Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-03 20:03:02    
Mapishi ya mbavu za nguruwe na vitunguu

cri

Mahitaji: Mbavu za nguruwe gramu 200, vitunguu gramu 50, pilipili mboga gramu 50, mchuzi wa sosi vijiko viwili, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, tangawizi gramu 5, vitunguu saumu gramu 5.

Njia:

1. Osha mbavu za nguruwe, halafu changanya na mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia na ukoroge pamoja.

2. Washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia vitunguu, tangawizi, vitunguu saumu, pilipili mboga, korogakoroga kisha zipakue.

3. tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia mbavu za nguruwe zikaange, mimina mvinyo wa kupikia, mimina maji kwenye sufuria, yachemshe. Baada ya kuchemka, tia mchuzi wa sosi, tia vitunguu, tangawizi, vitunguu saumu na pilipili mboga korogakoroga, tia punguza moto kidogo, endelea kuchemsha kwa dakika 40. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.