Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-09 15:54:20    
Matumizi ya mfugaji wa kabila la Watibet Bw. Danzhencuo

cri

Mkoa wa Qinghai ulioko kwenye sehemu ya magharibi ya China, unajulikana duniani kwa "water tower" (mnara wa maji) wa bara la Asia, ziwa la Qinghai pamoja na vyanzo vya mito mitatu mikubwa ya Changjiang, Manjano, Lancang vina athari ya moja kwa moja maisha ya karibu nusu ya idadi ya watu wa dunia. Katika miaka ya hivi karibuni serikali katika ngazi mbalimbali pamoja na watu wa China walitenga nguvukazi na vitu vingi kwa ajili ya marekebisho na hifadhi ya mazingira ya sehemu hiyo, hivi sasa mazingira ya viumbe ya mkoa wa Qinghai yameboreshwa kwa udhahiri. Katika kipindi hiki maalum kuhusu "Kuwepo masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya kimaumbile mkoani Qinghai", tunawaletea maelezo ya pili kuhusu "matumizi ya mfugaji wa kabila la Watibet Bw. Danzhencuo".

Mkoani Qinghai kuna Ziwa Qinghai linalopendeza, Watibet waliotegemea ufugaji wanaishi kizazi kwa kizazi kandoni mwa ziwa. Zamani wafugaji wa kabila la Watibet walionekana kila mahali wanaswaga ng'ombe na kondoo huku wakiwa wameshika mijeledi; lakini mwandishi wetu wa habari alipokwenda huko, hakuona ng'ombe wala kondoo hata mmoja. Kwa nini? Mfugaji Danzhencuo alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema:

"Tuliuza ng'ombe na kondoo wote, ili kuhifadhi sehemu ya ziwa Qinghai na kuhifadhi mazingira."

Mfugaji Danzhencuo anaishi katika wilaya ya Haiyan, kilomita 30 ya kaskazini mashariki ya ziwa Qinghai, ambayo ni wilaya wanayoishi watu wa kabila la Watibet. Mwandishi wetu wa habari aliingia kwenye hema la Danzhencuo, alikaribishwa kuketi kwenye zulia jekundu. Mwenye nyumba hiyo Bw. Danzhencuo alimpa kinywaji cha kipekee cha kabila la Watibet?chai iliyopikwa pamoja na samli na chumvi ya Tibet, na chakula cha jadi?unga wa shayiri iliyokaangwa na mtindi wenye ladha chachu, na mke wa Bw Danzhencuo Yingsheng pia aliingia kwenye hema na kuleta pombe iliyotengenezwa kwa shayiri aina ya Qingke ya Tibet. Baada ya kunywa pombe hiyo, Yingsheng alizungumza na mwandishi wetu wa habari akisema:

"Zamani tulikuwa tunafuga ng'ombe 400 na kondoo 400, na kwa kutegemea kuuza ng'ombe na kondoo tuliweza kupata Yuan zaidi ya 10,000 kila mwaka. Lakini tungeweza kuishi vipi bila ya ng'ombe na kondoo? Sisi watu wa kabila dogo tuliishi kwa njia hiyo kizazi baada ya kizazi, hivyo wakati ule tuliona hatuwezi kuishi bila kuwa na ng'ombe na kondoo."

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuongezeka kwa joto duniani, sehemu ya malisho iliyo karibu na Ziwa Qinghai ilibadilika kuwa jangwa, na kusababisha kina cha maji kupungua siku hadi siku. Matokeo hayo yataathiri moja kwa moja mabadiliko ya hali ya hewa ya China na hata ya dunia. Ili kulinda uwiano wa viumbe kwenye sehemu ya Ziwa Qinghai, mwaka 2003 serikali ya China iliamua kutekeleza mradi wa kurudisha sehemu ya malisho katika sehemu ya Ziwa Qinghai, ili kuhifadhi malisho yaliyo karibu na ziwa hilo, na kuzuia mmomonyoko wa ardhi. Hivyo Bw. Danzhencuo na wafugaji wengine kijijini hapo waliuza ng'ombe na kondoo wao.

Bw. Danzhencuo alisema, mwanzoni wakati wa utekelezaji wa sera ya kurudisha sehemu ya malisho, wanakijiji wengi hawakuelewa sera hiyo. Lakini Bw. Danzhencuo alisema anaweza kuelewa sera hiyo, na kuona kuwa hilo ni jambo zuri.

Lakini wafugaji kuwa bila ya ng'ombe na kondoo, ni sawa na wakulima kutokuwa na mashamba, walipoteza vitu walivyotegemea, Je Bw. Danzhencuo na familia yake walitatua vipi tatizo la chakula? Bibi Yingsheng ni mtu mwerevu, aligundua kuwa magari mengi yanayobeba watalii yanapita mara kwa mara katika barabara iliyo mbele ya hema lao, hivyo alikuwa na wazo la kufanya biashara ya utalii ya "furaha kuishi nyumbani kwa Watibet". Serikali ya kijiji iliunga mkono wazo la Bibi Yingsheng, hivyo sio tu iliwasaidia kushughulikia utaratibu husika kwa haraka, bali pia iliwaondolea kodi ya uendeshaji, na kuwapa hema inayotumiwa kuwapokea wageni. Bibi Yingsheng alisema:

"Ruzuku tunazopewa na serikali kutokana na sera ya kurudisha malisho zitakwisha siku moja, lakini baada ya kufanya biashara ya utalii, maisha yetu yanahakikishwa. Mwazoni pia tulikuta matatizo mengi, kama vile hatukuweza kuongea kwa kichina sanifu, hivyo hatukujua wageni wanapenda kula nini, lakini polepole tulianza kufahamu."

Bw. Danzhencuo alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, baada ya sera ya kurudisha malisho ianze kutekelezwa, serikali iliwapa wafugaji sera nyingi zenye unafuu, na kutoa bure mafunzo mbalimbali, hivyo maisha yao sio mabaya kama zamani. Alisema katika kijiji chao, baadhi ya watu wanafanya kazi mijini, baadhi yao wanaendesha malori wakijishughulisha na kazi za uchukuzi, na wengine wanafanya biashara ya utalii kama familia yake ilivyo. Alipozungumzia biashara ya utalii, Bw. Danzhencuo alisema kwa furaha,

"'Furaha kuishi nyumbani kwa Watibet' ni njia nzuri sana! Watalii wengi wa sehemu za ndani za China wanapenda sana kuja hapa kunywa mtindi au chai yenye krimu, na katika miezi ya Julai na Agosti ya kila mwaka biashara inakuwa nzuri kabisa, na katika mwezi uliopita tulipata mapato ya Yuan zaidi ya 4,000."

Bibi Yingsheng alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, sasa ingawa hawana ng'ombe na kondoo, lakini jambo linalomfurahisha ni kwamba, binti na mwanaye waliacha maisha ya ufugaji, na kujiunga na shule kama watoto wa mijini walivyo, na serikali pia imefuta ada zao. Mwanaye anayeitwa Duokezhexi ana umri wa miaka 13. Alisema sasa kila siku anaweza kusoma na kuishi na watoto wengi, anafurahi sana; lakini pia anakumbuka siku alipokuwa anachunga mifugo pamoja na dada yake mkubwa, na wimbo waliokuwa wanaimba walipokuwa wanachunga mifugo:

Duokezhaxi alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, katika sikukuu ya wafanyakazi ya mwaka huu, walimu walitushirikisha kupanda miti, yeye alipanda miche 37. Ana matumaini kuwa Ziwa Qinghai litakuwa zuri siku hadi siku.

Aliposikia wimbo ulioimbwa na mwanaye na binti yake, Bw. Danzhencuo alisema, ana nia moja moyoni:

"Sasa tunafanya biashara ya utalii, serikali inatupa unafuu mwingi, watalii pia ni wengi, hivyo maisha yetu ni mazuri kuliko zamani! Baada ya mazingira yetu kubadilika kuwa mazuri, napenda kufanya tena kazi ya ufugaji, na kununua ng'ombe na kondoo 500, ili kuchuma pesa nyingi zaidi kwa ajili ya watoto kusoma katika vyuo vikuu!"

Idhaa ya kiswahili 2007-10-09