Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-28 16:20:04    
Mkutano wa pande sita kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea wafunguliwa

cri

Mkutano wa kipindi cha pili cha mazungumzo ya pande sita ya duru la sita kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea ulifunguliwa tarehe 27 Beijing, wajumbe kutoka nchi sita husika China, Korea ya Kaskazini, Korea ya Kusini, Marekani, Japan na Russia wanahudhuria mkutano huo. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo naibu waziri wa mambo ya nje wa China ambaye ni mkuu wa ujumbe wa China Bw. Wu Dawei aliiwakilisha serikali ya China kuwakaribisha wajumbe, na alisisitiza umuhimu wa mkutano huo. Alisema,

"Huu ni mkutano muhimu katika mchakato wa mazungumzo ya pande sita, kazi yake ni kujadili na kubaini mpango wa utekelezaji wa kipindi kijacho."

Tokea mwezi Agosti mwaka 2003 mazungumzo ya pande sita, China, Korea ya Kaskazini, Korea ya Kusini, Marekani, Japan na Russia, kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yaliingia katika duru la sita. Mwezi Machi mwaka huu mazungumzo ya duru la sita yalianza mkutano wake wa kipindi cha kwanza, na mwezi Julai ulifanywa mkutano wa wakuu wa ujumbe wa pande sita. Bw. Wu Dawei alieleza kuwa kwa mujibu wa maoni waliyopata wakuu wa ujumbe kwenye mkutano huo, vikundi vitano vya kazi vilifanya mikutano na vilijadili mipango ya utekelezaji wa fani mbalimbali. Pande hizo ziliwahi kufanya majadiliano kuhusu masuala yanayofuatiliwa. Vyombo vya habari vinaona kuwa mkutano wa sasa utakuwa kama mazungumzo yaliyopita kwamba hakika utakabiliwa na matatizo mengi na changamoto kubwa. Naibu profesa wa chuo cha sayansi ya jamii cha China Bw. Liu Weidong alieleza,

"Kati ya matatizo hayo, kwanza kabisa ni namna ya kutimiza matakwa ya Marekani ya kuifanya Korea ya Kaskazini ipoteze kabisa uwezo wake wa nyuklia na isiweze kurudia tena. Pili ni tatizo linalohusu orodha kamili ya mpango wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mpango wa kusafisha uranium na kuwepo kwa silaha za nyuklia na kama zipo basi namna ya kuzishughulikia. Tatu ni tatizo linalohusu kuenea kwa silaha za nyuklia. Na tatizo la mwisho ni fidia kwa Korea ya Kaskazini wakati inapokuwa katika mchakato wa kuacha kutengeneza silaha za nyuklia ikiwa ni pamoja na ahadi za usalama, na mali."

Jambo linalotiliwa maanani ni kwamba kabla ya mkutano huo pande mbili muhimu, Marekani na Korea ya Kaskazini, zote ziliwahi kusema mkutano huo umeingia katika kipindi muhimu, na ziliwahi kuwasiliana mara nyingi. Naibu profesa Sun Ru wa ofisi ya mambo ya Marekani katika Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa cha China alisema,

"Umuhimu wa Marekani ni kupata maendeleo katika suala la kuifanya Korea ya Kaskazini ipoteze kabisa uwezo wake wa kutengeneza silaha za nyuklia. Kwa sababu serikali ya Marekani imeharakisha utatuzi wa suala la silaha za nyuklia la peninsula ya Korea na kutumai kuwa Korea ya Kaskazini itatoa mpango wake wa nyuklia kabla ya mwishoni mwa mwaka huu na kutatua kabisa suala la nyuklia la peninsula ya Korea katika mwaka 2008. Jambo muhimu kwa upande wa Korea ya Kaskazini ni kuwa Marekani ikubali kuiondoa Korea ya Kaskazini kwenye orodha ya nchi za kigaidi na kuondoa vikwazo vya kiuchumi."

Licha ya pande hizo mbili, pande nyingine pia zinatilia maanani sana mkutano huo na zinajitahidi kuwasiliana pande mbili mbili. Mkuu wa ujumbe wa China kwenye ufunguzi wa mkutano huo alisema, kutokana na juhudi za pamoja mazungumzo ya pande sita yamekuwa yakiendelea kwenye njia sahihi, kipindi cha kufanikiwa kinaonekana kukaribia. Alisema,

"Natumai kuwa pande zote zitakuwa na moyo wa kunufaishana na kutumia vizuri fursa ya mkutano huo kwa ushupavu kuvuka matatizo na vikwazo vyote na kuyapeleka mazungumzo haya kwenye ngazi mpya."

Idhaa ya kiswahili 2007-09-28