|
Tarehe 25 mkutano mkuu wa 62 wa Umoja wa Mataifa ulifanya mkutano wa kawaida. Siku hiyo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon, mwenyekiti wa mkutano huo Bw. Srdjan Kerim pamoja na viongozi wa nchi 27 kutoka Brazil, Marekani, Ufaransa, Iran na nchi nyingine walitoa hotuba na kueleza misimamo yao kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa, mabadiliko ya hali ya hewa?maendeleo na haki za binadamu.
Mkutano wa kawaida ni kikao muhimu kinachofanyika baada ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kufunguliwa. Kwa kawaida watu wanaotoa hotuba katika kikao hicho ni marais na viongozi wa serikali, ambao wanaeleza misimamo ya nchi zao kuhusu masuala makubwa duniani. Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa ni mkutano wa kwanza baada ya Bw. Ban Ki-moon kushika wadhifa wa katibu mkuu wa Umoja huo. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo alisisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa ukiwa ni shirika pekee la nchi zote duniani unapaswa kutoa mchango unaostahili katika mapambano dhidi ya changamoto kubwa duniani. Alisema anatumai kuwa nchi zote wanachama zitafanya juhudi kwa pamoja, na kuendelea kusukuma mageuzi ya Umoja wa Mataifa ili kuufanya Umoja huo uwe shirika la nchi zote linaloaminika. Kwa utani alisema, wakati wajumbe wa nchi mbalimbali wanapozungumzia mabadiliko ya hali ya hewa, kwanza wasaidie Umoja wa Mataifa upate "mabadiliko ya hali ya hewa", yaani kuondoa mtindo mbaya wa kazi na kuanzisha mtindo mpya wenye ufanisi zaidi.
Mwenyekiti wa mkutano huo Bw. Srdjan Kerim kwenye hotuba yake alisisitiza kuwa, mkutano huo una mada tano, yaani mabadiliko ya hali ya hewa, kuimarisha ukusanyaji fedha, malengo ya milenia, mapambano dhidi ya ugaidi na mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Alisema anatumai kuwa nchi zote wanachama zitatumia hali nzuri ya hivi sasa ambayo jumuiya ya kimataifa imelipa uzito suala la mabadiliko ya hali ya hewa, zichukue hatua na kuondoa vizuri tofauti kati ya maendeleo ya uchumi na uchafuzi wa mazingira. Alisema ingawa mali za binadamu zinaongezeka, lakini hali ya tofauti kati ya matajiri na maskini bado ipo. Alisema hivi sasa nusu ya watu wote duniani hawapati dola mbili kwa siku, watoto milioni mia moja hawawezi kupata elimu kwa sababu ya umaskini. Amezitaka serikali za nchi zote zitambue umuhimu wa kutimiza malengo ya milenia. Alisema wakati tunapoona kweli sote ni wa familia moja, na kuwa na wajibu na majukumu ya pamoja ndipo tutakapojitahidi kikweli kutimiza malengo hayo.
Kutokana na desturi, mjumbe wa Marekani hupangwa mtu wa pili kutoa hotuba katika mkutano huo. Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani kila ilipokuwa jukwaani ilikuwa inazikosoa nchi nyingine na kujitafutia malalamiko mengi, hali hiyo iliendelea kuwepo kwenye mkutano wa mwaka huu. Lakini ikiwa ni mara ya mwisho kushiriki kwenye mkutano huo, rais wa Marekani Bw George Bush tofauti na desturi hiyo, alitoa hotuba ya upole. Ingawa alizinyooshea kidole nchi nyingine, lakini hakutumia maneno makali, na zaidi ya hayo hakuzungumzia sana "tishio la nyuklia" la Iran kama ilivyotarajiwa na baadhi ya wajumbe. Ikilinganishwa na Bw George Bush, rais wa Ufaransa Bw. Nicolas Sarkozy ambaye ameshiriki kwa mara ya kwanza kwenye mkutano huo, alionekana kuwa na msimamo mkali kuhusu suala la nyuklia la Iran. Alisema Iran ina haki ya kuendeleza teknolojia ya nyuklia kwa ajili ya maendeleo kiuchumi, lakini ikiruhusiwa kuendeleza silaha za nyuklia italeta tishio kubwa kwa utulivu wa kikanda na hata kwa dunia nzima, na "Mkataba wa Kutoeneza Silaha za Nyuklia" pia utakuwa hatarini, hii haiwezi kukubalika. Kwa hiyo Ufaransa inatetea kufanya mazungumzo na Iran kwa msimamo mkali.
Mtu aliyefuatiliwa zaidi ni rais Mahmud Ahmadinejad wa Iran aliyetoa hotuba saa chache baada ya rais George Bush kuondoka jukwaani. Ingawa hakutaja jina, lakini kwenye hotuba yake ilikuwa wazi kuwa anailenga Marekani. Aliishutumu Marekani kwa kukiuka "Katiba la Umoja wa Mataifa", kutumia vigezo viwili tofauti, na ingawa vita vya pili vimemalizika miaka zaidi ya 60 lakini inaendelea kushughulika na mambo ya kimataifa kwa ujeuri wa nchi iliyoshinda vita, na kukiuka haki za nchi nyingine, kuchafua heshima ya Umoja wa Mataifa, na inaonekana kama ni pandikizi na kujivunia kama ni Mungu, lakini kwa kweli ni dhaifu hata inashindwa kushughulikia matatizo nchini mwake. Ingawa ombi la Ahmadinejad la kutembelea mabaki ya jengo la WTC na kulumbana na George Bush ana kwa ana lilikataliwa, lakini alipata fursa ya kutoa hotuba kwenye Chuo Kikuu cha Columbia na baada ya hotuba alikutana na waandishi wa habari.
Idhaa ya kiswahili 2007-09-26
|