Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-10 16:56:27    
Kijiji cha Najiaying cha watu wa kabila la Wahui mkoani Yunnan

cri

Kijiji cha Najiaying cha tarafa ya Nagu kiko kusini magharibi mwa mkoa wa Yunnan, kijiji hicho kina historia ndefu na kumewahi kuwa na watu maarufu wengi kizazi baada ya kizazi, wakiwemo profesa Nazhong wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing, ambaye pia ni mtaalamu maarufu wa historia ya lugha ya kiarabu aliyepewa tuzo ya kimataifa ya Sharjah la utamaduni wa kiarabu na Shirika la Elimu, Sayansi, na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, mtafsiri maarufu Bw. Na Xun, na maimamu maarufu zaidi ya 400. Aidha, watu wa kijiji hicho wanadumisha umaalumu wa dini ya kiislamu. Kila siku adhana inasikika kwenye kijiji cha Najiaying kuwaita watu kufanya ibada. Hivi sasa katika kijiji hicho, kuna familia zaidi ya 700 za waumini wa dini ya kiislamu. Mzee mwenye umri wa miaka zaidi ya 70 Bw. Na Jiarui alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, watu wanaoishi kwenye kijiji hicho wanaona fahari sana, kwa kuwa kijiji hicho kilianzishwa na mjukuu wa mtume Mohammed. Bw. Na Jiarui alisema,

"Tarafa ya Nagu ilianzishwa mwaka 1290, wakati huo kulikuwa na jenerali mmoja aliyeitwa Nashulu, alitumwa kwenye sehemu hiyo kuwa jemadari wa jeshi. Yeye ndiye mjukuu wa mtume Mohammed."

Bw. Na Jiarui alisema janerali Nashulu alikuwa na watoto wanne, kati ya hao watatu walikwenda nao kwenye sehemu moja yenye mandhari nzuri mkoani Yunnan na kujenga nyumba, baadaye sehemu hiyo ikawa kijiji cha Najiaying. Hivi sasa ni miaka zaidi ya 700 imepita, na waislamu wa kijiji hicho wanaendelea kudumisha mila na desturi zao katika sehemu mbalimbali, zikiwemo chakula, makazi, harusi na mazishi. Mkuu wa Taasisi ya Msahafu wa ya kiislamu ya kijiji cha Najiaying Bw. Ma Jiankang alisema,

"Waislamu wa kijiji cha Najiaying hawapendi kuandaa vyakula vingi kupita kiasi kwa wageni kama wanavyofanya wachina wengine, hata kwenye harusi, wanaandaa aina nane tu za vyakula."

Vijana wa kijiji hicho wakitaka kuoana ni lazima wawe wachumba kwanza, ama sivyo watalaumiwa na watu. Muda kati ya uchumba na kufanya ndoa huwa mrefu, unaweza kuwa mwaka mmoja, au hata miaka mitano mpaka miaka minane. Katika sherehe ya harusi, bwana harusi anapaswa kuvumiliwa mashambulizi ya kutupiwa kwa matope yaliyochanganywa kwa maboga na mayai, mashambulizi hayo yanaashiria familia hiyo mpya itapata maisha bora, na bibi harusi lazima avae nguo zinazofaa na kuvaa shela, asipofunikwa shela, imamu wa msikiti atakataa kufungisha ndoa.

Ili kuwafahamisha zaidi waandishi wetu wa habari kuhusu nguo ya harusi ya kiislamu ya kijiji cha Najiaying, Bw. Ma Jiankang aliwaonesha duka moja la kukodisha nguo hizo. Alisema,

"Duka hilo linanunua nguo kutoka nchi za Malaysia, Singapore na Saudi Arabia. Hii ni biashara, pia ni utamaduni, inalingana na nia ya dini yetu ya kiislamu."

Tukizungumzia dini ya kiislaamu ni lazima tutaje misikiti ya kijiji cha Najiaying. Kuna misitiki miwili kwenye kijiji cha Najiaying, yaani Msitiki wa Najiaying na Msitiki wa Wanawake wa Najiaying. Wa kwanza ni sehemu wanaposwali waislamu wanaume, wa pili ni sehemu mwingine wanaswali waislamu wanawake wa kijiji hicho. Wakati ukifika, waislamu wote wa kijiji hicho wazee, watoto au vijana, wanawake au wanaume wataingia kweye misikiti hiyo miwili kuswali.

Msikiti wa Najiaying ni msikiti mkubwa kabisa mkoani Yunnan. Msikiti huo wenye minara minne yenye urefu wa mita 72 ulizinduliwa rasmi tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 2004, una eneo la mita za mraba elfu kumi, na watu zaidi ya 3,000 wanaweza kuswali kwa wakati mmoja kwenye msikiti huo. Bw. Ma Jiankang alieleza kuwa, ujenzi wa msikiti huo uligharimiwa zaidi ya renminbi yuan milioni 20, fedha hizo zote zilichangiwa na wakazi wa kijiji cha Najiaying. Alisema,

"Zamani minara ya msikiti huo haikuwa mizuri, baadaye tuliirekebisha kutokana na ramani ya msikiti wa malaysia. Sasa msikiti huo una mtindo wa kiarabu na kuwavutia watu."

Msikiti wa Wanawake ulikuwa msikiti wa zamani wa Najiaying, unaweza kuwapokea watu karibu elfu kumi. Ili kujenga Msikiti mpya wa Najiaying, msikiti huo ulihamishiwa kwenye sehemu ya mashariki na kubadilishwa kuwa msikiti wa wanawake. Wakati waandishi wetu wa habari walipoangalia msikiti huo mzuri, walivutiwa na mwislamu mmoja mwanamke. Bibi huyo aliwaambia jina lake ni Ma Yunxiu, anatoka sehemu inayojiendesha ya Weiwuer ya mkoa wa Xinjiang, na sasa ni mwalimu wa lugha ya kiarabu na elimu ya dini katika kijiji hicho. Alipoulizwa kwa nini ameondoka nyumbani kwake na kwenda kijiji cha Najiaying, alisema,

"Zamani niliwahi kuambiwa habari kuhusu kijiji hiki, nilitaka kuja kuangalia, kwa kuwa waislamu wa Xinjiang hasa watu wa kabila la Wauygur, hawana umaalumu wa waislamu wa kabila la Wahui kama watu wa kijiji hiki. "

Kutokana na athari ya nidhamu ya dini ya kiislamu, na mila na desturi za wachina, waislamu wa kijiji cha Najiaying wanaishi maisha mazuri yenye masikilizano.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-10