Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-17 16:52:51    
Chuo kikuu cha Xinjiang

cri

China ni nchi yenye makabila mengi, mbali na kabila la Wahan, kuna makabila mengine 55 madogomadogo. Shughuli za elimu kwenye sehemu za makabila madogomadogo siku zote zinatiliwa maanani na serikali ya China. Leo tunawatembeza kwenye chuo kikuu cha mkoa unaojiendesha wa Wauyghur wa Xinjiang.

Mkoa unaojiendesha wa Wauyghur wa Xinjiang uko kwenye mpaka wa kaskazini magharibi mwa China, mkoa huo mwenye eneo la kilomita za mraba zaidi ya laki 1.6 ni mkoa mkubwa kabisa nchini China. Mkoa huo unapakana na nchi za Mongolia, Russia, Kazakhstan, Tajikistan, Kyrgyzstan, Afghanistan, Pakistan na India. Makabila madogomadogo yakiwemo makabila ya Wauyghur, Wakazak, Wahui, Wakerkez, Wamongolia, Watajik na Wasibe yanachukua asilimia 60 ya idadi ya wakazi wa mkoa huo, mkoa huo ni mmoja ya mikoa inayojiendesha ya makabila madogomadogo nchini China.

Chuo kikuu cha Xinjiang kilichoko huko Urumqi, mji mkuu wa mkoa wa Xinjiang ni chuo kikuu muhimu kinachoandaa wataalamu wa makabila mbalimbali nchini China. Hivi sasa chuo kikuu cha Xinjiang kina wanafunzi zaidi ya elfu 23, na nusu kati yao wanatoka makabila madogomadogo. Naibu mkuu wa chuo kikuu hicho Bw. Hu Xiaofan alisema:

"Chuo kikuu siku zote zinatilia maanani elimu ya wanafunzi wa makabila madogomadogo, na kimeandaa wasomi na viongozi wengi hodari. Chuo chetu chenye raslimali nyingi za walimu na miundombinu kamili ya elimu hakika kinaweza kuandaa wataalamu wanaohitajika katika ujenzi wa uchumi na jamii ya mkoa huo."

Chuo kikuu cha Xinjiang kilichoanzishwa mwaka 1924 ni kimoja kati ya vyuo vikuu vyenye historia ndefu nchini China. Mwanzoni kilikuwa kinatiwa shule maalum ya lugha ya Kirusi ya siasa na sheria ya Xinjiang. Mwaka 1935 shule ilibadilishwa jina kuwa chuo cha Xinjiang. Baada ya China mpya ianzishwa, chuo hicho kilipewa jina la Chuo kikuu cha Xinjiang. Baada ya China kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, chuo kikuu hicho kimechukuliwa kuwa chuo kikuu muhimu cha taifa cha China na kimepata maendeleo makubwa. mwishoni mwa karne iliyopita, chuo kikuu cha Xinjiang kiliidhinishwa kwa hatua ya mwanzo na mradi wa taifa wa kujenga vyuo vikuu mia moja muhimu katika karne ya 21, kiliungana na chuo cha teknolojia cha Xinjiang na kuwa chou kikuu kipya cha Xinjiang. Baada ya hapo, chuo kikuu cha Xinjiang kimekuwa chuo kikuu cha jumla chenye taaluma za fasihi, uhandisi, uchumi, usimamizi, sheria, historia na falsafa.

Mkoa wa Xinjiang una wanafunzi wengi wa makabila madogomadogo, katika mtihani wa taifa wa kujiunga na vyuo vikuu, wanatumia lugha tofauti. Hivyo mkoani humo, wanafunzi wa mtihani huo wanagawanyika kwa makundi matatu kutokana na lugha wanaoitumia katika mtihani. Wanafunzi wanaweza kuchagua kutumia lugha ya Kichina au lugha zao za kikabila katika mtihani huo. Kwa kuwa shule za msingi na za sekondari kwenye baadhi ya sehemu mkoani humo zinafundisha kwa lugha ya Kichina, wanafunzi wa makabila madogomadogo wanaosoma katika shule hizo wamejifunza vizuri lugha hiyo; kwa kundi jingine ambalo wanafunzi wa waHan wanaopenda lugha za makabila madogomadogo na utamaduni wake, wanaweza kutumia lugha za kikabila katika mtihani huo wa taifa. Kutokana umaalum huo wa Xinjiang, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wa makabila yote madogomadogo wanaweza kupata elimu ya juu, wanafunzi hao wanaweza kujiunga na vyuo vikuu kwa alama za chini zaidi kuliko wanafunzi wa kabila la waHan kwenye mtihani huo.

Lakini kuanzia mwaka 2003, mbali na masomo ya utafiti wa lugha za makabila, chuo kikuu hicho kimaanza kufundisha kwa kichina tu. Hali hiyo inamaanisha kuwa wanafunzi wa makabila madogomadogo walioshirki kwenye mtihani wa taifa kwa lugha zao za kikabila kama wakisoma masomo licha ya utafiti wa lugha za kikabila, wanapaswa kuwa na uwezo wa kusikiliza, kusema, kusoma na kuandika lugha ya Kichina. Bw. Hu Xiaofan alisema, chuo kikuu cha Xinjiang kimeandalia njia mbalimbali za ufundishaji ili kuwapa wanafunzi hao urahisi wa kupewa elimu.

Kuhusu hali hiyo, kulikuwa na wasiwasi kuwa kufundisha kwa lugha ya kichina peke yake kwenye chuko kikuu ni kama kutoheshimu lugha na utamaduni wa makabila mengine. Bw. Hu Xiaofan alieleza kuwa, lugha ni daraja la mawasiliano katika jamii, ili kuzisaidia vizuri makabila madogo kuharakisha ujenzi wa uchumi na jamii, ina haja ya kufundisha kwa lugha ya Kichina. Bw. Hu Xiaofan alisema:

" kama chuo chetu bado kinafundisha kwa lugha ya Kiuyghur kama ilivyokuwa zamani, kwanza tunahitajika kutafsiri sayansi na teknolojia za kisasa kwa lugha ya Kiuyghur, lakini kazi hiyo itachukua muda wa miaka kadha hata kumi. Lengo letu la kuchagua njia hii ya ufundishaji ni kuhimiza ustawi wa pamoja wa makabila madogomadogo nchini China."

Katika chuo kikuu cha Xinjiang, wanafunzi pia wana shughuli nyingi za burudani baada ya masomo. Wanafunzi wa makabila madogomadogo wanashiriki mara kwa mara kwenye shughuli za "daraja la lugha ya Kichina", na kuzungumza na wanafunzi wa kabila la Han ili kuinua uwezo wao wa Kichina. Kijana Abuduwaili kutoka kabila la Uyghur anasomo shahada la pili la l kemikali ya fizikia katika chuo kikuu hicho. Alisema, baada ya masomo anashiriki mara kwa mara kwenye michezo na utembezi pamoja na wenzake wa Wahan, uhusiano kati ya wanafunzi wa makabila madogomadogo ni mzuri sana. Bw. Abuduwaili alisema:

"Elimu ya muungano wa taifa ya Xinjiang imefanyika vizuri. Kwa mfano, mie nina marafiki wengi zaidi wa Wahan hata kuliko Wauyghur."

Mkuu wa chuo kikuu cha Xinjiang Bw. Hu Xiaofan alisema, asilimia 18 ya wanafunzi wa chuo kikuu hicho wanatoka sehemu za ndani za China. Chuo kikuu hicho kitampa kila mwanafunzi mpya kitabu cha maelezo kuhusu dini, mila na desturi za makabila mbalimbali na mambo anayopaswa kufuatiliwa katika mawasiliano, ili kuisha pamoja bila mikwaruzano.

Kutokana na mpango wa jumla wa kimkakati wa maendeleo ya Chuo kikuu cha Xinjiang, ifikapo mwaka 2010, chuo kikuu hicho kitakuwa chuo kikuu cha chenye umaalum ambacho kinachukua nafasi za mbele vya jumla nchini China na pia kina athari kubwa katika kanda ya Asia ya Kati.