Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-10 16:40:55    
Kuzuia chanzo cha mito mitatu kisibadilike kuwa bahari ya uchafuzi mweupe

cri

Mkoa wa Qinghai ulioko magharibi mwa China unajulikana kama ni "Mnara wa maji wa Asia" duniani. Hali ya mazingira ya kimaumbile ya Ziwa Qinghai na kwenye eneo la chanzo cha pamoja cha mito mitatu ya Changjiang, Huanghe na Lancangjiang linaloitwa "Sanjiangyuan" mkoani humo, inaathiri moja kwa moja maisha ya nusu ya watu kote duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, watu na serikali ya China katika ngazi mbalimbali wamekuwa wanatumia raslimali nyingi katika kazi ya kushughulikia na kuhifadhi mazingira ya sehemu hizo, na juhudi hizo zimeleta mabadiliko dhahiri.

Sehemu inayojiendesha ya watibet ya wilaya ya Yushu iko katikati ya sehemu hifadhi ya taifa ya Sanjiangyuan. Ikiwa ni njia muhimu inayounganisha mikoa ya Tibet, Sichuan na mji wa Xining, sehemu hiyo ina mbuga nyingi za malisho kwa ajili ya wanyama na hakuna dohani ndefu wala kelele za mashine hazisikiki, vinavyoonekana tu ni milima, mbuga, mito na maziwa.

"kaka, usitupe takataka ovyo, kwani italeta madhara makubwa kwa sehemu yetu ya Sanjiangyuan."

Wasikilizaji wapendwa, ulikuwa unasikiliza mazungumzo kwenye mtaa wa Yushu. Takataka alizotaja mwanafunzi huyo wa shule ya msingi, ni mifuko ya plastiki inayotumika mara kwa mara katika maisha yetu, pia zinaitwa "takataka nyeupe". Takataka hizo zinaleta madhara makubwa kwa chanzo cha Sangjiangyuan kwenye sehemu ya Yushu. Ili kutatua tatizo hilo, mwaka 2004 serikali ya sehemu hiyo ilitoa kanuni ya kupiga marufuku matumizi ya bidhaa za plastiki zinazotupwa baada ya kutumiwa. Kanuni hiyo inapiga marufuku matumizi ya bidhaa za plastiki zinazotupwa baada ya kutumiwa vikiwemo visanduku vya chakula na mifuko ya plastiki, na kuagiza kikundi cha upimaji na usimamizi wa mazingira kutekeleza kanuni hiyo na kutoa adhabu kali kwa vitendo vinavyokiuka kanuni hiyo kwenye sehemu hiyo. Hii ni kanuni ya kwanza iliyotolewa kuhusu suala hilo kote nchini China.

Naibu mkurugenzi wa idara ya hifadhi ya mazingira ya wilaya ya Yushu anayeshughulikia kazi kuondoa uchafuzi Bw. Ma Chengde alisema, uchumi wa sehemu ya Yushu kwa kiasi kikubwa unategemea kazi za kushughulikia bidhaa na mazao ya kilimo, kwa hivyo kazi ya hifadhi ya mazingira ya asili imewekewa mkazo na serikali ya huko. Sehemu ya Yushu ikiwa ni sehemu ya katikati ya eneo la Sanjiangyuan, inapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kushughulikia uchafuzi wa namna hiyo. Bw. Ma Chengde alisema:

"mwanzoni ilikuwa ni vigumu kutekeleza kanuni hiyo, kwa kuwa watu wengi walikuwa bado hawaielewi. Walikuwa wanaona kuwa miji mikubwa kama Beijing na Xining yote bado inaruhusu matumizi ya mifuko ya plastiki, kwa wilaya ya Yushu iliyoko mbali, kwa nini inapigwa marufuku kwa hatua kali namna hii? Hatua hiyo kwa kiasi fulani inaathiri maisha ya wakazi wa huku."

Ili kukabiliana na matatizo hayo, idara ya ujenzi na hifadhi ya mazingira ya sehemu hiyo imesaini makubaliano na maduka na idara ya utalii katika ngazi ya sehemu na wilaya, na kufanya shughuli za kueneza ufahamu kuhusu hifadhi ya mazingira kila baada ya muda kwenye shule, idara za serikali na jeshi. Mbali na hayo, sehemu hiyo pia inatangaza vipindi vya kuhifadhi mazingira kupita kituo cha televisheni cha huko mara moja kila wiki, na kwa lugha za Ki-han na Kitibet, ili kueneza ufahamu kuhusu hifadhi ya mazingira na kuinua mwamko wa kuhifahi mazingira kwa wakazi wa huko.

Aidha, idara husika pia zimeweka hatua halisi na kuimarisha usimamizi. Naibu mkurugenzi wa idara ya ujenzi na hifadhi ya mazingira Bw. Ma Chengde alisema:

"idara yetu pia imeweka hatua na sera mbalimbali, na kuagiza kazi kwa kila mtumishi na kila mtaa. Mwaka jana na mwaka juzi kilikuwa ni kipindi cha usimamizi wa jumla. Mpaka sasa hali ya jumla imetulia."

Katika miaka kadhaa tangu kanuni hiyo itolewe, mwamko wa uhifadhi wa eneo la Sanjiangyuan na kuondoa "takataka nyeupe" umewaingia mioyoni wakazi wa sehemu hiyo, na hatua mbalimbali pia zimeleta mabadiliko dhahiri. Katika soko la mboga la wilaya ya Jiegu, Mwandishi wetu wa habari alikutana na Bw. Wang aliyekuwa akinunua chakula, alipoulizwa kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki alieleza kuikubali hatua hiyo. Bw. Wang alisema:

"hatua hii ni nzuri kwa kuhifadhi mazingira, mifuko ya plastiki ina madhara kwa mazingira, basi sasa tunafunga chakula na mboga kwa kutumia magazeti."

Tarafa ya Batang katika wilaya ya Jiegu ni sehemu ya makazi ya wafugaji. Zamani mifuko ya plastiki ilikuwa inaonekana kila mahali kwenye mbuga za majani, takataka hizo zina hatari kubwa kwa mifugo kama ng'ombe na kondoo, na zinatishia usalama wa uzalishaji na maisha ya wafugaji hao. Mfugaji aliyeishi kwenye wilaya ya Batang kwa miaka zaidi ya 60 mzee Naimaqingmei alisema:

"zamani mifuko ya plastiki yenye rangi mbalimbali ilikuwa inaonekana kila mahali mbugani. Ng'ombe na kondoo wakiziona walikuwa wanakula, lakini mifuko hiyo hisagiki tumboni, hatimaye wanyama wengi walikuwa wanakufa. Nilikuwa nikifuga ng'ombe zaidi ya elfu moja, lakini nusu yao walikufa kutokana na sababu hiyo."

Shughuli za kuondoa uchafuzi mweupe zinanufaisha moja kwa moja wafugaji wa huko. Mzee Naima alifurahia hatua hizo, alisema:

"ninaunga mkono sera hiyo, kwani imetatua tatizo kubwa kwetu wafugaji, sasa hatuna wasiwasi tena wakati wa kufuga."

Wakati wa kushughulikia "uchafuzi mweupe", idara husika zimetambua kuwa, kuhifadhi mazingira ya viumbe kunahitaji kuinua mtizamo wa umma kuhusu shughuli hiyo. Kuhusu hali hiyo, serikali ya wilaya ya Yushu imeweka mkazo katika kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira, hasa kwa watoto, ili kubadilisha mtizamo kwa kizazi kimoja. Katika shule ya msingi ya Hongqi ya huko, kipindi kimoja au vipindi viwili kuhusu hifadhi ya mazingira vinafundishwa kila wiki, na ofisi ya elimu ya siasa ya shule pia inafanya mara kwa mara shughuli za kuwashirikisha wanafunzi kuokota takataka kwenye uwanja wa mashindano ya farasi, mbuga na sehemu nyingine ambazo watalii wanakusanyika, au kuwapeleka wanafunzi kila baada ya muda kwenye maonesho ya picha na michoro kuhusu hifadhi ya mazingira.

Kutokana na kuimarika kwa vipindi vya hifadhi ya mazingira, shule ya msingi ya Hongqi inawachagua wanafunzi wanaojitokeza katika shughuli hiyo kuwa "walinzi wadogo wa mazingira". Kila ifikapo sikukuu na siku za mapumziko, walinzi hao wanaenda pamoja na watumishi wa idara ya usimamizi wa mambo ya mji kufanya shughuli za kueneza ufahamu wa hifadhi ya mazingira mitaani, kueleza umuhimu wa hifadhi ya mazingira kwa wapita njia. Hii ndiyo sauti mliyoisikia mwanzo wa kipindi hicho.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-10