Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-19 18:35:48    
Mapishi ya kamba-mwakaje na vitunguu saumu

cri

Mahitaji

Kamba-mwakaje gramu 500, limao moja, vitunguu saumu gramu 10, vitunguu maji gramu 5, mchuzi wa sosi vijiko viwili, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, wanga wa pilipili manga kijiko kimoja

Njia

1. osha kamba-mwakaje, ondoa vichwa vyake.

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu saumu na vitunguu maji, korogakoroga, mimina juisi ya limau, mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, korogakoroga, tia wanga wa pilipili manga, sukari, mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga, mimina maji yasiyo ya baridi, korogakoroga halafu weka kwenye kamba-mwakaje.

3. chemsha maji kwenye sufuria, weka kamba-mwakaje kwenye sufuria, chemsha kwa mvuke kwa dakika 10. mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.