Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-26 19:13:33    
Mapishi ya firigisi za kuku

cri

Mahitaji

Firigisi za kuku gramu 200, pilipili mboga moja, tangawizi gramu 5, pilipili manga gramu 2, vitunguu saumu gramu 5, mchuzi wa chaza gramu 5

Njia

1. chemsha maji, halafu weka firigisi ya kuku kwenye maji ya moto, halafu zipakue, na uziweke kwenye maji ya baridi. Kata firigiri ya kuku iwe vipande.

2. kata tangawizi, vitunguu saumu, pilipili mboga iwe vipande.

3. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi, vitunguu saumu na pilipili manga kwenye sufuria, korogakoroga, tia firigisi za kuku kwenye sufuria, pilipili mboga, korogakoroga, mimina mchuzi wa chaza, korogakoroga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.