alisema, viongozi wa sehemu hiyo wanatambua kuwa hifadhi ya mazingira na matumizi mazuri ya maliasili yatakuwa sehemu muhimu katika maendeleo ya uchumi, hivyo wanazingatia kujifunza uzoefu wa kisasa wa Singapore katika kuhifadhi mazingira na kutumia maliasili.

Kwa mujibu wa mpango wa uendelezaji na ujenzi wa kisiwa cha Changxing, hadi kufikia mwaka 2010, kisiwa hicho kitakuwa kimekamilisha ujenzi wote wa miundo mbinu, ambapo kitaunda katika hatua za mwanzo eneo la uzalishaji karibu na bandari, ambalo uzalishaji wa zana za kuzalisha mitambo utachukua nafasi muhimu, na kujenga magati matano ya ngazi ya tani elfu 50 hadi 70, kupokea baadhi ya kazi za usafirishaji wa bandari ya Dalian, na kuanza kupokea kazi za usafirishaji kwenye sehemu nyingine duniani.

Idhaa ya kiswahili 2007-09-18