Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-25 15:15:13    
Mongolia ya ndani yaendeleza chapa za bidhaa zisizo na uchafuzi

cri

Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China una mbuga kubwa. Maliasili za kipekee zilizoko kwenye mkoa huo zimeyapatia makampuni mengi yanayotengeneza mazao ya kilimo na bidhaa za mifugo manufaa makubwa, baadhi ya makampuni yakitumia utamaduni wa mbugani yalianzisha chapa nyingi maarufu za bidhaa. Katika kipindi hiki cha nchi yetu mbioni, tutawaelezea jinsi mkoa huo ulivyoanzisha chapa maarufu za bidhaa zisizo na uchafuzi kwa mazingira.

Kampuni ya Erdos ni kampuni kubwa inayojihusisha na utengenezaji wa bidhaa za cashmer laini. Kampuni hiyo inazalisha nguo zaidi ya milioni 10 za cashmer laini kwa mwaka, ambazo zinachukua asilimia 30 duniani. Kutokana na uzalishaji mkubwa na kuwa na sifa nzuri, nguo nyingi za sufu za aina hiyo zinazotengenezwa na kampuni hiyo zinauzwa katika nchi za nje. Erdos si kama tu imekuwa chapa maarufu nchini China, bali pia imekuwa chapa inayopendwa na wanunuzi wa nchi za nje.

Ingawa mbuga kubwa iliyoko Mkoani humo imeipatia kampuni ya Erdos raslimali nyingi, lakini kampuni hiyo imefanya juhudi kubwa ili kuanzisha chapa hiyo maarufu. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Yang Zhiyuan alisema, kampuni hiyo inatilia maanani matumizi ya teknolojia katika utengenezaji wa bidhaa ili kuanzisha chapa maarufu, alisema,

"Kampuni yetu inaendelea na utafiti kuhusu bidhaa za cashmer laini, kwa mfano mwaka 2005 tulivumbua bidhaa za sufu za aina hiyo ambazo si rahisi kuchafuliwa na maji, mafuta na mavumbi, na mwaka jana tulivumbua bidhaa za sufu ambazo si rahisi kusababisha cheche (static electricity), tutatumia teknolojia nyingi zaidi za kisasa kwenye utengenezaji wa bidhaa."

Bw. Yang Zhiyuan anaona kuwa bidhaa zilizotengenezwa na kampuni hiyo kwa teknolojia ya kisasa ni sababu muhimu iliyoisaidia kampuni ya Erdos kuanzisha chapa maarufu. "Kwenye mbuga kubwa iliyoko chini ya anga ya kibuluu, ng'ombe na kondoo wanajificha kwenye nyasi ndefu. Maziwa yanayonukia ya kampuni ya Yili ni maarufu." Hayo ni maneno ya matangazo ya kampuni ya Yili kwenye televisheni. Mbuga kubwa na mazingira yasiyo na uchafuzi yameipatia kampuni ya Yili chapa ya bidhaa zisizochafuliwa, na chapa hiyo inaihimiza kampuni hiyo itilie maanani sifa ya bidhaa za maziwa. Meneja mkuu wa kampuni ya Yili Bw. Pan Gang alisema kuzalisha maziwa yenye sifa nzuri ni uhakikisho wa mafanikio ya kampuni ya Yili, alisema,

"Bidhaa za kampuni yetu zimekuwa zinafurahiwa na wanunuzi kwa miaka mingi iliyopita, sababu kubwa zaidi ni sifa ya bidhaa zetu, siku zote tunazingatia maendeleo ya kampuni yetu kwa ajili ya maslahi ya wateja, na tunafikiria vipi tunaweza kuwawezesha wachina wapate maziwa yenye sifa nzuri."

Bw. Pan Gang alisema makampuni ya bidhaa za maziwa yanatakiwa kutilia maanani ujenzi wa vituo vya kuzalisha maziwa, kwa sababu ni lazima bidhaa za maziwa zenye sifa nzuri zitengenezwe kwa maziwa yenye sifa nzuri. Hivyo kampuni ya Yili ilianzisha malisho kadhaa maalum ya ng'ombe, na yanawapatia wafugaji aina moja ya chakula cha mifugo na ng'ombe, ili kuhakikisha sifa za maziwa. Hivi sasa chapa nyingi za bidhaa zisizo na uchafuzi zimeanzishwa mkoani Mongolia ya Ndani, Takwimu zinaonesha kuwa, moja kati ya chapa 1600 za bidhaa mkoani humo imewekwa kwenye orodha ya chapa maarufu na idara za viwanda na biashara ya China.

Mbuga kubwa imeyapatia makampuni hayo uwezo wa kupata maendeleo na nguvu za uhai; wakati huo huo, makampuni hayo yamekuwa nguvu kubwa ya kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na jamii mkoani humo. Kazi moja muhimu ya makampuni hayo ni kuongeza nafasi za ajira. Kwa mfano Kampuni ya mikahawa ya Xiaofeiyang ya mji wa Baotou imetoa nafasi za ajira zaidi ya elfu 6, na kuwanufaisha watu zaidi ya laki 2. Kampuni ya Yili imetoa nafasi za ajira elfu kumi kadhaa kwa wakulima na wafugaji wa sehemu ambazo maendeleo ya uchumi yako nyuma. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2006, kwa ujumla kampuni hiyo ilitumia Yuan bilioni 10 kununua maziwa, fedha hizo zimezisaidia familia milioni kadhaa zinazofuga ng'ombe kujiendeleza.

Bw. Cao Youtang anayeishi huko Baijiayingzi kijijini Gucheng wilayani Tuoketuo alishiriki kwenye kazi ya ufugaji wa ng'ombe katika malisho ya ng'ombe ya kampuni ya Yili. Katika miaka mitatu iliyopita, ng'ombe wake waliongezeka na kuwa zaidi ya 50 kutoka zaidi ya 10, na uwezo wa kuzalisha maziwa pia umeongezeka. Bw. Cao anaridhika na hali hiyo, alisema,

"Baada ya kutumia chakula kinachotolewa na kampuni ya Yili kuwafuga ng'ombe, si rahisi kwa ng'ombe kupata magonjwa, tena wanaweza kutoa maziwa mengi zaidi. Zamani kila ng'ombe alikuwa anaweza kutoa lita 25 za maziwa, na sasa anaweza kutoa lita 60 hadi 70 za maziwa."

Aidha, makampuni hayo pia yamesukuma mbele maendeleo ya shughuli za uendelezaji wa malighafi, uchukuzi na ufungaji wa bidhaa pia yameinua nguvu ya kiuchumi ya mkoa huo, na kuwavutia wawekezaji na wataalamu. Uungaji mkono wa serikali ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ni muhimu sana kwa maendeleo ya makampuni hayo. Meya wa mji wa Huhhot Bw. Tang Aijun alisema, serikali haizuii maendeleo ya makampuni hayo, na inayahimiza yaingie kwenye masoko ya nchini hata duniani, alisema,

"Tunayahimiza makampuni hayo yajiendelee katika sehemu mbalimbali duniani. Baadhi ya miji hairuhusu makampuni yajitafutie maendeleo katika sehemu nyingine, lakini tunayahimiza yaingie kwenye masoko ya nchini na duniani, yafanye ushidani masokoni kwa njia nzuri na halali. Kama baadhi ya makampuni yanajaribu kuharibu sifa za makampuni hayo, tutachukua hatua za kiutawala."

Idhaa ya kiswahili 2007-09-25