Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-04 17:20:34    
Vitu vya kuchezea watoto vinavyotengenezwa nchini China vyawafurahisha watoto wa nchi mbalimbali

cri

Katika sehemu mbalimbali duniani, vitu vya kuchezea watoto ni marafiki wa watoto, vitu hivyo vinawaletea furaha watoto.

China ni nchi yenye historia ndefu, mabadiliko katika vitu vya kuchezea watoto vilivyotengenezwa nchini China yanatokea siku hadi siku. Zamani vitu vya kuchezea watoto vilikuwa ni vitu vya kawaida vinavyotumika katika maisha ya kila siku, na vingine vilikuwa ni vitu vilivyotengenezwa na wasanii kama vile tiara na shuttlecock. Vitu hivyo vinaweza kujenga afya, hivyo vinapendwa na watu wengi.

Bibi Liu Hang alipokuwa mtoto alicheza shuttlecock mara kwa mara pamoja wa marafiki zake. Alitufahamisha akisema:

"Tulipokuwa watoto tulipenda sana kukucheza mchezo wa shuttle cock, hasa sisi wasichana, tulitengeneza shuttlecock sisi wenyewe. Tulipokuwa tunacheza mchezo huo tulikuwa tunashindana, nani anaweza kupiga shuttlecock kwa mitindo tofauti ya aina nyingi zaidi, na nani anaweza kupiga shuttlecock kwa muda mrefu bila kukosea, kweli mchezo huo mzuri ulitufurahisha sana."

Kutokana na maendeleo ya uchumi wa China, hasa baada ya China kufungua mlango, aina za vitu vya kuchezea watoto zinaongezeka, vitu vya kuchezea watoto vinavyopendwa na watoto wengi duniani pia vinaingia kwenye soko la China. Viwanda vya China vinavyotengeneza vitu vya kuchezea watoto pia vilianza kutengeneza wanasesere, magari ya plastiki na kadhalika.

Hivi sasa, vitu vya kuchezea watoto vinavyotengenezwa nchini China, siyo tu ni marafiki wazuri wa watoto wa China, bali pia vinaleta furaha kwa watoto wa nchi mbalimbali duniani. Viwanda vyingi vinavyotengeneza vitu vya kuchezea watoto vinashirikiana na viwanda vya China. China imekuwa kituo kikubwa kabisa duniani cha kutengeneza vitu vya kuchezea watoto, na makampuni ya vitu vya kuchezea watoto ya nchi mbalimbali yanatengeneza bidhaa zao nchini China. Mwaka 2006, thamani ya bidhaa za vitu vya kuchezea watoto vinavyoagizwa kutoka nje imefikia dola za kimarekani bilioni 7, na kuchukua asilimia 70 ya soko la vitu vya kuchezea watoto duniani. Bidhaa hizo ziliagizwa na nchi na sehemu zaidi ya 160, na kuchukua sehemu muhimu katika masoko ya nchi za Umoja wa Ulaya, Marekani na Japan. Mkuu wa kiwanda kimoja cha kutengeneza vitu vya kuchezea watoto mkoani Zhejiang mashariki mwa China Bw. Ye Shangshui alitufahamisha akisema,

"Bidhaa zetu zote zinatengenezwa kwa mbao, na wengi kati ya wanaoagiza ni wateja kutoka Ulaya, Marekani, pia Japan. Wateja wa nchi za nje wanauza bidhaa zetu kwa kupitia kampuni ya biashara na nje. Kwa kawaida, wateja wanatoa sampuli au picha ya usanifu, sisi tunatengeneza kutokana na matakwa yao.

Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka jana China ilitengeneza vitu vya kuchezea watoto zaidi ya bilioni 22. Kila mwaka thamani ya biashara ya vitu vya kuchezea watoto ya China inaongezeka, watoto wengi zaidi wanapenda vitu vya kuchezea vilivyotengenezwa nchini China. Kamati ya usimamizi wa teknolojia ya Ujerumani hivi karibuni ilitoa taarifa kufahamisha hali ya kupima sifa ya vitu vya kuchezea watoto vilivyotengenezwa nchini China, na kusema uzalishaji wa vitu vya kuchezea watoto kutoka China ni salama zaidi kuliko wakati wowote uliopita."