Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-17 18:56:57    
Shirika la chakula duniani laadhimisha siku ya chakula duniani

cri

Tarehe 16 mwezi Oktoba ni siku ya chakula duniani. Siku hiyo shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, lilifanya shughuli katika makao makuu yako yake mjini Rome kuadhimisha siku ya 27 ya chakula duniani. Mkuu wa shirika hilo Bw. Jacques Diouf, rais Horst Koehler wa Ujerumani na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania walishiriki kwenye shughuli za maadhimisho na kutoa hotuba wakisisitiza kuwa "haki ya kupata chakula" ni haki ya kimsingi ya binadamu.

Shirika la Chakula duniani FAO lilianzishwa tarehe 16 mwezi Oktoba mwaka 1945, na ni moja ya mashirika maalumu makubwa ya mfumo wa Umoja wa Mataifa. Jukumu lake ni kujenga dunia yenye usalama wa chakula. Katika miaka ya 70 ya karne iliyopita, dunia ilikumbwa na mgogoro wa chakula, mwaka 1979 mkutano mkuu wa 20 wa FAO wa Umoja wa Mataifa ulifanya uamuzi wa kuifanya siku ya kuasisiwa FAO kuwa "siku ya chakula duniani", ili kutaka jumuiya ya kimataifa izingatie sana uzalishaji wa kilimo na usalama wa chakula. Kauli-mbiu ya siku ya 27 ya chakula duniani kwa mwaka huu ni "haki ya kupata chakula", ambayo inaonesha jumuiya ya kimataifa inatambua umuhimu wa haki za binadamu katika kutokomeza njaa na umaskini. Mkuu wa FAO, Bw. Diouf alipotoa hotuba kwenye sherehe ya maadhimisho, alisema,

"Ndiyo kwa ajili ya kujenga dunia ya usawa zaidi, kauli-mbiu ya siku ya chakula ya mwaka huu ni haki ya kupata chakula. Kiasi cha chakula kinachozalishwa kwenye dunia yetu vinaweza kabisa kukidhi mahitaji ya watu. Lakini katika usiku wa leo, bado kuna wanaume, wanawake na watoto milioni 854 wanalala na njaa. Kwa hiyo mahitaji ya binadamu yanapaswa kuchukua nafasi ya kwanza katika ufuatiliaji wetu, sera zetu na vitendo vyetu."

Tokea mkutano wa wakuu wa nchi wa chakula duniani ufanyike mwaka 1996, FAO na serikali za nchi mbalimbali zinajitahidi kuwania "haki ya kupata chakula". Haki hiyo ya kimsingi ya binadamu imepata kutambuliwa. Hivi sasa nchi 156 zimeidhinisha "mkataba wa kimataifa wa haki za uchumi, jamii na utamaduni", kutambua haki ya kupata chakula ni wajibu wenye nguvu ya kisheria. Katika hotuba yake, Bw. Diouf alisisitiza,

"Kumhakikishia kila mtu apate chakula cha kutosha ni matakwa ya utu, tena ni uwekezaji unaoleta manufaa makubwa: hii ni kutimiza aina moja ya haki za kimsingi zisizoweza kukosekana. Dunia sasa ina mbinu ya kutimiza haki ya kupata chakula, na sasa ni wakati wa vitendo!"

Rais Koehler wa Ujerumani aliyekuwa mtaalamu wa uchumi, katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa kupambana na njaa. Alisema, njaa siyo bahati mbaya isiyoweza kubadilishwa, bali ni tatizo linaloweza kutatuliwa kwa sera sahihi, hivyo nchi zinazoendelea zinatakiwa kuweka usalama wa chakula katika nafasi ya mbele kabisa. Alisema,

"Jukumu muhimu la mapambano dhidi njaa ni kuhawakikisha watu wanaweza kupata chakula cha kutosha kwenye ardhi yao au ardhi ya karibu. Hii inataka nchi zinazoendelea kuendeleza kilimo kwenye msingi wa kuwa na idara za serikali zenye haki ya umilikaji, ufanisi wa kazi na mbinu ya uzalishaji. Lakini kwa bahati mbaya, zamani nchi za kusini mwa dunia, maendeleo yake ya kilimo hayakuendelezwa vizuri. Kazi iliyofanya Ulaya ni kutaka nchi zinazoendelea kulima zao moja tu la kusafirishwa nje. Kwa mfano, wakulima walilima zao la kakao kwa ajili ya soko la dunia, lakini hawapandi mihogo wanayoihitaji wao wenyewe. Kurudia makosa ya zamani ni kosa kubwa.

Takwimu za FAO zinaonesha, hivi sasa watu milioni 840 hawapati chakula cha kutosha, ambao milioni 800 ya watu hao wako katika nchi zinazoendelea, na nchi maskini kabisa na zilizokuwa nyuma kimaendeleo, ziko barani Afrika. Rais Kikwete wa Tanzania alisema,

"Hivi sasa watu 4,000 duniani wanakufa kutokana na kutokuwa na lishe bora na magonjwa mengine husika. Watu hao ni watu walionyang'anywa haki ya kupata chakula.

Mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu chakula duniani wa mwaka 1996 uliahidi kupunguza nusu ya idadi ya watu wenye matatizo makubwa ya chakula kabla ya mwaka 2015. Kauli mbiu ya "haki ya kupata chakula" ya siku ya chakula duniani, inataka serikali za nchi mbalimbali zizingatie zaidi haki ya kupata chakula, ambayo si rahisi kupuuzwa.