Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-15 15:59:21    
Maingiliano ya kiutamaduni ya nchi tatu, China, Japan na Korea ya Kusini yazidi kuimarika

cri

Huu ni mwaka wa 35 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan na uanzishwe na ni mwaka wa 15 tangu uhusiano kati ya China na Korea ya Kusini uanzishwe. Tamasha la tisa la sanaa la Asia lililofanyika hivi karibuni katika mji wa Nantong, mashariki mwa China, lilikuwa ni jukwaa kubwa la maingiliano ya kiutamaduni ya nchi tatu, China, Japan na Korea ya Kusini.

China, Japan na Korea ya Kusini ni nchi jirani, maingiliano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo tatu yana historia ndefu. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo sambamba na kuimarisha maingiliano ya kiuchumi zinazidi kuimarisha maingiliano ya kiutamaduni, hususani katika fani ya filamu, michezo ya sanaa na utamaduni wa chakula. Maingiliano yanayoshughulikiwa na serikali pia yamekuwa mengi.

Mkuu wa kundi la opera la Korea ya Kusini Bw. Kim Jong Hee alisema, mapema miaka kumi iliyopita kundi lake lilianza ushirikiano wake na China na Japan, na alikuwa na matumaini kuwa nafasi za mawasiliano ya kiutamaduni kati ya nchi tatu zitakuwa nyingi zaidi. Alisema,

"Tumeanza kuwa na mawasiliano ya kiutamaduni kati yetu na China na Japan mapema miaka kumi iliyopita, niliwahi kushiriki kwenye maonesho ya michezo yetu mara nyingi. Nashughulika na mawasiliano ya maonesho ya michezo ya kuigiza, nina matumaini kuwa tutaweza kucheza michezo ya kuigiza na dansi kwa kushirikiana na wasanii wa China na Japan."

Utamaduni ulio karibu sawa na nchi hizo tatu kuwa karibu kijiografia, inafanya maingiliano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo yasiweze kukatika, na utamaduni ulio karibu unawasogeza karibu watu wa nchi hizo tatu.

Katika miaka ya 80 mchezo wa kuigiza wa Japan unaoitwa "Tuhuma ya Damu" ulipooneshwa kwenye televisheni nchini China uliwavutia watazamaji wengi. Katika miaka ya karibuni michezo mingi ya kuigiza ya Korea ya Kusini imekuwa inaoneshwa kwenye televisheni nchini China, mchezo wa televisheni unaoitwa "Kito ndani ya Kasri" ulipata rekodi mpya ya idadi kubwa ya watazamaji wa televisheni. Michezo ya televisheni iliyopigwa kwa ushirikiano wa nchi za China, Korea ya Kusini na Japan kama vile "Beijing, Mji wa Unaonivutia", "Usiku Mjini Shanghai" na michezo mingine ambayo sio tu ilioneshwa katika majumba ya filamu na vituo vya televisheni nchini China, bali pia iliingia kwenye soko la filamu nchini Japan na Korea ya Kusini. Matengenezo ya filamu za televisheni kwa ushirikiano hatua kwa hatua yameendelea kuwa matengenezo ya uwekezaji wa pamoja toka mwanzo ambapo China ilitoa fedha na nchi nyingine ziolitoa waigizaji na kutengeneza. Kundi la Wen Guang la Uenezi wa Utamaduni mjini Shanghai lina ushirikiano huo na Japan na Korea ya Kusini. Mwongozaji wa michezo ya televisheni wa kundi hilo Bw. Teng Junjie anaona kuwa, kama kukiwa na juhudi kutakuwa na fursa nyingi za ushirikiano na kupata maendeleo kwa pamoja. Alisema,

"Mwanzoni Japan na Korea ya Kusini zilishirikiana nasi kwa kununua filamu zetu mfululizo za televisheni, lakini baadaye kutokana na mahitaji makubwa ya soko, zilitoa mapendekezo ya kutengeneza filamu kwa ushirikiano. Huu ndio ushirikiano wenyewe ambao juhudi zikifanyika kutakuwa na maendeleo, na baadaye hali ya kufukuzana itatokea."

Bw. Teng Junjie aliwahi kuongoza vikundi vya michezo ya sanaa kwenda Japan na Korea ya Kusini. Aliwaambia waandishi wa habari kwamba kutokana na asili ya namna moja ya utamaduni, utamaduni wa jadi wa China unakubalika kwa Wajapan na wa Korea ya Kusini.

Pamoja na hayo, serikali ya China inahamasisha sana ushirikiano huo wa kiraia, na huku inaunga mkono ushirikiano huo kupitia maingiliano ya kiserikali. Shughuli muhimu katika tamasha hilo ilikuwa mkutano wa mawaziri wa utamaduni wa nchi tatu, kwenye mkutano huo wameafikiana kuhusu namna ya kuimarisha maingiliano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo tatu. Waziri wa utamaduni wa China Bw. Sun Jiazheng alisema,

"Mawasiliano baina ya serikali yamepanua njia ya maingiliano ya kiraia, na yameweka msingi imara wa maingiliano hayo katika sekta za utamaduni na uchumi kati ya China na Korea ya Kusini."

Bw. Sun Jiazheng anaona kuwa hapo zamani maingiliano yalitiliwa mkazo kwenye kufahamiana tu kati ya watu wa nchi tatu, lakini katika siku za mbele kipaumbele kitakuwa ni kwenye maingiliano ya mambo ya kiutamaduni, na kuyafanya maingiliano hayo yaunganishe mioyo ya watu wa nchi tatu na kuweka msingi imara wa urafiki wa kizazi baada ya kizazi miongoni mwa wananchi wa nchi tatu.

Mkutano wa mawaziri wa utamaduni wa nchi tatu ulipitisha "Taarifa ya Nantong" na kuanzisha mpango wa kufanya mkutano wa mawaziri wa utamaduni wa nchi tatu kila baada ya muda fulani, na umeamua kwamba mwakani mkutano kama huo utafanyika nchini Korea ya Kusini. Waziri wa utamaduni wa Japan Bw. Aoki Tamotsu alifurahia sana ushirikiano huo na alisema Japan imeandaa hatua za kustawisha maingiliano hayo. Alisema,

"Naona mkutano huo ni muhimu sana, tunatamani kupanua ushirikiano, ni furaha yetu kama michezo yetu ya sanaa ikiweza kuoneshwa nchini China, na kuimarisha zaidi maingiliano ya kiutamaduni na China."

Tamasha hili ni pamoja na maonesho ya michezo ya sanaa, maonesho ya sanaa ya maandishi kwa brashi ya wino na maonesho ya utamaduni wa jadi. Katika siku za baadaye watu wa nchi tatu watapata kuona shughuli nyingi zaidi za utamaduni na watakuwa karibu zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-15