Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-17 16:36:14    
Mapishi ya ngisi na kuku

cri

Mahitaji

Ngisi gramu 50, kuku mmoja, pilipili hoho gramu 10, pilipili mboga gramu 10, mchuzi wa sosi vijiko viwili, sukari kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, pilipili manga kijiko kimoja, wanga vijiko viwili, kiasi kidogo cha vitunguu maji, tangawizi, na giligilani.

Njia

1. kata kuku awe vipande vipande, koroga pamoja na mchuzi wa sosi, sukari, chumvi na wanga.

2. osha ngisi halafu umkate awe vipande. Kata pilipili hoho, pilipili mboga, vitunguu maji na tangawizi ziwe vipande.

3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia vipande vya pilipili hoho, vitunguu maji na tangawizi, korogakoroga tia vipande vya kuku korogakoroga, halafu mimina maji, baada ya kuchemka punguza moto, baada ya dakika 15, tia vipande vya mboga na ngisi korogakoroga, mimina mchuzi wa sosi, tia chumvi, pilipili manga, korogakoroga halafu tia giligilani, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.