Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-10 20:36:16    
Mapishi ya mchele unaonata na nyama ya kuku kwenye majani ya yungiyungi

cri

Mahitaji:

Majani sita ya yungiyungi, mchele unaonata gramu 500, kamba mwakaje gramu 100, nyama ya kuku gramu 50, uyoga gramu50, chumvi kijiko kimoja, sukari vijiko viwili, pilipili manga vijiko viwili, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, wanga vijiko viwili

Njia:

1.osha majani ya yungiyungi, weka mchele unaonata kwenye maji kwa saa moja, halafu upakue. Washa moto, mimina maji kwenye sufuria, weka kamba-mwakaje kwenye maji korogakoroga, wapakue. Pia weka vipande vya nyama ya kuku na uyoga kwenye maji joto, korogakoroga, vipakue.

2 washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia kamba-mwakaje, vipande vya nyama ya kuku, uyoga, korogakoroga, tia chumvi, sukari, pilipili manga na mafuta ya ufuta, korogakoroga, tia maji ya wanga, korogakoroga, Vipakue. Chemsha mchele unaonata kwa mvuke kwa saa moja, halafu koroga pamoja na chumvi, sukari, mafuta ya ufuta, maji na mafuta, korogakoroga.

3 weka mchele unaonata kwenye jani la yungiyungi, halafu weka vitu vilivyokorogwa kwenye hatua ya tatu, halafu weka mchele unaOnata tena, funga jani hilo kuwa mraba, endelea kufanya hivyo, mwisho weka kwenye sufuria chemsha kwa mvuke kwa dakika 10. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.