Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-12 16:46:26    
Mazungumzo kati ya Russia na Marekani yafuatiliwa

cri

Mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa ulinzi kati ya Russia na Marekani yanafanyika tarehe 12 huko Moscow, mada ya mazungumzo hayo ni suala ya usalama wa kimkakati ambalo linahusisha mfumo wa kukinga makombora unaopangwa kuwekwa na Marekani barani Ulaya, "makubaliano kuhusu nguvu za kawaida za kijeshi barani Ulaya" na masuala ya Iran na Kosovo. Kwa hiyo mazungumzo hayo yanafuatiliwa sana.

Mazungumzo hayo yanafanywa kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa Russia na Marekani wakati walipokutana kwenye jimbo la Maine nchini Marekani mwezi Julai mwaka huu, na hali ya mazungumzo hayo itaripotiwa kwa marais wa nchi hizo mbili.

Tokea mwaka huu Marekani imeharakisha mpango wa kuweka mfumo wake wa kukinga makombora barani Ulaya, kwa mujibu wa mpango huo Marekani itaweka mfumo wa rada wa kukinga makombora nchini Jamhuri ya Czech, na kuweka mfumo wa kuzuia makombora nchini Poland. Pamoja na hayo Marekani imeshirikisha Bulgaria, Romania na Ukraine kwenye mfumo huo. Marekani inatangaza kuwa kupanga mfumo huo ni kwa ajili ya kulinda usalama wa Ulaya, na haulengi nchi yoyote inayoheshimu sheria ya kimataifa ya usalama, bali ni kwa ajili ya kukinga mashambulizi ya makombora kutoka nchi kama Iran. Kutokana na hatua hizo za Marekani, mwezi Aprili rais Vladimir Putin wa Russia kwenye ripoti yake ya kazi za serikali alitangaza kusimamisha kwa muda utekelezaji wa "makubaliano kuhusu nguvu za kawaida za kijeshi barani Ulaya", na alipendekeza kufanya majadiliano kuhusu mfumo huo wa Marekani ndani ya jumuiya ya usalama ya Ulaya. Russia inatumai kuwa nchi za Ulaya zitatafakari kwa makini mpango wa kuweka mfumo huo wa kukinga makombora barani Ulaya. Kwenye mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane uliofanyika mwezi Agosti mwaka huu, rais Putin alimshauri rais George Bush wa Marekani kujenga kituo cha rada cha pamoja nchini Azerbaijan badala ya mfumo wa rada unaopangwa kuwekwa na Marekani nchini Jamhuri ya Czech. Tarehe 18 Septemba, wataalamu wa nchi tatu za Russia, Marekani na Azerbaijan walitembelea kwenye kituo cha rada kilichokodiwa na Russia nchini Azerbaijan, na wataalamu wa Russia na Marekani waliwasilisha ripoti yao kuhusu hali ya kituo hicho kwa wajumbe wa mazungumzo hayo ili kujadili kutumia kwa pamoja kituo hicho cha rada. Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kukubali kufanya majadiliano ili kutafuta uwezekano wa kutumia kwa pamoja kituo hicho.

Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov hivi karibuni alipogusia mazungumzo hayo ya mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi kati ya Russia na Marekani alisisitiza kuwa, baada ya Marekani kupanga kuweka mfumo wa kukinga makombora barani Ulaya kwa upande mmoja, Russia imetangaza mara nyingi msimamo wake na kutumai kuwa Marekani itajibu ushauri wa rais Putin ili kuimarisha utulivu wa kimkakati na isisababishe ujasiri mpya wa hatari.

Wachambuzi wanaona kuwa hivi leo duniani kuna nchi moja yenye nguvu kubwa kupita kiasi na nchi chache zenye nguvu, ingawa Russia na Marekani zinatofautiana katika masuala mengi lakini zinajitahidi zisigongane moja kwa moja. Hata hivyo kutokana na mfumo wa kukinga makombora, masuala ya Kosovo na maslahi ya kimsingi ya Russia, Russia haitarudi nyuma kirahisi na Marekani pia haiwezi kirahisi kuacha mpango wake kwa sababu ya upinzani wa Russia. Kwa hiyo mapambano kati ya nchi hizo mbili kuhusu mfumo wa kukinga makombora yataendelea. Mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa ulinzi kati ya nchi hizo mbili yameleta fursa ya kuelezana misimamo na kujitahidi kuufanya kila upande urudi nyuma.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-12